mimi sifungamani na upande wowote kati ya North korea na United States of America

falcon mombasa

JF-Expert Member
Mar 5, 2015
9,186
9,287
wakuu habari

moja kwa moja niende kwenye hoja. mimi kwa mtazamo wangu nimeamua kusimama upande wa wasiofungamana na upande wowote baina ya korea na marekani
sababu zilizopelekea msimamo wangu ni kutokana kutotabirika uwezo wa korea kaskazini endapo wataingia vitani na marekani kwakuwa korea kaskazini haina rekodi kubwa ya kupambana vita hivyo hakuna anaejua korea kuna nini.
suala la pili ambalo limenifanya kutofungamana na upande wowote ni suala la vikwazo, korea kaskazini ndio nchi inayoongoza kwa vikwazo lakin bado hii haijawa suluhu kuipoteza korea kwenye medani za mafanikio

Jambo lingine ni rekodi ya utiifu kati ya wanajeshi wa korea kaskazini na marekani, hadi sasa tumeshuhudia uvujishwaji mkubwa wa siri za usalama wa taifa la marekan lakini hatujasikia hata siku moja siri kutoka pyongyang zikavuja kizembe

Asanteni
 
Kutofungamana kwako kutaathiri vipi pande hasimu?
 
Nguruwe/Dampo akijifanya kuwafata face to face atakuisha. Kim co wa sport sport
Aah, wap yule mzushi tu anatishia nyau. Nadhan umeisahau marekan wale wana kampan kubwa mjomba hayuko peke yake. Yakija kuaanza, mashambuliz ya anga atashangaa na nyuklia yake anaeringishia watu
 
Ianze tu mana kuna ajira zitatengenezwa apo..watu tukawe masoldier us uko
 
Wakati sisi tukiendelea na ushabiki wetu wa vita hebu kwanza tuchambue watu mnafikiri N korea atapigwa siku moja tu na vita ikaisha hilo msahau vita inaweza kuchukua muda mrefu sana kingine N korea hana cha kupoteza alishatengwa na dunia muda mrefu japan na korea kusini hii vita inawahusu sana na Usa kawekeza sana huko je yuko tayari maslahi yake yashambuliwe? Japan na korea kusini wako tayari kupigwa nyuklia kwa sababu ya mjinga mmoja tu Donald Trump? Nyuma ya N korea hawa lazima wamuunge mkono Urusi china lazima wahusike hapo sasa ndiyo pananoga nauliza tena japan na korea kusini wako tayari kugeuzwa uwanja wa majaribio ya silaha ili hali Usa yeye atakuwa kwake anakunywa mvinyo hapana hatutaki vita sisi
 
Tunaipenda na kuheshimu sana USA lakini vita vya Asia Pacific vitakuwa vita vibaya sana kuwai kutokea Duniani KIM hato kubali kufa peke yake atakufa na watu

Inapofikia kipindi Police wa dunia ambae kila Taifa linamuogopa mpaka mataifa makubwa kama China,Russia wakati mwingine wanakuwa wapole mbele ya American Eagle lakini Kim au Korea kaskazini wamuogopi mfano leo IGP anakuja kumtamata mtuhumiwa lakini mtuhumiwa amwogopi akiambiwa kaa chini yeye anasimamia akiambiwa kaa kimya yeye anapiga kelele kama IGP inatakiwa ujiulize maswali matatu kichwan mwako
1 mtuhumiwa ni chizi
2 mtuhumiwa hana cha kupoteza na yupo tayali hata kufa

3 mtuhumiwa anawatu yuma yake ambao wapo tayali kumtetea au kupigana na ww ila walikuwa wanakutafutia sababu
Vita vya Nuclear havina mbabe au mwenye vifaa au uchumi mkubwa mshindi ni yule wa kwanza kubonyeza nuclear codes tu
 
wakuu habari

moja kwa moja niende kwenye hoja. mimi kwa mtazamo wangu nimeamua kusimama upande wa wasiofungamana na upande wowote baina ya korea na marekani
sababu zilizopelekea msimamo wangu ni kutokana kutotabirika uwezo wa korea kaskazini endapo wataingia vitani na marekani kwakuwa korea kaskazini haina rekodi kubwa ya kupambana vita hivyo hakuna anaejua korea kuna nini.
suala la pili ambalo limenifanya kutofungamana na upande wowote ni suala la vikwazo, korea kaskazini ndio nchi inayoongoza kwa vikwazo lakin bado hii haijawa suluhu kuipoteza korea kwenye medani za mafanikio

Jambo lingine ni rekodi ya utiifu kati ya wanajeshi wa korea kaskazini na marekani, hadi sasa tumeshuhudia uvujishwaji mkubwa wa siri za usalama wa taifa la marekan lakini hatujasikia hata siku moja siri kutoka pyongyang zikavuja kizembe

Asanteni
Saivi naona vita imekuwa na mashabiki kama mpira wa miguu bila kuwaza kwamba ili mtu ashinde inabidi watu wengi zaidi wauwawe na hasara zaidi ipatikane ndio ushindi sio jambo la kufurahia

Ila mpaka hapo wewe ni korea lakini lazima watashindwa coz hawana uchumi wa kushindana na hawa watu wa usA
 
Back
Top Bottom