Mimi si mla rushwa- Eliakim Maswi

Super Handsome

JF-Expert Member
Jul 16, 2013
3,846
6,439
Katibu Mkuu wa Kwanza kutamba kwamba rushwa kwake mwiko
.awataka watanzania kujitokeza katika uchimbaji na utafutaji gesi asilia
.asema waache kulalamika
.aahidi kuendelea kusimamia maslahi ya Taifa
.Wizara yake yaanda mkakati wa kuwakopesha wachimbaji wadogo wa madini nchini


Na Damas Makangale, MOblog
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Bw,.Eliakim Maswi mwishoni mwa juma alivunja ukimya na kutamka bayana kwamba wazawa wanaruhusiwa kuingia katika biashara ya kimataifa ya utafutaji na uchimbaji wa Gesi asilia nchini.


Akizungumza na MOblog katika mahojiano maalum baada ya kufunguka mkutano wa mwaka wa Chama cha Wafanyabiashara wa Madini na Nishati (Tanzania Chamber of Minerals and Energy) amesema kuna upotoshaji ukubwa kwamba serikali inazuia wazawa kufanya biashara ya utafutaji na uchimbaji wa Gesi asilia.


“Serikali ipo tayari kuzungumza na kuwapa vitalu baada ya kulipia wazawa wote wenye nia ya kuingia katika biashara hii ya kimataifa ya uchimbaji wa Gesi asilia hatuna matatizo na wazawa ambao wana nia ya kuingia katika biashara hii,” amesema
Maswi alilisitiza kwamba Mtanzania anapaswa kulipa Dola za kimarekani 700,000 ili apatie kitalu na ni bei ya chini tofauti na mwekezaji kutoka nje.


Alisisitiza kwamba Wizara ya Nishati na Madini ipo tayari kufanya kazi na wazawa katika sekta ya gesi asilia kwa sababu ufumbuzi wa madini hayo yataharakisha maendeleo ya Taifa katika Nyanja zote za uchumi.


Tukiharakisha uchimbaji wa gesi asilia itaongeza kasi ya kuondoa umasikini wa wananchi hasa katika maeneo ambayo gesi inapatikana,” aliongeza Maswi


Maswi amesema ingawa uchimbaji na utafutaji wa gesi asilia na utafiti (Exploration) kuhitaji mtaji mkubwa na wa muda mrefu ndiyo maana wizara ikaamua kupunguza gharama ya kitalu kwa wazawa ili kuwapa fursa murua ya kuingia katika biashara hiyo.


Kwa upande wa madini, Maswi amesema Wizara ya Nishati na Madini inaandaa mpango mkakati kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo nchini (TIB) ili waweza kukopeshwa na kuongeza mitaji katika biashara zao za madini nchini.


“tupo katika hatua za mwisho na uongozi wa Benki ya Maendeleo ya Taifa (TIB) ili waweze kuwakopesha wachimbaji wadogo wadogo wa madini nchini kwetu, wizara inawajali wazawa jamani alisisitiza,”


Wakati huo huo, hivi karibuni Rais wa Jakaya Kikwete alinukuliwa akisema kwamba maandalizi ya uchimbaji gesi nchini Tanzania yasichukue muda mrefu kwa sababu wananchi wanahitaji kuona manufaa ya Gesi asilia katika kipindi kifupi iwezekanavyo na kwamba, makadirio ya miaka kumi ni mingi sana.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameongeza kuwa, gesi asilia inayoendelea kugunduliwa nchini humo ni rasilimali muhimu na ni lazima itumike katika kuwatoa Watanzania katika umasikini na kwamba, ni lazima rasilimali hiyo ibadilishe maisha ya wananchi

source: Mo Blog!
 
Back
Top Bottom