"Mimi si Fisadi....."

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,526
1,530
Kwenye msiba wa familia moja iliojikusanya pale Dar na kwenda Hedaru kwa mazishi, palikuwa na watu kibao tangu Alhamisi ya April 17 2008 mpaka mazikoni.

Kama kawaida ya jamii zetu, ndugu jamaa na marafiki hujumuika kwenye shughuli.

Basi wakati wa nasaha, pakatolewa ukumbi na huyu jamaa baada ya kutambulishwa na kupewa fursa ya kuzungumza kutokana na umashuhuri wake akasema

"Bwana Yesu asifiwe.....Mimi ni ...mimi si Fisadi au Mwizi...kama....." EL
 
Nimeisikia habari hii; alienda hapo msibani na mchungaji akamtambua na kumpa ukumbi aseme maneno ya rambirambi na Lowassa akihisi anaangaliwa kwa "jicho baya" akaanza kubreak "the ice" kwa kusema kinyume na watu wengi wanavyosikia kuwa yeye ni fisadi kwa kweli yeye si fisadi ni mkristu tu, na akachomekea "Bwana asifiwe sana"... Sina uhakika kama alitoa pole yenyewe...
 
Duh....! Mzimu wa ufisadi unamfuata hadi msibani? Wengine basi wajifunze kwa hilo.
 
hahaha....EL na wenginewe wote, hiyo ni mizimu ya watoto wadogo waliokufa kwa ukosefu wa dawa, mama wajawazito waliopoteza maisha pamoja na walikufa barabarani kwa ajali za kuepukika iwapo ingechukuliwa hatua....
na bado
 
Mi napenda kujua kwa nini huyo mchungaji alimtambua Lowassa tu among all na kumpa hiyo nafasi?This perhaps could explain somethin here...
 
Siasa za Tanzania siku hizi siyo za kawaida, mpaka misibani?

Kuelekea 2010, tutaona mengi. Hila Kwa nini?
 
EL nauhakika hata usiku anaota watanzania wote tumemwangalia kwa jicho baya huku Mwakyembe kakanyaga shingoni mwake
 
EL nauhakika hata usiku anaota watanzania wote tumemwangalia kwa jicho baya huku Mwakyembe kakanyaga shingoni mwake

Nimecheka sana!! Duh!... ila inauma hivi bado kuna watu wanamtambua EL kiasi hicho? Wote wanaompa hii audience ni mafisadi tu kama yeye!!!

damn!!!
 
Kwenye msiba wa familia moja iliojikusanya pale Dar na kwenda Hedaru kwa mazishi, palikuwa na watu kibao tangu Alhamisi ya April 17 2008 mpaka mazikoni.

Kama kawaida ya jamii zetu, ndugu jamaa na marafiki hujumuika kwenye shughuli.

Basi wakati wa nasaha, pakatolewa ukumbi na huyu jamaa baada ya kutambulishwa na kupewa fursa ya kuzungumza kutokana na umashuhuri wake akasema

"Bwana Yesu asifiwe.....Mimi ni ...mimi si Fisadi au Mwizi...kama....." EL

Natamani nipewe nafasi kuimalizia hii sentensi.....!!!!:rolleyes:

But why EL? Why did you do it?? Ulifikiri Tz ya leo ndo ile ile ya siku zote? You can fool some people at some time but you can't fool all the people all the time!

Sasa hivi kiama chako chaja ni kushitakiwa na kuhukumiwa kwenda Ukonga/Keko/Segedansi!!!! Sio kutoa mawaidha kwenye misiba...ebo!
 
Jamani hii stori ina ukweli kiasi gani maaana sasa tunakoenda ni kumfanya jamaa awe jingle unnecessary.

Mch.Tusaidie ni msiba wa nani na kama ulikuwa hapa Dsm ni kitongoji kipi kinyume cha hapo ipelekwe kwenye nyepesi za Nyaisanga.

All in all umenichana mbavu sana kwa nyepesi kaka.
Tumsifu yesu kristu
 
Nimeisikia habari hii; alienda hapo msibani na mchungaji akamtambua na kumpa ukumbi aseme maneno ya rambirambi na Lowassa akihisi anaangaliwa kwa "jicho baya" akaanza kubreak "the ice" kwa kusema kinyume na watu wengi wanavyosikia kuwa yeye ni fisadi kwa kweli yeye si fisadi ni mkristu tu, na akachomekea "Bwana asifiwe sana"... Sina uhakika kama alitoa pole yenyewe...

Huu msiba ulikuwa unamuhusu? Kwa nini apewe nafasi? Hizi siasa zitatufikisha pabaya hadi katika viwanja vya Mungu? Hapakuwa na haja ya kuleta siasa katika majonzi. Mwenzetu ametangulia mbele ya haki badala ya kufikiria kumuombea marehemu asamehewe na Bwana, tunaleta mchezo. Hii ni hatari sana. Nani alimuuliza jamaa kama ni fisadi au la? Badala ya kutubu kwa Mungu, anaanza kubabaikia binaadam. Najua wapo watakaosema amewakosea binaadamu lakini kosa la ufisadi kwa Mungu ni makubwa zaidi.
 
Kwa analysis za haraka!

Spirit ya Watanzania imekuwa captured na FORCE against UFISADI!

Si jambo baya hii...! Kila mtu kuwa very consciouse na Dhana nzima ya kuukana ufisadi...hatakama ni kwenye ndoto, ulevini, msibani,kanisani etc!!

Sijambo baya!

Huo wimbo uendela na kuota mizizi kwa kila kichwa cha mtz. Kwa nini ngonjera za vijiweni, bongofalv, vichekesho etc vitawale fikra za wananchi...? Na isiwe kuukana ufisai? Kuukana ufisadi kukiigia vichwani na kwenye mioyo kama ya huyo bwana ...Psychologicaly speaking that is a blessing!!!

Posibility is..! Finaly one day the force can cristilise to pure "ACTION" against the realy FISADI of the national! Na kulitikisa BUNGE na hii SEREKALI inayonuka uvundo wa UFISADI mpaka misibani.
 
Mnaupenda sana Utomaso, hamuamini nilichokisema? muulizeni Askofu Mkuu wa KKKT Malasusa!
 
Duu kweli ukiwa mchafu sana unaweza ogea hata kojo! So desperate to clean himself, anatumia kila opportunity!
Hii kali, mchungaji anampa shetani-fisadi mic!!!?
 
Kama ni kweli basi huyu jamaa atakuwa ameanza kudata!

Ngabu,

huyu mbona alishadata siku nyingi na hitimisho lilikuwa siku ile interview yake ilivyozimwa pale TVT. Mambo yake mengine yamekufa kiaiana - mojawapo ikiwa ile kampeni ya kumtumia Balile kusafisha jina lake.

The guy ameanguka kama tembo mzee...... puuuhhhhhh
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom