Mimi nimeolewa naishi na mume wangu huu ni mwaka wa tatu bado hatujabahatika kupata mtoto

1. Ushauri ninaoweza kukupa ni kwenda kuonana na daktari bingwa wa mambo ya uzazi - wewe na mume wako. Kama uko Dar es Salaam unaweza kwenda Muhimbili au hata Regency au hospitali ingine yeyote ambayo mtu unayemfahamu aliweza kusaidiwa kwa tatizo kama la kwako. Wanaume mara nyingi wanaweza kukwepa hiki kipimo cha kujua kama anaweza kumpa mke wake mimba au la.
2. Wakati mwingine kuna kitu kinachoitwa 'hormone imbalance' na ili upate mimba mpaka upate dawa ya ku'balance hormones' zako kama tatizo liko kwako. Wakati mwingine wewe huna tatizo, ila labda mume wako ndiye ana tatizo na wakati mwingine wote hamna tatizo au wote mna matatizo. Ili kugundua tatizo liko wapi, mpaka mumpate daktari bingwa mzuri. Kuna mmoja namfahamu naye ni daktari bingwa wa mambo ya uzazi (hasa kwa akina mama). Anaitwa Dr Mashavu: ana hospitali yake Mwalusembe, Mukuranga (mji mdogo kabla hujafika Kimanzichana. Lakini kwa Dar es Salaam huwa anapatikana pia Kings Hospital (Kariakoo), kuna hospitali moja iko kati ya Bungoni na Soko la Karume (upande wa kulia kwa ndani kidogo kama unaelekea barabara inayotoka Keko kwenda Magomeni). Hii hospitali ama iko chini ya shirika la Kiislamu au mumiliki wake ni Mwislamu. Hospitali nyingine anakopatikana ni ile iliyokuwa inaitwa Sabrina (siku hizi nadhani ilishabadilishwa na kujengwa jengo la ghorofa. Unaweza kwenda mojawapo kati ya hizo sehemu kuulizia anapatikana lini ili upate appoitment na mkubaliane mkutane wapi ambapo unaona ni rahisi kwako. Dr Mashavu ni mtu mwema sana kwa wagonjwa. Wakati mwingine anashindwa kula lunch na kula saa 12 jioni kwa sababu anawapa wagonjwa wake muda wa kutosha kueleza matatizo yao. She's a good listener na naona pia imani ya dini imemwingia sana - anajali utu zaidi ya chochote na anaongea kwa upole kuliko madaktari wengine ambao wanaonyesha kiburi na lugha mbaya kwa wagonjwa wao.
3. Mimi na mke wangu tulikaa miaka 7 baada ya kufunga ndoa (2007) bila mtoto na hata baada ya mke wangu kwenda kupimwa hospitali (ambayo sitaitaja) na kuambiwa hawezi kuzaa. Alipokuja kuniambia kwamba ameambiwa kuwa 'hawezi kuzaa' mimi nilikubaliana na hiyo hali na kumwahidi kuwa 'sitamwacha kwa vile hazai na wala sitamwoa mke mwingine kwa vile hazai'. Kisha nikasema 'Kama Mwenyezi Mungu anataka tuishi hivi bila mtoto tulipokee kwa mikono miwili.' Na ndivyo tulivyoishi.
4. Baada ya muda kupita, mke wangu alisikia maumivu fulani kwenye tumbo la uzazi na kwenda kuonana na daktari bingwa Regency (alikuwa akiitwa Dr Anna Punnar, alikuwa Muhindi ila alisharudi kwao). Akamuuliza kama anaweza kumpima kipimo cha uzazi (kuona kama ana mayai ya uzazi) na matokeo yalionyesha kuwa yapo.
5. Kwa sasa tuna watoto wawili - wa kwanza alizaliwa Januari 15, 2015 na wa pili Agosti 1, 2018.
6. Wifi yake yeye alikaa miaka 11 na nadhani karibu alikuwa ameshakata tamaa na hata alidiriki kumwambia mume wake kuwa kwa vile dini yao inaruhusu kuoa wake hadi wanne anaweza kuoa mwingine. Kwa sasa hiyo familia wana watoto watatu.
7. Katika yote, mwombe Mwenyezi Mungu akusaidie - umtegemee yeye - na sala yako iwe 'Ee Mwenyezi Mungu ukitaka nizae, nifungue nami nipate watoto. Ukitaka niendelee hivi, nalipokea kwa mikono miwili na naomba unipe nguvu ya kulipokea kwa furaha maana wewe ukitaka hakuna linaloshindikana kwako'. Sala yetu sisi ilikuwa 'Ee Mwenyezi Mungu tupe ishara ya wema wako' ni phrase inayopatikana kwenye Zaburi 86 karibu na mwisho wa Zaburi.
Asante.. ila kuvumilia ndo nashindwa jmn. Nataman kupakata
 
Hii Sabrina kwa sasa inaitwa Tayma na ipo mbagala sabasaba, ukishuka tu kituoni unaiona ipande wa pili wa barabara, nakubaliana nawe hapo kuna kinadada wamejaaliwa utaalam huo kwani nami nilishampeleka mwari wangu hapo, na kwa sasa alhamdulillah si haba.
 
Mwnye dawa jmn naomba anisaidie. Mimi nmeolewa naishi na mume wangu huu ni mwaka wa tatu bdo hatujabahatika kupata mtoto. Anaejua dawa naomba anishauri.

Hosptal tumeshaenda
Dada pole sana,ni hivi hapa Jf utatapeliwa. Ushauri wangu ni huu.Tafuta sehemu lilipokanisa linalofanya maombezi.Narudia tena tafuta kanisa linalofanya maombezi.Kajisalimishe hapo,mwakani majira kama haya utakuja humu kututajia jina la mwanao.

Kama uko Mbagala Uliza Mchungaji Florian Katunzi

Kama uko Mbezi beach Uliza kwa Sylvester Gamanywa.BCIC

Au KKKT,Mbezi beach

Kama uko Kimara Uliza kwa Mch.Matsai KKKT

Kama Uko maeneo ya Mwenge,Uliza Mch.Kimaro Wa KKKT. Yuko Kakobe pia karibu na Mliman city.Pia yupo Mwingila karibu na daraja la lugalo.

Ukirudi hapa ubungo Riverside yupo Mzee wa Upako Antony Lusekelo.

Kawe yupo yule jamaa anaitwa Mwamposa

Ukiwa Ukonga ,Mtafute Suguye:huyu yupo Banana kuelekea kule kitunda
Ama fika kwa kanisa lolote lile lililokaribu nawe linalomkiri Yesu Kristo kuwa ni BWANA NA MWOKOZI wa Ulimwengu,

Na kwake hakuna jambo gumu.hata kama umekatwa mirija ya uzazi utapata mtoto.

Sema sharti lake ni moja tu,utatakiwa kutubu na kuziacha dhambi zote
 
Back
Top Bottom