Mimi ninadhani Lowasa anakurupuka mno bila ya kufikiria wewe unasemaje?

tibwilitibwili

Senior Member
Sep 12, 2006
184
10
Nyumba kuwekwa X marufuku -Lowassa

2006-09-30 09:20:56
Na Boniface Luhanga, Njombe


Serikali imepiga marufuku uwekaji wa alama za ’X’ ambao hufanywa na Wakala wake wa Barabara (TANROADS) katika nyumba zilizoko kwenye miliki ya barabara ikiwa upanuzi wa barabara inayokusudiwa hautafanywa kwa wakati huo.

Amri hiyo ilitolewa jana na Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa baada ya kupata taarifa za kuwekwa alama za ’X’ katika baadhi ya nyumba zilizoko? eneo la Lupembe, wilayani Njombe licha ya kwamba ujenzi wa barabara inayokusidiwa, haueleweki utafanywa lini.

Alipata taarifa hizo kupitia kwa Mbunge wa Njombe Kaskazini, Bw Jackson Makwetta, kufuatia kuhojiwa na Waziri Mkuu juu ya kinachoendelea huko Lupembe.

Hata hivyo, Bw. Makwetta alisema suala hilo siyo tatizo kubwa bali yawezekana lilikuzwa na baadhi ya vyombo vya habari kwa kuwa mpango wa kuijenga na kuipanua barabara hiyo ni wa muda mrefu.

Baada ya Waziri Mkuu kuelezwa hivyo na Mbunge huyo, alimtaka Mhandisi wa Barabara mkoani Iringa, Bw. Bernard Mugina, aeleze ni lini kazi ya upanuzi ama ujenzi wa barabara hiyo unatarajiwa kufanywa.

Hata hivyo, Bw Mugina alishindwa kueleza lini kazi hiyo itaanza kutekelezwa bali alisema ni kutoa tahadhari tu kwa wavamizi wa maeneo ya barabara ili pindi maeneo hayo yatakapohitajika, waondoke.

Kufuatia majibu hayo, Waziri Mkuu aliagiza kuwa si vema kuwaweka watu roho juu juu kwa kuweka alama za ’X’ kwenye nyumba zao wakati kazi ya upanuzi ama ujenzi haijulikani itafanywa lini.

Mbali ya eneo la Lupembe, Waziri Mkuu alisema pia aliona alama kama hizo katika nyumba za wakazi wa Bulongwa, ambao baadhi yake wanaishi wajane na wagonjwa wa Ukimwi.

”Msiwaletee bughudha watu, Bulongwa pia nyumba zao wamewekewa alama hizo lakini hata barabara yenyewe haijulikani itapanuliwa lini,” alisema.

Bw Lowassa alisema uamuzi wa kutowabughudhi wananchi kwa kuwekea alama za ’X’ wakati ujenzi wa barabara husika haujapangwa ama kujulikana, uliamriwa na Baraza la Mawaziri tangu enzi za utawala wa Serikali ya Awamu ya Tatu chini ya Rais mstaafu, Bw Benjamin Mkapa.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Bi. Halima Kasungu, alisema mtindo wa TANROADS kuweka alama hizo katika nyumba za wananchi wakati ujenzi wa barabara haujulikani, una madhara makubwa sana kisiasa.

Naye Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Bi. Mwantumu Mahiza, alisema TANROADS inakusudia kubomoa shule karibu ya 20 kupisha upanuzi wa barabara.

Hata hivyo, Waziri Mkuu alisema hawataweza kufanya hivyo kwa kuwa TANROADS haina fedha za kulipa fidia kwa shule hizo.

SOURCE: Nipashe
 
He's an opportunist and a populist.Ikijitokeza tu nafasi ya kujipatia umarufu wa jukwaani basi haiachii.Kila siku anawaumbua viongozi wa mitaa,kata,tarafa,wilaya,etc lakini sijamsikia akimuumbua mla rushwa hadharani,au akimtoa nishai waziri hadharani.Kule Dodoma ndie alikuwa mstari wa mbele kuokoa bajeti za kina Mramba na wenzake.
 
Lowassa anataka kuweka Headlines tu,amri hii inaonyesha kiu yake ya kusifiwa na jinsi gani mawazo yake ni mafupi yanaishia leo! kwanini wasiweke x kutahadharisha watu ili wasiJE wakawekeza zaidi na badae wakajapata hasara kubwa zaidi? Au kuweka x si itakuwa ni ishara kuwafanya watu wajiandae kuhama taratibu

Kwa Kuondoa hizo alama anahalalisha watu kuendelea kujenga eneo hilo,na bora hata angeshauri watu wasiendelea kuwekeza hela zao katika maeneo hayo na waliopo wajiandae kuhama taratibu taratibu!

Tanroads wanafanya vyema na wanawaokoa watu wasipate hasara hapo badae!

Tatizo kuu la Lowassa ni kwamba anajaribu kugeuka kivuli cha mtu mwingine(anataka kuwa Sokoine),kwa kufanya hivyo anajikana na kugeuka kikaragosi cha aina yake ambacho kitaigharimu sana nchi yetu!
 
Lowasa na kuropoka kwake kila mara nabakia kushangaa na sasa kapata support ya waziri kwa kusema kuweka x kwenye kuna gharama kisiasa that shows how serikali ya mtandao haiko tayari kufanya maamuzi mzito ya kitaifa bali wanaangalia ulaji wao tu . Kama no warning is given now na kesho jamaa wakapata pesa wakaanza kujenga barabara nyumba zitabomolewa hapo itakuwa mbaya zaidi kisiasa maana CCM mtashindwa kuuzima moto. Lowasa anaendelea kusema tanroad hawana pesa za kulipa fidia .Jamani Lowasa inaonekana akil yako haina akili . Kumbe you know better lakini kweye majukwaa mnapiga kelele za kuongeza miungu mbingu kumbe huwa ni kuomba kura tu ? Mnajimaliza maana inaonekana sasa umaarufu unaweza kuwa balaa zaidi mwishowe.
 
Tibwiltibwili hii nchi inahitaji kufumuliwa na kusikwa upya! Hawa jamaa na ma MC(wasema chochote)!
 
Halafu tatizo linazidi kuwa baya zaidi unapochanganya na waandishi wetu wa habari ambao wamekaa kishabiki. Cheki hii stori hapa chini, kuwa

Lowasa agundua chanzo kingine cha umeme

. Abaini maporomoko yenye uwezo wa kuzalisha megawati 222
. Ashangaa TANESCO kukalia taarifa za utafiti uliofanyika
. Aahidi kumwagiza Waziri, Wataalamu wa Wizara kufuatilia

Na Magnus Mahenge, Makete

WAZIRI Mkuu, Bw. Edward Lowassa ameshangazwa na kile kilichoelezwa kuwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO ) kukalia taarifa za utafiti za utafiti wa maporomoko ya mto Luvanyina, ulioko Makete, mkoani Iringa ambayo yanaweza kuzalisha megawati 222 na kusaidia tatizo la mgowo wa umeme unaoendelea nchini

Taarifa iliyosomwa juzi kwenye maporomoko hayo yaliyopo
Madihani na Mkuu wa Wilaya hiyo, Bw. Lepy Gembe ilieleza kuwa kama TANESCO ingetumia utafiti huo na kujenga mtambo wa kuzalisha umeme kwenye maporomoko hayo Taifa lingeondokana na tatizo sugu la mgawo wa umeme ambao umekuwa kero kubwa kwa wananchi.

Ilielezwa kwamba umeme huo ungezidi kiwango cha ule unaozalishwa Mtera ambao katika hali ya kawaida ni megawati 80 na sasa zimefikia megawati 30 tu .

Akiwahutubia wananchi wa Bulongwa, Bw. Lowassa alisema atamwagiza Waziri wa Nishati na Madini na watalaamu wake kwenda kwenye mto Luvanyina kuhakiki uwezo wa maporomoko hayo haraka, yaliyo kwenye mwinuko wa mita 3,000 kutoka usawa wa bahari.

Bw. Lowassa alitoa kauli hiyo baada ya wananchi wa Makete
kuiomba Serikali itupie macho maporomoko hayo, kwa lengo la kupata chanzo kingine kitakachosaidia kuapatikana ufumbuzi wa kudumu wa tatizo la umeme.

Waziri Mkuu, alishangaa kusikia kwamba pamoja na TANESCO kufanya utafiti miaka mingi iliyopita na kuthibitisha uwezo wa maporomoko hayo kuzalisha umeme , hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kuandaa miundo mbinu ya upatikanaji wa nishati hiyo.

Mbali na utatifiti huo, Bw. Lowassa alishangaa kusikia kuwa miaka miwili iliyopita, Kampuni iitwayo Sudpower kutoka Swedeni kwa kushirikiana na nyingine kutoka Afrika Kusini, zilifanya utafiti mwingine na kubaini uwezo wa mto huo kuzalisha umeme lakini hakuna kilichofanyika.

Ilielezwa kuwa kutokana na sababu ambazo hazieleweki hadi sasa , iliamuliwa mtambo huo ujengwe bwawa la Kihansi lenye uwezo wa kuzalisha megawati kati ya 80 na 100, badala mto Luvanyina wenye uwezo wa kuzalisha mara mbili zaidi yake.

Utafiti mwingine kwenye maporomoko hayo ulifanywa mwaka 1992 na Idara ya Maji kwa lengo la kujua uwezo wa mto huo kuongezeka na kupungua wakati wa kiangazi na ikabaini kuwa una nguvu za kutosha kusukuma maji hayo misimu yote.

"Maji yanayotoka wilayani Makete asilimia 90 yanaingia katika Ziwa Nyasa, na mito mingi ukiwemo Luvanyina, haikauki, imejaa wakati wote na inafaa kwa kuzalisha umeme lakini hadi sasa haitumiki.." alisema Bw. Gembe.

Alieleza kuwa mwaka huo Kanisa na Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) , Dayosisi ya Kusini Kati, Bulongwa Makete, baada ya kupata wafadhili kutoka Swideni, lilijenga mashine ya umeme na miaka miwili baadaye, umeme ulianza kutumika.

Umeme unaozalishwa na kanisa hilo, unatumika katika hospitali ya Bulongwa na Shule ya sekondari ya Bulongwa zinazomilikiwa na kanisa hilo na maeneo ya vijiji jirani kwenye mashine za kusaga ,ambazo zinatumia asilimia tano tu ya umeme huo.

Ilielezwa kuwa kama umeme wa maporomoko hayo ungetumika, ungeongeza kiwango cha mahitaji ya taifa ya megawati 500, ambapo kwa sasa megawati 200 zinazalishwa na Songas, 100 na IPTL .

Bw. Lowassa amekuwa akifanya juhudi kubwa kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa tatizo la umeme hapa nchi. Hivi karibuni alipokuwa ziarani Asia, aliwasilisha ombi lake kwa Taasisi ya Kifalme ya Thailand, kuangalia uwezekano wa kupatiwa teknolojia ya kutengeneza mvua , kwa lengo la kujaza kina cha bwawa la Mtera ambalo ni chanzo kikuu cha kuzalisha umeme.

http://majira.co.tz/kurasa.php?soma=tanzania&habariNamba=1307
 
Vyombo vya Habari vinatuangusha sana! Hivi Lowassa kaingia serekalini mwaka huu!! Kwa hiyo anataka kuiambia dunia hilo suala kalijua jana alipokuwa anafanya ziara huko Iringa!!!
 
Haya ni mnatokeo ya mwandishi kuhakikisha kwamba anakuwa anakumbukwa na waziri anapokuwa mikoani ama nje .Yaani mtu kuhakikisha kwamba kipato kiko salama sawia , kupalilia ulaji, kutaka mkate uisipate mavumbui huku Taifa linauawa na kuonekana mjinga mbele ya Umma kwa taaluma yako .Bora kuandika Lowasa aone .Kulipa fadhila za kuwemo kwenye msafara .Haya ni matokeo ya watu kukosa uzalendo, intergrity and honest.Kutokujua kwa nini ni mwandishi wa habari na kutokujua aandike nini labda pia ni Elimu yake mbovu yeye mwndishi .Je mhariri naye yukpo wapi ama bora kuuza magazeti na kulamba miguu ya bwana mkubwa ?Hapa kweli Kenge ambaye ni Lowasa kapigiwa ngoma kwenye maji tena mtoni na sasa kila kitu ni tibwilitibwili wakiwemo waandishi .
 
umeme unaweza kuzalishwa kwa gharama ipi na baada ya muda gani? kwanini Lowassa anakurupuka na kutoa matamko baada ya kusikiliza upande mmoja tu? kwanini hawaulizi Tanesco sababu za kutofanyia kazi "utafiti" huo?

ni kweli kabisa Lowassa anajaribu kuwa Sokoine wa pili. tatizo ni kwamba Lowassa, bila kijitambua, anaiga mapungufu aliyokuwa nayo Sokoine, yaani maamuzi ya haraka, yasiyofanyiwa utafiti, na yasiyoangalia athari za muda mrefu.

Ni vizuri Lowassa akamsoma vizuri Sokoine, na akaiga uzalendo wake, kuzingatia maadili ya uongozi, na kukataa rushwa.
 
Eric Ongara said:
Vyombo vya Habari vinatuangusha sana! Hivi Lowassa kaingia serekalini mwaka huu!! Kwa hiyo anataka kuiambia dunia hilo suala kalijua jana alipokuwa anafanya ziara huko Iringa!!!

JK na Lowassa wake wanaendelea kupata sapoti ya wanamtandao,some of whom ni journalists.Yaani Lowassa kawa mvumbuzi kma wale tuliowasoma kwenye some la historia!?Huyu mtu alikuwepo siku zote hizi,na katika awamu iliyopita alikuwa waziri wa maji (meaning miongoni mwa majukumu yake yalikuwa ni kubaini vyanzo vya maji kama hicho "alichokivumbua" baada ya kupata u-PM).Hivi majuzi tu aliwataka DAWASA wampelekee orodha ya wadaiwa sugu wa maji...why didnt he come up with that idea when alipokuwa waziri wa maji?

Wanatafuta umaarufu kwa kutumia mgongo wa matatizo ya wananchi.
 
Sasa naanza kutafakari miaka kumi ya lowassa kama uwaziri mkuu,nanangalia uwezekano wa Lowasa kuchukua mikoba ya J.K 2015! Mungu atuepushe!
 
Ndiyo maana wakati mwingine unaona bora kina Daily News inapokuja suala la uandishi wa habari, kwa maana ya content, objectivity na kutokuwa unnecessarily sensational. Kwa kuwa wao ni gazeti la serikali, waandishi/mhariri haongozwi na kutaka kuongeza mauzo ya tajiri. Tatizo ni kwamba wao hawawezi kumuumbua bosi wao (serikali).
 
Salaam Wanabodi,

Jamani katika awamu zoooote nne za utawala wa nchi yetu tz, hatujapata PM wakuchonga kama EL!

Tulikuwa tumamjoke Naibu waziri mkuu Mrema kwa kauli zake, lakini hili la EL ni funga kazi!

Waziri mkuu, ambaye kwa kawaida ni mtendaji wa serikali, iweje afanye mambo kisiasa kiasi hiki? Hivi wewe ukiwa na shamba lako pori huna fedha za kulimia kwa muhula huu, ati utawaambia wananchi wakalime then ukipata pesa utawaambia waondoke! Je wataondoka kweli?

Nielewavyo Alama za X, zinasaidia kuwa alert wananchi kuwa hayo maeneo yapo reserved kwa magari, imagine gari limepata ajali likafunga barabara, na right of way zimejengwa nyumba sasa ndo wasafiri wakwame? Shiiiiiit! Kama mwaka huu kuna nyumba tatu ndani ya hifadhi ya barabara huna hela za kujenga, ukipata fedha after five years kukawa tayari kuna nyumba mia moja, Je MTAWALIPA WOTE HAO FIDIA?

.......................
:U Can't Change The Nature:
 
Lowassa awageuka wenye alama X Tanga

Na Burhan Yakub, Tanga
WAZIRI Mkuu, Edward Lowassa, amewaagiza wenye nyumba zilizowekwa alama za X pembeni mwa barabara ya Tanga-Horohoro, kuzibomoa haraka ili kupisha ujenzi wa barabara hiyo.

Lowassa alitoa agizo hilo jana, wakati akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Duga wilayani Mkinga, wakati wa ziara yake mkoani Tanga.

Alisema wakazi wa Mkinga wasitegemee kuwa atazuia ubomoaji kama alivyofanya Iringa kwa kuwa barabara ya Horohoro ipo karibu kuanza kujengwa kwa kiwango cha lami.

Waziri mkuu ambaye aliwasili na na kupokea taarifa ya mkoa Ikulu ndogo mjini Tanga, alieleza kusikitishwa kwake na kasi ndogo ya uanzishwaji wa vyama vya kuweka na kukopa (saccos) Mkoa wa Tanga.

Akiwa kijijini Duga, Waziri Mkuu alifungua Saccos ya wananchi na kuchangia Sh5 milioni kwa ajili ya kuipa nguvu Saccos hiyo. Pia alikagua majengo ya makao makuu ya Wilaya ya Mkinga.

Akiwa ziarani wilayani Njombe, Mkoa wa Iringa, Waziri Mkuu aliwataka viongozi wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), kufuta mara moja alama za X walizoziweka katika nyumba mbalimbali kwenye maeneo ambayo serikali haina mpango wa kupanua barabara katika miaka ya karibuni.

Alitoa malalamiko hayo baada ya kulalamikiwa na Mbunge wa Njombe kaskazini, Jackson Makwetta, aliyemweleza kuwa nyumba nyingi katika Kijiji cha Lupembe wilayani humo zimewekewa alama ya X pamoja na kwamba hakuna mpango wowote wa kupanua barabara katika maeneo katika miaka ya karibuni.

Lowassa alimwamuru Meneja wa Tanroads Mkoa wa Iringa, kufuta mara moja alama hizo na kusitisha kazi ya kuziwekea alama hizo nyumba nyingine ambazo zipo katika maeneo ambayo hayatarajiwi kuendelezwa katika miaka ya karibuni.
 
Kama kuna kipindi TZ tumepata PM msanii ndio sasa. Lowasa anakurupuka mnoo bila kufuata sheria zilizoweka na serikali na vyombo vyake husika. Sheria ya ardhi inakataza kabisa watu kujenga kwenye Hifadhi za barabara kwa sababu. Hifadhi ya barabara inatumika kama "buffer zone" kati ya barabara na makazi ya watu. Any time gari likiacha njia/ kupinduka lisidhuru watu na makazi yao na ni eneo linalotumika kwa upanuzi wa barabara.Serikali iliyopita chini ya Wizara ya ujenzi na TANROADS kwa kufahamu umuhimu wa hifadhi ya barabara walikuwa busy kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kuahama eneo hilo na walitumia mamilioni ya pesa kwa zoezi hilo. Leo unawambia waendelee kukaa je ajui kwamba anahatarisha maisha ya wapiga kura wake wanaojenga maeneo hayo pindi ajali zinapotokea?

Ni kiongozi dhahifu asiyekuwa na maamuzi ya mda mrefu anafikiria hapo alipo tu na sio miaka 25-50 ya mbele. Ni kiongozi asiyefuata maadili ya uongozi, ni kiongozi anayejali kusifiwa.Ni kiongozi anayetoa maamuzi bila kufanya utafiti na kushirikisha taasisi nyingine za serikali. Ni kiongozi anayekuwa mkali kwa viongozi wadogo wa serikali kama wa-kuu wa wilaya na wafanyakazi wadogo ili kujitafutia umaharufu.Upokuwa na aina hii ya MP na Rais kilaza bila kusahau waandishi dhahifu wa habari sijui wapi tunakwenda. Nchi yetu sasa inaongozwa na wasanii na watu walagahi.Ni viongozi wanaowapangia waandishi wa habari nini cha kuandika na nini sio cha kuandika.
 
tibwilitibwili said:
Nyumba kuwekwa X marufuku -Lowassa

2006-09-30 09:20:56
Na Boniface Luhanga, Njombe


Serikali imepiga marufuku uwekaji wa alama za ’X’ ambao hufanywa na Wakala wake wa Barabara (TANROADS) katika nyumba zilizoko kwenye miliki ya barabara ikiwa upanuzi wa barabara inayokusudiwa hautafanywa kwa wakati huo.

Amri hiyo ilitolewa jana na Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa baada ya kupata taarifa za kuwekwa alama za ’X’ katika baadhi ya nyumba zilizoko? eneo la Lupembe, wilayani Njombe licha ya kwamba ujenzi wa barabara inayokusidiwa, haueleweki utafanywa lini.

Alipata taarifa hizo kupitia kwa Mbunge wa Njombe Kaskazini, Bw Jackson Makwetta, kufuatia kuhojiwa na Waziri Mkuu juu ya kinachoendelea huko Lupembe.

Hata hivyo, Bw. Makwetta alisema suala hilo siyo tatizo kubwa bali yawezekana lilikuzwa na baadhi ya vyombo vya habari kwa kuwa mpango wa kuijenga na kuipanua barabara hiyo ni wa muda mrefu.

Baada ya Waziri Mkuu kuelezwa hivyo na Mbunge huyo, alimtaka Mhandisi wa Barabara mkoani Iringa, Bw. Bernard Mugina, aeleze ni lini kazi ya upanuzi ama ujenzi wa barabara hiyo unatarajiwa kufanywa.

Hata hivyo, Bw Mugina alishindwa kueleza lini kazi hiyo itaanza kutekelezwa bali alisema ni kutoa tahadhari tu kwa wavamizi wa maeneo ya barabara ili pindi maeneo hayo yatakapohitajika, waondoke.

Kufuatia majibu hayo, Waziri Mkuu aliagiza kuwa si vema kuwaweka watu roho juu juu kwa kuweka alama za ’X’ kwenye nyumba zao wakati kazi ya upanuzi ama ujenzi haijulikani itafanywa lini.

Mbali ya eneo la Lupembe, Waziri Mkuu alisema pia aliona alama kama hizo katika nyumba za wakazi wa Bulongwa, ambao baadhi yake wanaishi wajane na wagonjwa wa Ukimwi.

”Msiwaletee bughudha watu, Bulongwa pia nyumba zao wamewekewa alama hizo lakini hata barabara yenyewe haijulikani itapanuliwa lini,” alisema.

Bw Lowassa alisema uamuzi wa kutowabughudhi wananchi kwa kuwekea alama za ’X’ wakati ujenzi wa barabara husika haujapangwa ama kujulikana, uliamriwa na Baraza la Mawaziri tangu enzi za utawala wa Serikali ya Awamu ya Tatu chini ya Rais mstaafu, Bw Benjamin Mkapa.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Bi. Halima Kasungu, alisema mtindo wa TANROADS kuweka alama hizo katika nyumba za wananchi wakati ujenzi wa barabara haujulikani, una madhara makubwa sana kisiasa.

Naye Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Bi. Mwantumu Mahiza, alisema TANROADS inakusudia kubomoa shule karibu ya 20 kupisha upanuzi wa barabara.

Hata hivyo, Waziri Mkuu alisema hawataweza kufanya hivyo kwa kuwa TANROADS haina fedha za kulipa fidia kwa shule hizo.

SOURCE: Nipashe
lowasa amekuwa ni mtu anayetaka kuiendesha nchi hii kwa amri na si kwa sheria na kama tukiendelea namtindo huu basi mwisho wake ni mbaya sana.

lakini ikumbukwe kwamba anafanya haya kwa wanyonge wa nchi hii na si kwa wanyonyaji na matapeli wakubwa wanaoiba uchumi wanchi kila iitwapo leo

chonde LOWASA rekebisha mfumo wa utendaji fuata haki na sheria ubabe weka pembeni.
 
Back
Top Bottom