Mimi ninadhani Lowasa anakurupuka mno bila ya kufikiria wewe unasemaje?

kama umewahi kusoma kitabu cha mfalme juha basi utakubaliana nami kwamba kutojua au kujua na kuamua kwa maksudi kuacha kuzifuata na kuzitekeleza sheria za nchi ndiyo ilikuwa chanzo cha mfalme kwa hiari yake kuamua kunyongwa.
kama hujasoma kitabu hiki nakushauri kitafute usome. washauri wa Lowasa kama wapo basi hawasikilizwi na kama wanasikilizwa basi wanashauri ujinga kila siku. hivi inaingia aikilini leo unasema hakuna kuweka X kwenye nyumba kesho unageuka kwamba hizo X hazihusiani na kauri yako?

maana yake nini? ni kwamba kila mahali kauri itokayo hapo ni ya hapo tu na haina mahusiano na sehemu nyingine za nchi. ikiwa PM ndo mwenye maamuzi haya basi subirini yananyokuja. nchi ya kichaa hii hapa.
 
Hivi huyu wa kulipuka bila kujiuliza mvua ile ya Thailand kwa wala rushwa wenzake ataileta lini ?Maana tunangoja mvua aimwage mtera tupate umeme .
 
tibwilitibwili said:
Nyumba kuwekwa X marufuku -Lowassa

2006-09-30 09:20:56
Na Boniface Luhanga, Njombe


Serikali imepiga marufuku uwekaji wa alama za ’X’ ambao hufanywa na Wakala wake wa Barabara (TANROADS) katika nyumba zilizoko kwenye miliki ya barabara ikiwa upanuzi wa barabara inayokusudiwa hautafanywa kwa wakati huo.

Amri hiyo ilitolewa jana na Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa baada ya kupata taarifa za kuwekwa alama za ’X’ katika baadhi ya nyumba zilizoko? eneo la Lupembe, wilayani Njombe licha ya kwamba ujenzi wa barabara inayokusidiwa, haueleweki utafanywa lini.



Alipata taarifa hizo kupitia kwa Mbunge wa Njombe Kaskazini, Bw Jackson Makwetta, kufuatia kuhojiwa na Waziri Mkuu juu ya kinachoendelea huko Lupembe.

Hata hivyo, Bw. Makwetta alisema suala hilo siyo tatizo kubwa bali yawezekana lilikuzwa na baadhi ya vyombo vya habari kwa kuwa mpango wa kuijenga na kuipanua barabara hiyo ni wa muda mrefu.

Baada ya Waziri Mkuu kuelezwa hivyo na Mbunge huyo, alimtaka Mhandisi wa Barabara mkoani Iringa, Bw. Bernard Mugina, aeleze ni lini kazi ya upanuzi ama ujenzi wa barabara hiyo unatarajiwa kufanywa.

Hata hivyo, Bw Mugina alishindwa kueleza lini kazi hiyo itaanza kutekelezwa bali alisema ni kutoa tahadhari tu kwa wavamizi wa maeneo ya barabara ili pindi maeneo hayo yatakapohitajika, waondoke.

Kufuatia majibu hayo, Waziri Mkuu aliagiza kuwa si vema kuwaweka watu roho juu juu kwa kuweka alama za ’X’ kwenye nyumba zao wakati kazi ya upanuzi ama ujenzi haijulikani itafanywa lini.

Mbali ya eneo la Lupembe, Waziri Mkuu alisema pia aliona alama kama hizo katika nyumba za wakazi wa Bulongwa, ambao baadhi yake wanaishi wajane na wagonjwa wa Ukimwi.

”Msiwaletee bughudha watu, Bulongwa pia nyumba zao wamewekewa alama hizo lakini hata barabara yenyewe haijulikani itapanuliwa lini,” alisema.

Bw Lowassa alisema uamuzi wa kutowabughudhi wananchi kwa kuwekea alama za ’X’ wakati ujenzi wa barabara husika haujapangwa ama kujulikana, uliamriwa na Baraza la Mawaziri tangu enzi za utawala wa Serikali ya Awamu ya Tatu chini ya Rais mstaafu, Bw Benjamin Mkapa.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Bi. Halima Kasungu, alisema mtindo wa TANROADS kuweka alama hizo katika nyumba za wananchi wakati ujenzi wa barabara haujulikani, una madhara makubwa sana kisiasa.

Naye Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Bi. Mwantumu Mahiza, alisema TANROADS inakusudia kubomoa shule karibu ya 20 kupisha upanuzi wa barabara.

Hata hivyo, Waziri Mkuu alisema hawataweza kufanya hivyo kwa kuwa TANROADS haina fedha za kulipa fidia kwa shule hizo.

SOURCE: Nipashe

Sijui kama viongozi wetu huwa wanafuata masharti au hata wanaheshimu kazi za watu wengine hata kama wako chini yao. Inabidi wachukue muda kuongea na Idara/Wizara husika na sio kuropoka tu kwa kila kitu wanacholalamikiwa na wananchi. That's why we have people specialize in one area of study and these leaders don't know any rules of engagement in these area.

All this is lack of good leadership skills, and good governance

Its TATU,
JumaTATU
 
Tanzania kwa muda wote tangia Mkoloni aondoke Mwalimu aliingiza siasa hadi Jeshini na Polisi na michezoni hadi kazini. Sasa wana siasa na hasa hawa wa serikali ya VGD hawana wajualo ila kulipuka na kuanza kusema kisiasa magazeti yaandike huku hakuna kitu . Ndiyo madhara haya . Naomnba tuangalie katiba kama kuna sehemu inaruhusu kumshitaji Rais na kundi lake lote wakisema uongo chini ya kiapo ama kuvunja sheria wakiwa madarakani waburuzwe Mahakamani .
 
Mlalahoi said:
He's an opportunist and a populist.Ikijitokeza tu nafasi ya kujipatia umarufu wa jukwaani basi haiachii.Kila siku anawaumbua viongozi wa mitaa,kata,tarafa,wilaya,etc lakini sijamsikia akimuumbua mla rushwa hadharani,au akimtoa nishai waziri hadharani.Kule Dodoma ndie alikuwa mstari wa mbele kuokoa bajeti za kina Mramba na wenzake.

jamaa huwa anakurupuka sana.
 
Katika pita pita zangu nimefukua hii kuhusu EL back in 2006, miaka 6 baadaye utabiri wa wakongwe hawa wa JF unaelekea kutimia?
 
Back
Top Bottom