tibwilitibwili
Senior Member
- Sep 12, 2006
- 181
- 10
Nyumba kuwekwa X marufuku -Lowassa
2006-09-30 09:20:56
Na Boniface Luhanga, Njombe
Serikali imepiga marufuku uwekaji wa alama za X ambao hufanywa na Wakala wake wa Barabara (TANROADS) katika nyumba zilizoko kwenye miliki ya barabara ikiwa upanuzi wa barabara inayokusudiwa hautafanywa kwa wakati huo.
Amri hiyo ilitolewa jana na Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa baada ya kupata taarifa za kuwekwa alama za X katika baadhi ya nyumba zilizoko? eneo la Lupembe, wilayani Njombe licha ya kwamba ujenzi wa barabara inayokusidiwa, haueleweki utafanywa lini.
Alipata taarifa hizo kupitia kwa Mbunge wa Njombe Kaskazini, Bw Jackson Makwetta, kufuatia kuhojiwa na Waziri Mkuu juu ya kinachoendelea huko Lupembe.
Hata hivyo, Bw. Makwetta alisema suala hilo siyo tatizo kubwa bali yawezekana lilikuzwa na baadhi ya vyombo vya habari kwa kuwa mpango wa kuijenga na kuipanua barabara hiyo ni wa muda mrefu.
Baada ya Waziri Mkuu kuelezwa hivyo na Mbunge huyo, alimtaka Mhandisi wa Barabara mkoani Iringa, Bw. Bernard Mugina, aeleze ni lini kazi ya upanuzi ama ujenzi wa barabara hiyo unatarajiwa kufanywa.
Hata hivyo, Bw Mugina alishindwa kueleza lini kazi hiyo itaanza kutekelezwa bali alisema ni kutoa tahadhari tu kwa wavamizi wa maeneo ya barabara ili pindi maeneo hayo yatakapohitajika, waondoke.
Kufuatia majibu hayo, Waziri Mkuu aliagiza kuwa si vema kuwaweka watu roho juu juu kwa kuweka alama za X kwenye nyumba zao wakati kazi ya upanuzi ama ujenzi haijulikani itafanywa lini.
Mbali ya eneo la Lupembe, Waziri Mkuu alisema pia aliona alama kama hizo katika nyumba za wakazi wa Bulongwa, ambao baadhi yake wanaishi wajane na wagonjwa wa Ukimwi.
Msiwaletee bughudha watu, Bulongwa pia nyumba zao wamewekewa alama hizo lakini hata barabara yenyewe haijulikani itapanuliwa lini, alisema.
Bw Lowassa alisema uamuzi wa kutowabughudhi wananchi kwa kuwekea alama za X wakati ujenzi wa barabara husika haujapangwa ama kujulikana, uliamriwa na Baraza la Mawaziri tangu enzi za utawala wa Serikali ya Awamu ya Tatu chini ya Rais mstaafu, Bw Benjamin Mkapa.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Bi. Halima Kasungu, alisema mtindo wa TANROADS kuweka alama hizo katika nyumba za wananchi wakati ujenzi wa barabara haujulikani, una madhara makubwa sana kisiasa.
Naye Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Bi. Mwantumu Mahiza, alisema TANROADS inakusudia kubomoa shule karibu ya 20 kupisha upanuzi wa barabara.
Hata hivyo, Waziri Mkuu alisema hawataweza kufanya hivyo kwa kuwa TANROADS haina fedha za kulipa fidia kwa shule hizo.
SOURCE: Nipashe