Mimi nina masters nataka kuoa Darasa la saba

Hapo tatizo si elimu ila walitofautiana interest", kila mtu ana interest yake hata wote mkiwa maprofesa. Na kwa ufahamu wangu interest haifundishwi darasani
Kijuujuu unaweza ukafikiri tatizo la huyo dokta na mkewe ni interest tofauti.Naomba nikupe undani
wa hili tatizo lililokumba ndoa ya dokta.Hiki kisa cha dstv kilitokea mwaka 2006.
Dokta alimweleza mkewe kwamba tamthiliya za Mambo Hayo na Tausi zilishaisha zamani hazipo tena.Mkewe
hakuamini, aliona mume anamyima raha makusudi.Mke akanyamaza lakini rohoniakahifadhi cheche ya hasira iliyolipuka na kuvunja ndoa mwaka 2008 mume alipomnunulia simu.

Kwa sababu ya uelewa mdogo wa mambo, kila akimpigia mumewe simu akaambiwa na mitambo yenye sauti ya kike:"Namba unayopiga kwa sasa haipatikani kwa sasa, jaribu baadaye" mke anafikiri sauti ni ya hawara wa mumewe!
Mume akirudi nyumbani mke analianzisha, mume anamfahamisha juu ya hiyo sauti inakotoka, mke anang'ang'ania msimamo na uelewa wake.

Mwishowe waliachana oktoba 2013 baada ya vikao vyingi vya usuluhishi kushindikana.

Daktari yu mbioni anatafuta mke.
 
Mh hapo sina la ziada
 
Jamani wanajamvi naombeni Mawazo yenu. Kuhusiana na kichwa cha habari hapo juu, mie ni Muislam, nilioa Mwalimu wa Primary nikaachana nae baada ya kubaini anafanya Ngono na afisa Taaluma wa Jiji.
Nimepata binti aliyeishia Darasa la saba. Nipeni uzoefu haya Maisha yatakuaje kwa gepu hilo kubwa la elimu.

Nawasilisha.

Kwenye ndoa hakuna mzoefu kwani hata wazee huachana. Mshirikishe Mwenyezi Mungu pekee utapata mke mwema anayekufaa. Elimu, Pesa, sio vigezo !
 
tarajia cost kubwa itakayotokana na ujinga!!!

cost gani wewe mwanambunyu? Wewe kama unaweza kuishi na matatizo kwa kuogopa gharama ndogo pole yako. Nyie ndio mnaokufa na njaa tukiwasachi tunawakuta na milioni 2 mfukoni.
 
kipusy mdau, Mwenyezimungu ukimuomba atakupa mke mwema,Mtume Muhammad (SAW) alitaja sifa za mke mwema,baadhi ni hizi:-awe anaijua dini yake, awe mrembo,nasaba yake pia iwe nzuri huko kwenye familia yake na awe na kipato,ili ukifulia akuwezeshe.
Sasa basi kigezo cha elimu hakikutajwa,ila elimu hapo inaangukia kumjua Mwenyezimungu,kama huyo std seven anafaa si tatizo oa,mke wako wa kwanza alikua hana hofu ya mwenyezimungu,wewe hofu yako ipi kwa huyo la 7?
Mkoroshokigoli
Nilikupata vyema ndugu, nikalifanyia kazi. Sasa hivi tuna watoto wa 2 na huyo Binti. Ni mke mwema sana.
 
Jamani wanajamvi naombeni Mawazo yenu. Kuhusiana na kichwa cha habari hapo juu, mie ni Muislam, nilioa Mwalimu wa Primary nikaachana nae baada ya kubaini anafanya Ngono na afisa Taaluma wa Jiji.
Nimepata binti aliyeishia Darasa la saba. Nipeni uzoefu haya Maisha yatakuaje kwa gepu hilo kubwa la elimu.

Nawasilisha.

Elimu ya darasani na elimu ya Maisha ni vitu viwili tofauti, mwanamke anaweza akafika mpaka level ya degree lakini akapitwa kiakili na mwanamke aliyeishia primary. Muoe tu, kwa kuwa wewe una elimu basi inatosha mana utakua ni msimamizi yeye atakua mtekelezaji
 
Swala la ndoa ni kumuomba mungu tu akujaalie mke mwema, maswala ya elimu hayo sidhani kama yana jalisha.

Unaweza kupata mke ambaye hajasoma na akawa wa heri kwako, na unaweza ukapata aliesoma sana na pesa zake ila akawa si mke mwema.

Cha msingi fanya ibada sana umuombe mungu akuongoze njia sahihi tu.
 
Oa darasa 4 Mkuu, la saba nao wasumbufu tu, ninae hapa ananipa shida kweli!
 
Swala la ndoa ni kumuomba mungu tu akujaalie mke mwema, maswala ya elimu hayo sidhani kama yana jalisha.

Unaweza kupata mke ambaye hajasoma na akawa wa heri kwako, na unaweza ukapata aliesoma sana na pesa zake ila akawa si mke mwema.

Cha msingi fanya ibada sana umuombe mungu akuongoze njia sahihi tu.
:p:p
 
imeandikwa wapi mwenye master anaona mwenye master mwenzie sasa kama dalasa la saba ni vzr zaid utamfunza mengi ukisha muoa elimu ni tofauti katika mahusiano unaweza kuwa na master alafu ukazidiwa na dalasa la saba kwenye think capacity oa ndgu
 
Ndugu na Jamaa mie kiukweli kabisa nilioa huyo binti. Maisha na mapenzi mubashara sana. Ndoa ina heshima sana. Full respect in all direction. Na tumeshazaa watoto wawili. Mtoto mkubwa atafikisha miaka mitatu ikifika February, mdogo atafikisha miaka miwili ikifika March, 2019. Next year July nawabeba wote waje kuungana na Mimi nikiwa China kimasomo ya PhD. Na nina mpango nikirudi TZ baada ya shule kuisha nitampeleka mkewangu shule awe na elimu ya form 4 kisha tutaangalia mipango mingine. Asanteni mlionishauri nioe. Naona sijakosea kabisa.
 
mke hasomeshwi
 
Mkuu, kiwango cha Elimu hakipimi ubora wa mke, tuliza akili fanya uchaguzi sahihi
 
Back
Top Bottom