Mimi nina masters nataka kuoa Darasa la saba

Swala la uaminifu halina uhusiano wowote na elimu.

Huyo wa darasa la saba pia anaweza asiwe mwaminifu. Msomi mwenzio pia anaweza asiwe mwaminifu.

Usioe elimu kiongozi, oa mke. Mke mwema hutoka kwa Mungu, sio darasani.

Dogo atuambie Ana master ya nini..... isije ikawa ya kushinda JF 24/7
 
Maisha ya ndoa hayana darasa wala kidato,elimu sio kuishi,hakuna uhusiano kati ya maisha ya ndoa na elimu dunia...kikubwa Anglia umempenda?hayo mengine baadae..
 
Jamani wanajamvi naombeni Mawazo yenu. Kuhusiana na kichwa cha habari hapo juu, mie ni Muislam, nilioa Mwalimu wa Primary nikaachana nae baada ya kubaini anafanya Ngono na afisa Taaluma wa Jiji.
Nimepata binti aliyeishia Darasa la saba. Nipeni uzoefu haya Maisha yatakuaje kwa gepu hilo kubwa la elimu.

Nawasilisha.


Tarajia cost kubwa itakayotokana na ujinga!!!
 
Kama hivo afadhali.
Unajua ni kwa nini? Kwa uzoefu wangu mvulana au msichana aliyekulia mjini ana exposure kubwa zaidi kuliko wa kijijini.Na generally waalimu wa shule za mjini wanafundisha kwa bidii zaidi kuliko wa vijijini.

Mdogo wangu daktari alioa msichana wa darasa la saba la kijijini.Daktari alipata shida sana ya kuendana na mkewe kimtazamo na kimaisha. Alifunga dstv nyumbani kwake akawa anatazama sana vipindi vya sayansi: discovery,nk.Mkewe akawa analia kwa kusema anapunjwa anataka atezame Mambo Hayo ya Bishanga na Tausi ya akina Dama.Mumewe alipata shida sana.
Hapo tatizo si elimu ila walitofautiana interest", kila mtu ana interest yake hata wote mkiwa maprofesa. Na kwa ufahamu wangu interest haifundishwi darasani
 
Kwani kwenye Masters hamjasoma itakuwaje ukioa la saba..kama bado endelea kusoma Misters
 
Huyo wa la saba akikutana na mashangingi ya jiji utalia. Waendesha bodaboda wafyatua tofali wauza bucha wrote wake. Angalia tu mwanamke msomi anayejitambua.

Mbona mababu zetu na bb zetu hawakugusa hata hilo la saba na ndoa zao zilikuwa zina uaminifu. Na hawa walosoma leo mbona ndo wanaoongoza kwa michepuko. Ni akili ya mtu tu na kujitambua.
 
Nadhani shida yako ilikuwa kututangazi elimu yako tumekusikia mapenzi na elimu wapi na wapi
 
Mkuu,ishu ya ndoa haijalishi cha Amesoma au hajasoma,Jambo la msingi mwombe kwanza Mwenyezi MUNGU,akusimamie ktk kumpata
 
Tayari umeshatengeneza ubaguzi na dhambi hiyo itakutafuna, kama kweli unampenda sidhani kama kulikuwa na haja ya wew kuja hapa, cha msingi sikiliza moyo wako kwani nyumban kwako una office kwaiyo lazma uoe mke mwenye elimu sawa na wewe. Elimu haina tatizo muhimu ni hekima huyo wa la saba anaweza kuwa na akili na ushauri mzuri wa maisha kuliko hata mwenye degree
 
Back
Top Bottom