Mimi Nikipewa Yanga au Simba tunasumbua sana Champions League kwa style ya Enyimba, Mamelodi Sundows, Diamond Platnumz

FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
8,822
33,515
Habari wadau,

binafsi ni mshabiki wa yanga miaka mingi. Simba ni watani wangu japo tabia zetu zinafanana ndio maana tunaishia kushindana wenyewe kwa wenyewe mchangani huku

Natamani sana kabla sijafa nije nione mechi ya simba na yanga ambayo sio ya ligi kuu wala kombe lolote local

natamani mechi ya simba na yanga taifa iwe ya nusu fainali ya ligi ya mabinga Africa. Ile tumewatoa sana watu mwisho wa siku tunakutana wenyewe kwa wenyewe. Kama real madrid vs barcelona UEFA, au Chelsea vs liverpool UEFA.

hata africa inawezekana sana na game zinakuwakaga kaliii balaa.. eg zamalek na al haly wakikutana caf champions league vurugu la mashabiki hapo misri hadi wanapigwaga mabomu ya machozi. Why not this in Tanzania?

Mchawi mkubwa wa Yanga yangu na watani zangu Simba ni Poor Management, matumizi mabovu ya scarce resources, matajiri ambao hawana nia ya dhati ya kuzikomboa hizi timu, na fikra mbovu za TFF

Mimi nikipewa yanga leo niwe decision maker wao.... nita cut vitu vingi sana kama Uncle Magu vile na hela nyingi nitaipeleka kwenye salary na bonus za wachezaji, gharama za hotel na usafiri wa timu.

Mambo yote yasiyo na msingi sipeleki hata sentii, hii ndio style iliyoipa enyimba ubingwa wa caf champions league mwaka 2003 na 2004.

Sina takwimu nzuri ila Yanga yangu inasemekana ina wanachama zaidi ya milion 1.. na mashabiki ambao sio wanachama zaidi ya milioni 6.

Naweza kutumia huu mtaji wa mashabiki na wanachama tu kupata hela za kuendesha timu mwaka mzima bila kumtegemea manji.

humu kuna mauzo ya jezi, humu kuna kadi za wanachama, humu kuna michango tu ya wanachama na mashabiki watakaoguswa. Kuna fund raising kwa watu tofauti tofauti ambao ni mashabiki, alumni na fans wa yanga ambao ni wana uwezo kifedha.

Na style ya pili baada ya kulipa wachezaji vizuri na kwa wakati. Naweka mfumo wa ukicheza chini ya kiwango nakutimua naajiri mwingine.

Na kila ushindi ukipatikana wachezaji wote wanagawana bonus nzuri tu.

Why nimeweka mfano wa Diamond Platnumz pia. Nitarudi kueleza mbinu yake aliyoitumia kutawala Africa, kwamba hata kwenye soka inafanya kazi ikitumika kwa timu zetu.
 
Safi! Inasikitisha sana tokea tupata uhuru hakuna klabu yoyote kongwe Kati ya Simba na Yanga iliyofanikiwa kunyakua kombe la klabu bingwa Africa au Shirikisho sisi tumebaki wa mchangani tu. Tumejiloga wenyewe
 
Safi! Inasikitisha sana tokea tupata uhuru hakuna klabu yoyote kongwe Kati ya Simba na Yanga iliyofanikiwa kunyakua kombe la klabu bingwa Africa au Shirikisho sisi tumebaki wa mchangani tu. Tumejiloga wenyewe
Mkuu, Africa kuna nchi ngapi? Nchi ngapi zimefanikiwa kuchukua ubingwa wa africa kwa ngazi za vilabu?
 
kwanini hayo mengine hayakuhusu wakati hilo kombe unagombea na "hayo mengine"?? sasa kama hutaki kutambua chochote kuhusiana na wapinzani wako na nafasi yako dhidi ya wapinzani wako wewe utakuwa mshindani wa namna gani??
Naamanisha si kazi yangu kujua hao wengine wamechukua au hawakuchukua naangalia upande wangu
 
Naamanisha si kazi yangu kujua hao wengine wamechukua au hawakuchukua naangalia upande wangu

Ndugu yangu, hakuna ushindani usioangalia unashindana na nani!kutokujua unayeshindana nae ni sehemu mojawapo ya kushindwa.lazima ujue wenzako wako wapi na wanafanya nini,wamefanikiwa kipi na kipi hawajafanikiwa na kwanini,hapo ndipo utajua ufanye nini ili upate nini.Umeshawahi kusikia kitu kinaitwa S.W.O.T Analysis?
 
ndugu yangu,hakuna ushindani usioangalia unashindana na nani!kutokujua unayeshindana nae ni sehemu mojawapo ya kushindwa.lazima ujue wenzako wako wapi na wanafanya nini,wamefanikiwa kipi na kipi hawajafanikiwa na kwanini,hapo ndipo utajua ufanye nini ili upate nini.Umeshawahi kusikia kitu kinaitwa S.W.O.T Analysis??
Sawa!
 
Mkuu, tusipende kuikimbia hali halisi. Hata mimi ni Yanga hasa. Tuseme katika hao million moja, wangapi wanalipa ada ya Shs 2,000 kwa mwezi? Nusu yetu kiasi cha watu laki 5 tukilipa ada kwa mwaka,itapatikana billion 6.

Angalia wenzetu na mfumo wao mpya. Naambiwa hisa moja ni laki 4. Wangapi watanunua hisa hizo.
Wakati wa uchaguzi ndiyo wanachama hulipiwa ada iwe Yanga au Simba. Tunayo Safari ndefu kwa kweli.
 
Back
Top Bottom