Mimi ni mwanabaiolojia na huu hapa ndio uthibitisho wa uhalali wa Mungu(2)

Uhakika Bro

JF-Expert Member
Mar 29, 2022
2,389
3,052
Kuna mtindo wa kwenye social media watu kutosoma maelezo marefu sana. Hivyo basi nimeamua kuileta sehemu tu ya ile sehemu ya pili, enjoy;
sense-2326348_1920.jpg

....................kukazia pointi kadhaa na kufunga;
Ndugu zangu, haidhuru mtu au mfumo kutokujua mwisho au mwanzo wake ili kuleta maana – ‘sense’. Maana inakuja pale kipande cha mfumo husika utakapokuwa unatenda kulingana na muelekeo sahihi ukiuchukulia mfumo mzima juu kabisa hadi chini kabisa. Sense ni ule tu uelekeo sahihi basi. Hata kama labda moyo unafahamu tu kwamba ‘ulimwengu mzima’ ni wenyewe tu na ukajijali wenyewe tu hautakuwa na maana tena mwilini. Lakini ukawa na akili ya kuelewa kwamba kuna mfumo mzima wa mishipa na kazi yake ni kuisambazia hiyo mishipa damu basi tayari utakuwa na maana na utaishi. Utaishi vizuri hata kama haujawahi kuiona mivitu migumu kama mifupa [damu yenyewe inatengenezwa huko]. Moyo ukasema wenyewe unajua kuna nyama tu na nyama ndiyo kila kitu kilichopo. Utaendelea kuishi huku ukilindwa na mifupa hiyohiyo uliyoikataa kwamba haipo na haina maana yoyote. Lakini ukitaka [ufe huo moyo] ni pale utakapofanya kitu ambacho ni non-sense yaani kinyume na ukweli wake. Mfano ukaamua kunyonya damu badala ya kuisukuma. Au kuji mwambafai na kujipa umuhimu wa kwanza badala ya kusambaza damu wenyewe ndiyo uitumie damu kukua na kuitumia zaidi. Kujitukuza kujipa umuhimu wa kwanza wewe badala ya vyote sio jambo zuri. Maana viungo vipo kwa ajili ya viungo wenzake na kwa ajili ya lengo la jumla la kuwepo kwa huo mfumo. Kwa hiyo tukirejea kwa mwili tutasema moyo ni kwa ajili ya mapafu, miguu, mikono, ubongo, moyo na mwiliwote na mtu mzima kwa ujumla. Kwa hiyo moyo unaweza kusema kuwa lile wazo la mtu ndiyo mungu. Mungu wake anaonekana kuwa tofauti kabisa na asili ya moyo wenyewe ulivyo kwanza haonekani wala hashikiki.

Mfano wa seli pia ni hivyohivyo mitochondria ipo kwa ajili ya ribosome, nucleus, membrane, mitochondria yenyewe na seli nzima kwa ujumla wake. Mitochondria akiongeza ujuzi wake atagundua kuwa hata ile idea nzima ya seli sio mwisho. Ni mungu wake kwa level fulani lakini sio mwisho. Atagundua kwamba zipo seli nyingine pia mwilini mamilioni na mamilioni nazo zina mitochondria zake na zoote zinafanya kazi kwa ajili ya kuuendeleza huu mwili mzima. Ndio zinaonekana kama zimaulisha ubongo wa mwili huo lakini ukitizama kwa makini utagundua kuwa hata ubongo unafanya kazi kwa ajili ya mtu ambaye ni jitu zima limalotawala seli zooote moja moja katika makundi. Lakini hapohapo ukipindisha kidogo kubadili mizania ya utazamaji unaweza kusema kuwa huyu mtu naye yupo kwa ajili ya kuvitumikia hivyo viseli [na vimitochondria] vyoote mwilini mwake ili viendelee kuishi. Nayo sio mbaya ukiamua hivyo kwa sababu huo pia ni ukweli na ni kitu kilekile tunachokisema kila siku. Na huyu mtu ameonesha kuwa yuko na upendo woote na kujali kote na uangalizi wote kwa viseli vyote vilivyo chininya uangalizi wake. Kwa hiyo kwa viseli vya mwili mtu ni Mungu wao.

Tukibakia hapohapo ona jinsi mambo yote yanavyopata majibu ya wazi kabisa. Tunaona ni sahihi kwa seli hai nyekundu za damu kufa kila zinapotimiza wastani wa siku 120. Sijui kama zinalalamika au zinaumia kufanya hivyo sijui. Lakini inaonesha kuwa zimezaliwa zimemtumikia mungu[mtu] na mwisho zimekufa zitaacha nyingine zikifanya kazi. Zitazaliwa seli nyingime. Haya ikatokea mwili umevamiwa na wadudu hatari. Tunaona rasilimali muhimu kwa matumizi ya seli nyingine zikibadilishwa njia na kupewa askari [chembe za kinga] ili zikapambane na wavamizi. Labda seli nyingine huwa zinanungunika na kuleta migomo ndio maana sababu tunaona mwili ukinyon’gonyea. Mfano ni kichwa ndio kinauma au ni damu ndiyo imeambukizwa maralia. Lakini misuli ya miguu, tumbo na viungo vya uzazi vyote vinalala, si hamu ya chakula wala ya kula inayobakia. Au mfano wa pale ambapo mwili unapoamua kuviua vipande vyake vinavyotaka kuleta shida kwa mwili mzima. Mfano; seli zilizokaidi kufa zenyewe zikaamua badala yake kukua tuu pasipo kujali zinaleta faida wala hasara kwa wenzie. Zenyewe zinachojua ni kula kunenepeana na kukua zaidi na zaidi. Kila aliye jirani nazo anaumia tena anachukizwa na uwepo wake. Muda utafika mwili utaamua kuziua japo kutokana na mapendo makubwa utafanya hivyo kwa maumivu makubwa sana. Ukisikia kansa inatesa jua kwamba kansa inatesa kweli kweli. Ni maumivu makali na ndio maana wanaoiugua huwa wanasemwa kuwa ‘they are battling cancer’ ni vita! Lakini hata yanapotokea haya tunapaswa tutambue kuwa yote ni katika upendo tu wa baba yao hizo seli mtu mwenyewe. Maana kwa upendo anaidhinisha seli mbaya ziuwawe hata kama zinazobaki zitayapata maumivu hakuna namna. Yote haya yangeepukika kama seli mbovu zitaamua kufa zenyewe kwa upendo kuwaachia wengine waishi. The key hapa ni upendo. Mungu ni pendo walishasema. Hata kama kwa upendo ataamua kwamba wacha tu vyote viishi [ambavyo mara nyingi hutokea] na mwishoni atauvunjavunja mwili wote huyu mtu katika kifo nao ni upendo. Sema tu namna hii ya pili itawaacha wale seli wengine na mateso makali hadi kufa kwao. Seli wazuri wamapoumia na mtu naye anaumia lakini kwa upendo anavumilia.

Panda hatua moja tuje kwa binadamu binadamu anaweza kujihisi kwamba yeye yupo na anajifanyia kazi kwa ajili yake kwa faida zake lakini hilo jambo haliwezekaniki. Kwanza tukianza tu kwenye kufanya kazi mara nyingi ni kuwatumikia wengine. Mfano umejiajiri unanyoa nywele unawanyoa wengine. Unapika mamantilie umawapikia wengine. Mganga anawatipu watu wenzake wanaomzunguka. Kwa kufanya hivyo unafanya kile ambacho Mungu anataka; kuwatumikia wengime na kumtumikia yeye. Na Mungu naye anajishughulisha na kuendelea kuwepo kwa sisi wote duniani pamoja na vyote vinavyotuzunguka ili tuendelee kuwepo kwa ujumla wake. Wanazaliwa wanadamu wengine wengine wanafariki. Wote tunapendezwa na kukua na maendeleonya kiuchumi. Mungu pia anayafurahia hayo ikiwa yanaleta hali nzuri kwa wote viumbe, wanadamu na mazingira. Wote wanadamu, majirani na Mungu huchukizwa pale mtu anapoamua kukua tuu hata kwa madhara kwa watu wengine. Mtu ambaye badala ya kuwatumikia watu ataamua kuwatumia watu kujikuza pasipo faida yoyote kwa watu na dunia kwa ujumla anaenda kinyume na mantiki senseless. Basi yanaweza kumpata mabaya kutokana na mifumo tuliyojiwekea labda mwizi atafungwa gerezani. Au kuugua kutokana na matumizi yaliyopitiliza ya chochote hadi akajiharibu. Au kwa upendo akaachwa aendelee kuishi japo hii itakuja kwa gharama ya maumivu ya wale wengine wote wenye kuwa wema machoni pa Mungu. Lakini mwisho wa siku utakuja na kila kitu kuvunjwavunjwa na hukumu kupitishwa.

Baada ya kufa sasa ndiyo kila kipengele kitajihukumu kutokana na kiwango kilichofuata hiyo mantiki. Kama kilifanya vyema ni furaha tuu milele na kama kilifanya visivyo ni shida tuu milele. Kama ambavyo sisi binafsi hufanya makosa na kuumia nafsini. Na wakati mwingine kutamani kurudi nyuma na kurekebisha makosa. Labda ni kweli huwa zinatolewa nafasi za pili ili kuja kurekebisha makosa hilo sina hakika japo uwezekano ni mkubwa wa ukweli huo. Au labda kile kilichotenda vibaya kinarudishwaga tena levo ya chini ili kikajifunze kutenda mema baadaye kitapandishwa. Kwa usemi huohuo na kile kilichotenda vema basi kitarudishwa katika levo ya juu yake maana kimeuthibitishia mfumo kwamba kinafahamu lengo lake. Aliye mwaminifu kwa kidogo tunaweza kumuongeza majukumu zaidi maana tunamuamini au sio? Wapo watu wanaoamini hivyo. Mfano labda kwenye ufufuo ile kuvikwa miili mipya itakuwa na zile taarifa za seli zilizofanya vizuri wakati wa uhai wake. Maana tofauti na kufanyiana kazi hapa duniani tupo pia kwa ajili ya kujifunza kitu fulani.

Basi ndugu zangu nahitimisha; kama ambavyo neutroni zipo kwa ajili ya protoni, nyutroni wenzake zenyewe na ulimwengu mzima kwa ujumla. Ndivyo ambavyo atomu nzima ipo kwa ajilinya atomu wenzake, lengo fulani la uwepo wa maada na ulimwengu mzima kwa ujumla. Ndivyo ambavyo seli zipo kwa ajili ya seli wenzake, viungo na tishu mtu na dunia na ulimwengu mzima kwa ujumla. Ndivyo ambavyo sayari zipo kwa ajili ya zayari nyingine, vimondo, jua na lengo zima la kuanzishwa kwa sayari na mfumo wa jua na ulimwengu mzima kwa ujumla. Ndivyo hivyohivyo ndugu zangu magalaksi yapo kwa ajili ya magalaksi mengine na gesi, na nafasi na ulimwengu mzima kwa ujumla. Basi kwa mfananisho huo mimi nasema wazo la Mungu ni wazo halali kabisa na linaleta mantiki kuliko ile kuwepowepo tu bila lengo lolote, bila jukumu lolote. [Ili unielewe basi rudia hii aya ya mwisho ukibadili [replace] neno ulimwengu mzima kwa ujumla na neno Mungu.] Mungu yupo ndugu zangu Mungu yupo. Nakubali kuwa anaweza kuwa katika muonekano tusioweza kuung’amua kisawasawa hadi inapelekea kuambizana sisi kwa sisi kuwa hachunguziki. Ni sawa lakini lile wazo la kwamba yupo linabaki palepale. Na sifa zake za kuwa na upendo wote na ujuzi wote ni sahihi kabisa. Kuwepo pote hiyo ndiyo haswaa imejionesha katika makala hii ndefu. Hata kama sayansi au watu wataamua kumficha mbali juu kabisa infinity au kumficha chini kabisa infinitesimall bado Mungu ataonekana tu kwa sababu yeye ni mwanzo na mwisho, hana mwanzo wala mwisho ni hamna na ndo kila kitu. Ukivichunguza vitu vikubwa juu kabisa yako utamkuta mungu. Na hata ukivichunguzwa vitu vidoogo vya wewe na chini yako utamkuta Mungu pale. Somo lolote ukilichukua ukalifafanua ukalisoma na ukalichunguza mpaka mwisho wake utamkuta Mungu. Kwa hiyo iwe ni baiolojia, fizikia, filosophia mwisho utamkuta Mungu. Nawasilisha.
AAA_7510.jpg

Kuna mtindo wa kwenye social media watu kutosoma maelezo marefu sana. Hivyo basi nimeamua kuileta sehemu tu ya ile sehemu ya pili, enjoy;
View attachment 2174800

View attachment 2174803
Ni mjinga tu, aliyepotoshwa akakubali kupotoshwa,anayelipwa ujira ili apotoshe, aliyedanganywa kwamba Lucifer ndiye Mungu na kila kitu hupatikana kwake, ndiye anayeweza kusema hakuna Mungu. Otherwise common sense tells us that there is a God who created everything, and this is the God we worship.
 
uwezo wa mtu kufikiri unapimwa na yeye kuamin kama mungu yupo au hayupo hakuna binadamu mwenye akili timamu aseme Mungu hayupo
Hakika, binadamu mwenye akili timamu ni lazima amuamini Mungu yupo kwa namna moja au nyingine. Binafsi nitamuelewa mtu yeyote atakayesema Mungu yupo hata kama tutatofautiana naye suala la yukojekoje, hilo halina shida.

Maana najua kila mmoja anamuona Mungu kwa namna yake kulingana na anachokijua zaidi. Ni kama tu wale vipofu walivyokuwa na picha tofautitofauti za Tembo. Mmoja alijua yupo kama sahani kubwa [ aligusa sikio], mwingine akaonelea kuwa yupo kama mkuki mkubwa [aligusa pembe/tuskers], mwingine akasema ni kama nyoka [mkonga], mwingine mti. Lakini ukiangalia tembo sio hivyo vitu exactly. In fact ni hivyo vitu vyote na zaidi na zaidi. Badala ya kubishana, wangesikilizana labda mwisho wangejenga taswira halisi ya Tembo
 
Ni mjinga tu,aliyepotoshwa akakubali kupotoshwa,anayelipwa ujira ili apotoshe,aliyedanganywa kwamba Lucifer ndiye Mungu na kila kitu hupatikana kwake,ndiye anayeweza kusema hakina Mungu.Otherwise common sense tells us that there is a God who created everything,and this is the God we worship.
We just have to keep re-informing these brothers who are misled to return to their senses. All is not lost
 
Ongea na Mungu mwambie kule Ukraine watu aliowaumba Putin anawaua kinyama bila huruma yoyote. Mbona Mungu kanyamaza
Sijui kama sisi hapa tunaifahamu kwa undani vita yao mpaka tuitolee hukumu kwamba 'anawauwa bila huruma' labda Putin anaumia naye [raia wakifa] sijui. Bila kusahau kuwa Putin nae kaumbwa na Mungu.

Tukirejea kwenye swali lako asee kila jambo lina kusudi lake. Halafu nisiendelee sana, nikuulize tu wewe unataka kumpangia Mungu cha kufanya? na namna ya kuenenda? Labda umuombe ila sio kumpangia bhana
 
Kuna supreme power governing the universe .....
Ila nachelea kusema kwamba ni mungu.
Tuko pamoja mimi nakubaliana na wewe kabisa wala sina kipingamizi kwa sababuu; It doesn't matter by which name you call God. God is God.

Hichohicho unachokijua wewe nenda deep [sijui high? vyovyote tu juu au chini nisawa tu!] kichunguze kadri uwezavyo mwisho pale mbele utamshuhudia Mungu waziwazi. Endelea halafu share na sisi tuzidi kumfahamu zaidi pia.
 
Hayo maelezo bado ni marefu sana, jaribu kufupisha
 
uwezo wa mtu kufikiri unapimwa na yeye kuamin kama mungu yupo au hayupo hakuna binadamu mwenye akili timamu aseme Mungu hayupo
Ni imani tuu, na nyie watu wa imani mnajifanyaga mna akili sana kumbe mnaonekana mataahira tuu na mnapigia watu makelele na nyimbo zenu mnazoimba usiku kucha kwenye mikesha yenu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom