Mimi ni mwalimu, naacha kazi nijiajiri

Sio mihemko anawatia moyo wengine ambao wana woga wa kuthubutu! Pia hapa atakutana nawalio tangulia kuacha hapo awali wampe mbinu nyingine!
Moyo hautiwi kwa namna hiyo aisee, kama unajua kifuatilia vizuri uandishi ukahusisha na emotions za mwandishi, utagundua jamaa yetu mpaka anaadika alikuwa na stress nyingi
 
Kuna baadhi ya members humu JF ni wajinga wajinga tu kama wajinga waishivyo.
Binafsi wazazi wangu walikuwa Walimu though by the time Baba yangu nyakati za mwisho wa uhai wake alikuwa akitumikia kama Afsa Elimu Wilaya na alibakisha miaka 4 kufikia ukomo katika ajira ya utumishi wa umma.
Mama yangu ni mstaafu kwa sasa.
Nakumbuka kipindi nahitimu kidato cha sita(2004 SONGEA BOYS) mimi na wazazi wangu tulisigana sana kuhusu kipi napaswa kusomea chuo kikuu make walikuwa na uhakika lazima nitapass. Wote waliafiki niwe mwalimu kama walivyo wao!
Binafsi sikutaka kabisa ajira yoyote iwayo amma lah iwe kama daraja tu! Kweli Mungu ni mwema alijaalia nikapata div II nikawa enrolled kusoma Accounts na mwishowe nikaajiriwa kuwa Assistant Accountant kwenye kampuni ya Wazungu. Baada ya miezi15 nikapiga chini na kurudi mtaani mpaka leo hii.
Ninayo mengi sana ya kuelezea but i reserve them all execept to all who deserves like this guy Felice1
Mdogo wangu usikatishwe tamaa na watu waoga njoo ntakupa shamba, waterpump n.k bure.
Uko wapi boss!! Naomba hiyo fursa ya pump na shamba!
 
Ninyi mnaomsema mwalimu ana mshahara mdogo...niambieni kada IPI Ina mishahara mikubwa serikalini???? Na je iweje uanze kazi Leo upate mshahara mkubwa?? Kumbuka ualimu ni wito istoshe si walimu wote wanafanana mishahara!!! Mwisho jiulize wewe unaemsema mwalim nyumbani wazazi wako ni mabalozi au wabunge??? NB Kabla hujaongea fikilia nini unataka kuongea na akina nani unaongea nao!
 
Ninakaribia 30. Nafundisha sekondari, somo la Basic Mathematics. Sina furaha na kazi yangu kwa sababu kipato hakiendani na kasi ninayoipenda. Nimegundua kuwa na degree hakuendani na kipato. Bado tunatishwa tishwa. Walimu nimegundua ni waoga. Hasa kufanya maamuzi magumu na sahihi. Mwalimu wa Tanzania anaishi kimaskini. Naacha kazi, naenda kujiajiri mwenyewe. Kwa heri utumwa, Kwaherini walimu. KWAHERINI. Usiniige kama hujajipanga. Nina sh milioni 2. naenda kuipanda. Hii sio ndogo kwangu. Sirudi tena kufunza.
Hongera hayo ndo maamuzi magumu tena yenye tija kama unajua unachoenda kufanya kila la kheri chief
 
kama ni hivyo mbona huu mshahara unafanya mambo mengine kabisa naona baadhi ya shule za binafsi mishahara huwa hiyo laki 7, kuna watu wanalipwa laki 3 na wanaishi fresh.
Kuwa na mshahara mkubwa haimanishi utatimiza malengo yako malengo yanatimia hata ukiwa ukiwa na mshahara mdogo cha mhimu ujue namna yakuupangilia
 
Unataka kujiajiri for wrong reasons na kufikiri kujiajiri ni kuakimbia matatizo yako. Kijana you need a mentor ambaye ni mfanya biabishara akupe A to Z kisha ufanye ifnrmed decision. Biashara inahitaji uifanye kwa moyo ndo utafanikiwa na si kwa sababu ilizozitaja hapo juu. Ushauri wangu mtafute mtu aliyefanikiwa ndo akupe ushauri don't seek advice from losers
Asante kwa ushauri wako kuhisi sio kugusa
 
Shamba lipo Moro maji ya uhakika ardhi yenye rutuba kuvuna 100% guaranteed.
Mkuu upo Mori sehem gani. Mi naishi Iringa natafuta sana sehemu ambayo naweza kupata shamba zuri lenye maji kwa kilimo. Morogoro niliwahi kuplan kuhamia huko lakn mambo yakakwama nikaahirisha. Mkuu naomba mrejesho wa sehem gani nzuri
 
Back
Top Bottom