Mimi ni mtanganyika, siupendi muungano natamani ufe

MASIKIN JEURI

Senior Member
Jan 31, 2013
134
22
Haya niyangu kutoka kumtima wange, Wazanzibari kwa dharau wanatuita wa bara au Tanzania bara. hawa watu tunawapa umeme buree, tunabembeleza muungano kwa gharama nyingi sana, wazanzibar wana serikari yao ya mapinduzi, inayotunga sheria zao, budget yao, na mambo lukuki kwa faida yao, afu wanataka fikra za serikali yao tuzi adopt wa Tanganyika kwa manufaa yao na machache ya Tanganyika. tumeng'ang'ania muungano eti kwa sababu za kiusalama, nikitu cha kushangaza. bona hatujaungana na Kenya, Rwanda Msumbiji, Malawi, Zambia, DRC, Burundi, Unganda na tunaendelea na mwendo mdundo. kama ikitokea fyokofyok si tunajeshi, sasa wuoga wa nini? kama Muungano hamtaki ujifie mbali serikali tatu ni suluhisho la kelo hizi. Serikali ya Muungano inaweza ikafanywa kuwa serikali ndogo tu, kama serikali ya wawakilishi ya watu wachache kutoka Tanganyika na watu kutoka Zanzibar. mchezo unaisha.


Nawasilisha
 
So muungano ukifa Wazanzibar waliopo huku kwetu itabidi waombe uraia na vivyo hivyo wabara waliopo Zenj sababu kuna watu wamejenga nyumba zanzibar na si wa huko na tupo na wazenji kibao mitaan kwetu huku.
 
So muungano ukifa Wazanzibar waliopo huku kwetu itabidi waombe uraia na vivyo hivyo wabara waliopo Zenj sababu kuna watu wamejenga nyumba zanzibar na si wa huko na tupo na wazenji kibao mitaan kwetu huku.

Waala hiyo siyo sababu yakusitisha ndoa hii. kwani wewe ukitaka kuishi Kenya au Uganda unashindwa nini. je hakuna waarabu au wazungu wanaoishi tz. bila shaka umenisoma
 
kuna thread humu ya madau filbonde inasema,
"Kwa kweli nimelazimika kuandika hivi kwa kuona sisi wabara wengi saana tunapenda kuwaponda na kuwachukia wazanzibar,lkn kwa utafiti tu mdogo wale woote wanaowaponda ni wale waliokuja dar ukubwani au walikuja kwa kusoma na kwa kazi,mm ni mzaliwa wa dar na dar ndio kwetu halisi na nipo tangu mwaka 1962,tukitaka tusitake hawa wazanzibari ndio waliotustaarabisha sisi wabara,watu wa kwanza kuwa na ustaarabu wa hali ya juu ni wazanzibar kwa afrika mashariki na kati na kusini,watu wa kwanza kuja kututoa tongo za macho sisi wa bara ni wao,kila unachokiju cha electroniki kilianza kuletwa na mfanyabiashara mmoja anaeitwa ba Hamadi ambae aliwahi kukamatwa kuingizwa tv na video bara,wakati huo aliambiwa sio ruhusa na marufuku,baada ya kuruhusiwa pia akawa wa kwanza kuingiza vitu vya electonic vyooote mnavyovijua tz,wakati huo watu wote wanaenda mjini kushangaa tu dukani kwake,hizo tv,friji,video,mashine za kufulia,mafeni,aircondition,re dio kubwa kubwa,vyote kwa mara ya kwanza viliingizwa na wapemba,na wapemba ndio waliowafundisha ndugu zetu wa kichaga kwenda nje kwenda kuchukua bodhaa,magorofa makubwa makubwa ukiachia majengo ya serikali wao ndio wakwanza kuanza kujenga,km leo mnapaona kariakoo majengo marefu msidhani wachaga na sisi wazaramu,ni wapemba wale,leo hii mtu anaporoja tu eti wapemba wasumbufu bara,ujue huyo katoka mikoani na anajifanya mtoto wa mjini saivi,tuulizeni sisi wazawa wa dar es salaam tunajuwa mengi sana khs hawa ndugu zetu na sio wale wakuja from mikoani."


  • ipitie mkuu
 
Last edited by a moderator:
Mimi nataka muungano ufe hata Leo mambo ya serikali tatu ya nini!! Nahitaji Tanganyika yangu nchi ya babu yangu siitaki Tanzania ningeweza hata sasa ningeuvunja! Natamani kiwe na kura ya maoni nitafanya kampeni za uvungu kwa uvungu muungano ufe! Tuojenge tanganyika yetu!
 
Nimesoma gazeti moja la mwananchi, linasema ccm inagwaya serikali tatu, inasisitiza sera yake ya serikali mbili! napenda kuwashauri wana ccm wakubali mabadiliko. pia wajue katiba si ya chama Fulani lkn kwa manufaa yetu sote. katika picha aliyopiga Lwakatale akiwa anatoka mahabusu, ameshikiria kitabu kinachosomeka, "tough times never persist but tough people do"! hivyo ccm hata watoe sababu zao lkn mwisho wao umefika, naamini hata wakiiba kula mwaka 2015 sijui kama watabaki salama.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom