Mimi ni mmoja wa wahanga wa Country economy policy

falcon mombasa

JF-Expert Member
Mar 5, 2015
9,186
9,287
Wakuu habari,

Kwa hakika naomba nikiri kuwa mimi ni mmoja wa watu waliopata changamoto katika kipindi cha Rais Magufuli. Hii inatokana na sera zisizobashirika kuhusu uchumi,benki nyingi zinashindwa kuendelea kutoa mikopo hususani mikopo ya magari ya abiria kama ilivyokuwa zamani, benki karibia zote zimepoteza dira hazijui cha kufanya.

Nionavyo mimi kinachoimaliza Tanzania ni wingi wa propaganda kuliko uhalisia halisi wa hali ilivyo, chama cha CCM ni muhimu kubadili sera zake pia kwakuwa ndio kinaendesha nchi KWASASA, kiukweli wafanyabiashara wengi tumekuwa njia panda hata kuendelea kuwekeza au kufanya biashara Tanzania kutokana na risk of country economy policy imekuwa kubwa kuliko inavyozungumzwa kwenye vijiwe vya kahawa.

Nasikitika sana kama Rais halijui hili au wanaompa taarifa za uchumi wanampotosha kutokana na kugopwa kwake kama Rais.

Nasisitiza suala linaoendelea sasa kuhusu uchumi ni major extremely complex situation na hii inasababishwa zaidi na propaganda kuliko uhalisia.

Investors walio nje ya Tanzania huu ndio muda ambao wanajazwa chuki na nchi majirani wahasimu wa Tanzania.

Mimi licha ya kuishi Kenya na Tanzania hili nalisema waziwazi kwakuwa najua kama tukiendekeza propaganda atakayeumia sio rais mgufuli bali ni raia wa kawaida ambao tunawaachisha kazi

USHAURI:
Magufuli hupaswi kuwa mkali uliopitiliza kwakuwa watendaji wako wanashindwa kufanya mambo kwa uweredi bali wanafanya kwa kukuridhisha wewe.

Salam toka Mombasa, Kenya
 
Msinipangie!!! Ndio jibu lake. Kwa bahati mbaya serikali iliyopo haina mipango yoyote hata lile onyo la IMF wanaona kama propaganda mara nyingi hutoa majibu mepesi kwenye mambo magumu, inashangaza sana.
 
hii ndio karata inayotumiwa na mahasimu wa tz
 
Mkuu falcon mombasa hukumbuki kuwa mapato yameongezeka baada ya makontena kupungua bandarini? Kutoka kontena 40,000 hadi 1,000/ na bado pato limeongezeka mara kumi zaidi!!! Je siku tukipokea kontena moja tu kwa mwezi mapato si yatapaa mara hamsini zaidi? Hesabu za kisukuma ni tofauti na za kichagga mkuu!! Kisukuma ukitaka kukuza uchumi basi ondoa pesa zote za serikali kwenye mzunguko(Benki za kibiashara)kisha fungia pesa zote benki kuu!! Wakati wahindi wanatoa fedha central bank kwenda Baroda zikawakopeshe wakina Manji huko Tanzania ili wapate mtaji wa kuwakamua wabongo!
 
sasa kwahesabu za propaganda ndio zinadidimiza uchumi na kuwaumiza wananchi
 
USHAURI:
Magufuli hupaswi kuwa mkali uliopitiliza kwakuwa watendaji wako wanashindwa kufanya mambo kwa uweredi bali wanafanya kwa kukuridhisha wewe.

Salam toka Mombasa, Kenya

= uweledi

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
Wanabodi,
REPOA Wanajadili maendeleo na uchumi wa viwanda, wana live stream kwenye page yao ya FB
Tufuatilie ili tuweze kuchangia hoja zitakazo isaidia serikali yetu kupiga hatua.
 
Magufuli anatekeleza sera za kijamaa za chama chake. Msimlazimishe awe Mjaa passive. Huo msimamo wake ni kijamaa halisi. Kwani hatujui kama Chama cha Mapinduzi ni chama cha kijamaa?
 
Back
Top Bottom