Mimi ni dereva wa magari, nina cheti cha NIT na leseni daraja C1 na uzoefu wa kutosha

Yani jamaa una leseni kubwa na cheti juu ila hujui kuvitumia,ama kweli penye miti hakuna wajenzi
 
Kama unaelimu ya kidato cha nne jisajili katika tovuti ya utumishi ili nafasi zikitoka uombe. Hata sasa zipo nafasi za udereva huko
 
Umeonaaa eh? Yaani jamaa yupo tu kakaa kama boga!! Halmashauri kila leo wanatoa nafasi za kazi,au anangojea mpaka ashikwe mkono apelekwe kwenye gari kabisa,apewe funguo
Madereva wenye sifa kama zake na zaidi wapo wengi tu lakini hawapati hata daladala tu, kwaiyo msimlaumu na inavevekana hata hiyo C1 kaipata mwaka huu au mwaka jana ko huenda pia hana experience kubwa ya kuendesha magari makubwa ya abiria cha kufanya apambane tu asikate tamaa,
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom