Mimi ni dereva mzoefu, natafuta kazi

Mar 20, 2017
36
125
Habari ndugu zangu! wapambanaji na watafutaji wenzangu kweli kazi ni changamoto sana kupata, na hasa kama auna connection utasota sana itokee tu mkono wa mungu ukuguse!

Nina miaka 26 na naishi jijini Dar es Salaam. Nimekuja tena mbele yenu wana JamiiForums kuomba kazi ya udereva..elimu yangu mimi ni form four,mm ni dereva mzoefu sana sana. Nimeanza kazi ya udereva 2013 na nimepitia changamoto zote za kazi hii..naielewa vizuri sana. Ni kazi ambayo ipo damuni kabisa yani nahisi nimezaliwa kwa ajili ya kazi hii ila bado tu sijapata sehem nzuri ya kutoboa kimaisha.

Mimi nina uzoefu wa kuendesha gari ndani ya dar au nje ya Dar (mikoani). Pia nina uwezo mzuri wa kuzungumza na kuandika kiingereza na kifaransa kwa ufasaha zaidi.

Nina uzoefu wa miaka mitatu kwa kazi ya Uber, Bolt. Yaani wakati uber inaingia sisi ndio tulikuwa madereva wa mwanzo ambao tulipewa hadi simu kwenye account ya Uber nimetimiza trip 5400.

kwa kazi ya Uber imenifanya nijue jiji la Dar vizuri sana bila shida, Mimi sichagui sehemu ya kufanyia kazi hata mikoani naweza kuja kufanya kazi.

kwa mwenye uhitaji wa dereva kwa ajili ya

*kuendeshwa tu (binafsi)
*kampuni
*safari za mbali

tuwasiliane kwa namba 0769130951.
shukrani
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom