Mimi ndio mwenye nyota ya kusalitiwa, vipi wenzangu haya mnayapata pia?

Covax

JF-Expert Member
Feb 15, 2021
5,884
20,182
Tumezaliwa watoto watano kwa mama na watoto 9 kwa baba.Mimi ni mtoto wa tatu kwa mama na ni mtoto wa tano kwa baba.

Mimi nina bahati kubwa kwamba nimefanikiwa mapema kwa upande wa elimu na upande wa utafutaji mali, ila halimanishi kwamba ndugu zangu wote hawakusoma au hawana mali, wamesoma ila nimesoma zaidi yao with (MA in human resource). Wengine wana shahada na stashahada, mmoja form 4 drop-out, kwahiyo wanapokea mishahara yao ya kawaida (wage earners) wakati mimi ni self employed.

Mada yangu hapa ni kusalitiwa kwa mambo mengi kutoka kwa ndugu marafiki na mke najiuliza kwanini mimi? (why me alone) au pia na nyie mmeshawahi kusalitiwa?

Naomba mnipe uzoefu katika hili au kuna sehemu nakosea?

Usaliti wa kwanza

Mimi nilichelewa kuzaa na nilivyooa kaka zangu walikuwa na watoto wakubwa na nilikuwa katika position nzuri ya kuwasaidia, pesa nilikuwa nayo na nyumba kubwa nilijenga. Niliamua kuwasomesha hao watoto wa ndugu zangu bila tatizo shule za Engilish medium kwa sababu mimi naheshimu sana elimu kuliko kitu chochote. Mimi nina fikra kwamba "education is the key to success" kwahiyo niliwapa quality education kwa fikra ya kusaidia ukoo wetu pamoja na kaka zangu.

Nilidhani watanishukuru na kunipenda na tutakuwa wamoja, ila ilikuwa kinyume chake. Mpaka watoto wanamaliza form four baba zao hawajawahi kukanyaga nyumbani kwangu au kunijulia hali au kunipa 'word of appreciation'. Kilichoniumiza zaidi kuna kipindi vitoto vyangu vya kuzaa vinaanza chekechea narudi home wote na wale wa ndugu zangu wamerudishwa ada, nikamwambia wife kwamba hela iliyopo ni kiasi kadhaa hatuwezi kuwalipia wote, nikaweka msimamo wangu siwezi kulipia wa chekechea wakati wapo wa darasa la sita na tano kwahiyo nitalipia wa ndugu kwanza wa kwangu wiki njao. Maana yake my kids walipata (second priority).

Mtoto moja wa ndugu alifanikiwa kufaulu viziri na akawa pia anamlaumu baba yake kwanini haji hata kuwajulia hali nyumbani kwangu. Nikaona huyu mtoto tuna maono sawa sawa nikamuendeleza mpaka Chuo Kikuu kupata bachelor yake, nikawa na mu train kufanya biashara nakumpa majukumu ili ajifuze na azoee pesa. Mwaka 2018 sector binafsi ziliyumba kweli wengi tulipoteza mitaji na wateja, biashara zilizorota, malengo yalibadilika sio faida tena, ila kulinda mtaji wakati tunasubiri the 'dust to settle down'. Tukawa na matumaini kwamba biashara zitarudi tena vizuri, tulipunguza matumizi ili kulinda mtaji kwahiyo maisha ya nyumbani yalibadilika hatukuwa tu naenda supermarket tena kununua mahitaji tulikuwa tunanunua gengeni, tunapanda bodaboda kwa usafiri wa hapa na pale. Cha kushangaza huyu mtoto wa ndugu alinikimbia nyumbani na ku-niblock kwenye simu zake FB, Twitter n.k. Nilisikiaga tu kaanzisha mji wake Sinza.

Usaliti wa pili

Dada yangu alisoma diploma ya ualimu akaniomba nimfadhili ili asome degree apidishwe cheo na mshahara. Nilimlipia miaka mitatu karibia 4.7m kwa sababu alikua in-service hakupata mkopo. Siku ya mahafali yake aliwashukuru watu wote waliomsaidia hususani mume wake (a primary teacher) ila hakunitaja mimi wala hakutambua mchango wangu. Sitaki nieleweke vibaya kwamba nilitaka kusifiwa hapana, kama mtu pia inauma ku-sacriface kiasi hicho bila mtu kutoa recognition and appreciation kwako. Kwangu huo ni usaliti.

Usaliti wa tatu

Wakati biashara inaenda vizuri kuna mdada moja alikuja ofisini kuniomba kazi yoyote ili aweze kulisha mtoto wake; alikuwa singo maza aliyetelekezwa na mzazi mwezie. Tulimwambia hatuna kazi labda za nyumbani, ila arudi kesho tuone kama nafasi itapatikana. Aliporudi kesho yake nikamuhoji vizuri, kumbe alizalishwa baada ya form 4 alikuwa amefaulu vizuri. Nikashauriana na wife kwamba tumpe kazi za ndani ila jioni asome computer kozi atakuja kumsaidia wife kwenye kazi zake katika upande wa mahesabu. Kwa sababu she was too smart to be a house girl, alikubaliana na sie akawa sehemu ya familia. Tangu 2014 hadi 2017 alikuwa amepata cheti kizuri cha uhasibu pale CBE akawa tunamtumia katika kazi zingine za uhasibu na secretarial.

Mwaka 2018 biashara zilianza kuwa sio nzuri, kuna nyumba yangu ya wapangaji walishindwa kunilipa na nikakosa wapangaji kwa muda huo, nikamuomba huyu dada awe anakaa kwenye ile nyumba, niliweka vitu vyote muhimu kwa kuhamisha kwasababu tulikuwa na vitu vya ziada nyumba kuu.

Kuna kosa nilifanya hapa najilaumu tu kipato kilivyoyumba na ndoa ilianza kuyumba pia. Mke wangu alikuwa hanisikilizi kama zamani alinifanyia visa vingi but I wasn't ready kum-devorce kimkakati. Kuna siku nilikuwa nazidiwa hadi kuamua nisilale nyumbani kwasababu niliogopa naweza kupiga mtu hadi kufa na nikaiingia jela bure. So nikawa naenda kulala kwenye nyumba yangu nyingine kulikuwa na master bedroom.

Kama mara tano hivi sikuwa na wazo lolote la kumlala huyu singo maza, ila kuna siku moja nilienda pale mchana, kama saa nane hivi kupumzika kidogo. Hapo huyu singo maza alivyoingia chumbani mwangu kuniwekea sabuni duh kwakweli niliteleza (Mungu anisamehe stress za ndoa mbaya sanaa unaweza ukapata ugonjwa hata bila kujua) so it became a daily routine. Ila usaliti uko hapa huyu singo maza alipata ajira nzuri mkoani bila kuniambia, kaleta gari kahamisha kila kitu ndani na kuondoka. majirani hawakuniambia kwasababu walijua ni mpangaji ameamua kuhama tu, ila nasikia kajifungua mtoto wa kike sina uhakika 100% kama ni wangu, ila alinisaliti nilimsomesha nikamhifadhi nikamstiri ila kaondoka bila kuniaga na akanipora vitu vyangu. Baada kuuliza uliza kwao watu wanaowajua waliniambia hawara wa kisukuma wako hivo atakuachia hata pesa au hati kiwanja ila hatakuwachia vitu vya ndani kama sahani, vikombe, godoro, mashuka n.k.

Kwahiyo nilishapuuzia hayo yote. Na pia bado nina usaliti mwingine kutoka kwa ndugu marafiki ila nitawachosha bure.

Je, kuna wenye kusalitiwa kama mimi au ni mimi tu mwenye nyota ya kusalitiwa?
 
Pole sana, ila mkuu hujamalizia story yako...baada ya kuachana na hawara umerudi kwa mkeo,...au bado mambo ni moto?lol
Mke ni lishamrudia ila kanifanyia visa vingi sina mapenzi nae tena japo nimesharudi barabarani vuzuri ila instinct yangu ya ndani inamkata ila kumdvorce ni expensive kuliko kuka nae, kwahiyo naka nae kimkakati sasa hivi kalala yeye mimi niko sembuleni na chat saa 7 na nusu
 
Mke ni lishamrudia ila kanifanyia visa vingi sina mapenzi nae tena japo nimesharudi barabarani vuzuri ila instinct yangu ya ndani inamkata ila kumdvorce ni expensive kuliko kuka nae, kwahiyo naka nae kimkakati sasa hivi kalala yeye mimi niko sembuleni na chat saa 7 na nusu

Ndoa hizi jamaniii.....unawaona mtu na mkewe barabarani wako pamoja,kumbe wanaishi 'kimkakati' ... 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 umenichekesha sana mkuu na kunifunza pia..
 
ndoa hizi jamaniii.....unawaona mtu na mkewe barabarani wako pamoja,kumbe wanaishi 'kimkakati' ... umenichekesha sana mkuu na kunifunza pia..
Ndoa ni chagamoto mkuu, ndoa iki kushinda wakati huna pesa nyingi ukipata hera usithubutu achana nao kabisa, kwanza akili inahamia kwenye biashara, zako mke ana waza pesa zako na lini unakufa ndoa ya kimasikini ni raha kiasi fulani mnaishi kwa matumaini mengi.
 
umenikumbusha kitu. shemeji/wifi yenu nilimuoa akiwa na technician certificate,nikampeleka shule akapata diploma. nikamtafutia field nzuri sana akilipwa posho ya chakula na nauli. Akanipa nipitie ripoti yake ya field kama ipo sawa, nikaja nikagundua amewashukuru mpaka ndugu zake wa kijijini lakini mimi simo kwenye pongezi (ambaye nimemsomesha,nimemtafutia field,na hela ya steshenari).

Bro sisi binadamu ni wapumbavu sana,tuache hivyohivyo tu.
 
23 Reactions
Reply
Back
Top Bottom