Nasumbuliwa na fangasi (kama utangotango/mba) katikati ya mapaja

humblemimi

Member
Apr 14, 2021
7
5
Habari za majukumu wapendwa wana JF,

Mimi nasumbuliwa na fangasi (kama utangotango/mba) katikati ya mapaja, kulikopelekea sehemu hiyo kuwa nyeusi sana.
Fangasi hizo haziwashi bali zinakuwa kama unga unga, yaani kama ngozi inababuka, lakini haiwashi wala kutoa harufu.

Moderators kama naruhusiwa kuweka picha,nitaweka ili nipate msaada zaidi.

Nawashukuruni sana.
 
Sasa kama ushajua ni fangasi si uende kutatibiwe hospitali mkuu.

Fangasi ni fangasi Mkuu uite mba au uite fangasi unazunguka palepale. Labda kama unataka uthibitisho tu.

Tatizo la zama hizi ndo maana watu hata mahospitalini hawaponi wanakuja wanajua wanachoumwa, na vipimo na matibabu wanayotaka.

JF Doctor haitakiwi kutumika kama replacement ya Vituo vya afya. Hapa zaidi utapata ushauri ni nini ufanye au umeenda hospitali haujapona labda nini inaweza kuwa suluhisho.
 
Binafsi nimekata tamaa na hilo tatzo nimetumia kila tiba Hakuna nimeenda mapka agakhan nikukutana na professor wa magonjwa ngozi lakn hakuna nafuu ni zaid ya miaka 15 sasa na hilo tatzo now nimeamua ishi nalo tuu
 
Nilipo hospitali ni 106 km.

Kuna zahanati hapa ambayo haina daktari zaidi ya afisa msaidizi wa afya.
 
Binafsi nimekata tamaa na hilo tatzo nimetumia kila tiba Hakuna nimeenda mapka agakhan nikukutana na professor wa magonjwa ngozi lakn hakuna nafuu ni zaid ya miaka 15 sasa na hilo tatzo now nimeamua ishi nalo tuu
Pole sana ndugu.
 
tumia hii dawa hapa chini ikiambatana na yafuatayo
##kujikausha maji vema ukitoka kukoga
#zingatia usafi wa mwili
#fua nguo zako na zikauke vema
#epuka kushare nguo

maelezo zaid utayapata ukitembelea pharmacy inayoaminika iliyoko karibu na wewe

images%20(2).jpg
 
Nilipo hospitali ni 106 km.
Kuna zahanati hapa ambayo haina daktari zaidi ya afisa msaidizi wa afya.

Mm nimekulia kwenye Medical professional nakwambia moyo mmoja mkunjufu, Magonjwa ambayo ni magumu kuya Diagnose na kuyatibu ni Magonjwa ya Ngozi. Ndio maana unaona kuna Hadi madaktari bingwa wa Ngozi. Usitegemee utibiwe tatizo la ngozi kwa mitandao upone kirahisi, bila kuwa evaluated na daktari.

Kila kata kwa sasa ina Health Centre na Magufuli ameajiri Medical Officers(MO/MDs) 1000 wote wanapatikana vijijini kila kata, Tanzania nzima.

MD ni level ya elimu inayotambulika duniani kote hivo utapata quality service as if upo Mamtoni
 
Mm nimekulia kwenye Medical professional nakwambia moyo mmoja mkunjufu, Magonjwa ambayo ni magumu kuya Diagnose na kuyatibu ni Magonjwa ya Ngozi. Ndio maana unaona kuna Hadi madaktari bingwa wa Ngozi...
Unaongea siasa. Kuna kata hazina hata kituo cha afya zaidi ya majengo tu. Kituo cha afya au hospitali unaipata km 100+ toka hapo katani.
 
Pole sana kijana, kutibu vimelea vya fangasi inahitaji uwekezaji ( dawa stahili za muda mrefu mfululizo pasipo kuacha) kwa sababu hao fangasi wanachukua muda mrefu kuwadhibiti kutegemeana na aina ya dawa, hali ya kinga ya mwili pamoja na mazingira yako ( usafi wa mwili, nguo n.k pamoja na hali ya asili ya ngozi yako kama unyevu au ukavu ukijumuisha aina za mafuta au lotion unazotumia).
 
Binafsi nimekata tamaa na hilo tatzo nimetumia kila tiba Hakuna nimeenda mapka agakhan nikukutana na professor wa magonjwa ngozi lakn hakuna nafuu ni zaid ya miaka 15 sasa na hilo tatzo now nimeamua ishi nalo tuu
Mkuu fangasi sugu Ina pona tuwasiliane Kama hutojali.njoo pm tujadiliane tuulizane kidogo na Kisha tupeane tiba.Naamini HAKUNA UGONJWA USIO NA DAWA.
Karibu
 
Habari za majukumu wapendwa wana JF,

Mimi nasumbuliwa na fangasi (kama utangotango/mba) katikati ya mapaja, kulikopelekea sehemu hiyo kuwa nyeusi sana...
Pole Mkuu utapona.
Ushauri :
Ukianza tiba hakikisha nguo ZAKO zote zinafuliwa kwa maji ya Moto,na sabuni , Zisuuzwe vema kuhakiki a povu na vumbi la sabuni havipo,zianikwe juani,zipigwe pasi Happ waweza pona fangasi.
ANGALIZO;
HAKIKISHA NGUO ZINA SUUZWA VEMA KUONDOA VUMBI LA SABUNI.!
 
Nitumie jina lako Inbox then nitakuombea
Itaisha kabisa .. Ukiona umepona uende kanisa lolote Yesu anahubiriwa ukatoe Shukrani. Asante.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom