Mimi nasema Katiba Mpya kwanza, Tume Huru ya Uchaguzi itajileta automatically

Matendo Andrew

JF-Expert Member
Apr 1, 2014
748
365
Watanzania wenzangu unajua kunamambo huwa hayahitaji kutumia nguvu wala akili nyiiingi sana.

Hebu tujifunze kua uweredi wa mafundi kinyozi huyu jamaa halipwi kulinganga na mashine yake kukaa sana kichwani kwa mteja bali kunyoa haraka na vizuri ndio kunampa umahiri wa kazi yake.

Tofauti na mafundi radio au gari, unaweza kumpa radio akajizungusha siku nzima halafu akakwambia imekufa AC kumbe alikua kabisa radio nzima ila cable ya umeme ndio mbovu.

Nimetoa mfano kwasababu ya level yangu ya elimu ambayo najivunia sana kuwa nayo ni Std 7.

Sasa suala la Tume Huru ya Uchaguzi na mambo mengine yote yanayotuvuruga na kujaribu kutuingiza kwenye malumbano na machafuko shida ipo kwenye (katiba tu) kwahiyo watu kama ACT kushiriki uchaguzi Mbagala Kuu na sehemu nyingine wakati kikijua kwamba wao nimoja kati ya vyama pendwa vya kisiasa ni sawa na kuikalisha mashine mda mrefu kichwani wakati utalipwa hela ileile.

Au hawakujua kwamba kushiriki kwao kunawapa uhalali CCM kujiona wapo juu? Haya sasa mmeshindwa vibaya; imesaidia nini wenzenu walishajiridhisha kwamba hakuna njia nyingine bali ni Tume Huru ya Uchaguzi ambayo shina lake ni Katiba.

Hata mimi nasema katiba mpya kwanza. Tume huru itajileta automatically
 
Unataka Tume ya uchaguzi itakayoundwa na wazungu ndio utaamini?
Hapana mkuu tume huru itakayochaguliwa kihuru (wanaotaka kufanya kazi kwenye tume hii itabidi wapeleke maombi na kuhojiwa na kamati ya Bunge) na ni muhimu ikawa na watumishi wake kwa ngazi zote za kiuchaguzi) matokeo ya uchaguzi yanahesabiwa pale pale kituoni na kuwa wired straight kwenye kituo kikuu cha kukusanyia matokeo na kila mmoja wetu kupata matokeo haya straight sio kusubiri mteule mmoja mwenye njaa ya tumbo kutoa matokeo, au DEDs eti ndio watoa matokeo wakati hawa ni political appointee wa chama dola
 
Katiba ni jambo la msingi lakini halina umuhumu kwasasa, ni kama kupanga misiba kwa watu ambao vipimo vinasema wako fit.
 
Hapana mkuu tume huru itakayochaguliwa kihuru (wanaotaka kufanya kazi kwenye tume hii itabidi wapeleke maombi na kuhojiwa na kamati ya Bunge) na ni muhimu ikawa na watumishi wake kwa ngazi zote za kiuchaguzi) matokeo ya uchaguzi yanahesabiwa pale pale kituoni na kuwa wired straight kwenye kituo kikuu cha kukusanyia matokeo na kila mmoja wetu kupata matokeo haya straight sio kusubiri mteule mmoja mwenye njaa ya tumbo kutoa matokeo, au DEDs eti ndio watoa matokeo wakati hawa ni political appointee wa chama dola
Utasubiri sana kupata katiba mpya chini ya utawala wa CCM. Kushindwa kwa CCM ni matokeo ya katiba mbovu iliopo. Katiba mpya haitakuja kwa hiari, bali kwa mhanga wa wapigania haki wa kizazi kitakacho kuwa kimechoshwa na hila za CCM. Kwa sasa hali hiyo inaandaliwa na CCM yenyewe, kwani imevimbewa mezani na sasa imeanza kumshika kipofu mkono.
 
Nashauri mchakato wa katiba mpya uanze January 2026 (umalizike October 2028), lakini tume ya katiba mpya iundwe January 2022.

Tume huru ya uchaguzi ipatikane October 2023 (miaka miwili kabla ya uchaguzi mkuu wa October 2025).

Vyama vya siasa viruhusiwe kufanya mikutano ya hadhara ya kisiasa from January 2022.

Mada kuu ya katiba mpya iwe:

Katiba mpya iwe na a Bill of rights, itakayoheshimu basic human rights.

Muhimili wa Mahakama uwe huru.

Muhimili wa Bunge uwe huru.

Rais wa JMT asiwe na uwezo wa kulivunja Bunge la JMT.

Ikitokea kuna mvutano wowote ule usiotatulika baina ya Rais na Bunge, a national referendum ita amua nani kati yao aachie madaraka, na hakutakuwa na uchaguzi mpaka kipindi kijacho cha uchaguzi mkuu. Kama Bunge litashindwa referendum, nchi itakuwa haina Bunge mpaka uchaguzi mkuu ujao. Kama Rais atashindwa referendum, Bunge litamchagua kaimu Rais atakae kaa mpaka uchaguzi mkuu ujao. Kaimu Rais huyo anaweza awe au asiwe Makamu wa Rais wa huyo Rais ambae ameshindwa referendum.

Principle hiyo hiyo ita apply kwa Rais wa SMZ na Baraza la wawakilishi.

Wananchi wa pande zote za Muungano watapiga referendum kama upande wao unataka Muungano au la. Na kama wanautaka Muungano, wanataka Muungano wa serikali ngapi, moja, mbili au tatu.

Wananchi wa upande husika wa Muungano, watapiga referendum kama wanataka serikali centralised (kama sasa) au serikali za mikoa (zinazoiga zile za counties za Kenya, ila kwa Tanzania zitakuwa kwa level ya mikoa na sio kwa level ya counties/districts) au serikali za majimbo kama kule Nigeria. Mimi nadhani, kwa Tanzania serikali itakayo faa ni serikali za mikoa, zinazoiga zile za counties za Kenya. Serikali za majimbo kama za Nigeria hazitafaa.

Je, Bunge la JMT litakuwa na two houses (house of representatives na Senate) au litakuwa na house moja (kama sasa hivi)?

Since uhuru wa Bunge utaongezeka, basi qualifications za wagombea ubunge zifanane kabisa na qualifications za wagombea urais. Isipokuwa tu, umri wa mgombea ubunge uwe miaka 21 au zaidi.

Since muhimili wa mahakama utakuwa huru, basi qualifications za mahakimu na majaji ziwe zina fanana kabisa na qualifications za wagombea urais isipokuwa tu, umri wa mahakimu na majaji uwe miaka 21 na kuendelea, na wawe na degree ya sheria (au degree ya somo lenye uhusiano na mambo ya sheria).

Tume hiyo mpya ya katiba inaweza ichukue au isichukue mapendekezo ya rasimu ya katiba ya tume ya Warioba.

Mwenyekiti wa tume mpya ya katiba anaweza kuwa Jaji Mary Longway.
 
Hapana mkuu tume huru itakayochaguliwa kihuru (wanaotaka kufanya kazi kwenye tume hii itabidi wapeleke maombi na kuhojiwa na kamati ya Bunge) na ni muhimu ikawa na watumishi wake kwa ngazi zote za kiuchaguzi) matokeo ya uchaguzi yanahesabiwa pale pale kituoni na kuwa wired straight kwenye kituo kikuu cha kukusanyia matokeo na kila mmoja wetu kupata matokeo haya straight sio kusubiri mteule mmoja mwenye njaa ya tumbo kutoa matokeo, au DEDs eti ndio watoa matokeo wakati hawa ni political appointee wa chama dola
Mkuu, tatizo kuna watu wengi hata humu jamvini ambao hawaelewi kabisa nini maana ya Tume huru ya uchaguzi. Kwa hiyo utapsta shida sana kuwaelezea...!!
 
Back
Top Bottom