Mimi mdogo wenu / mtoto wenu nahitaji ushauri wa kisheria kwenye hili

Ivan Martin

Senior Member
Jun 13, 2020
155
500
Habari zenu wakubwa! Mimi ni kijana wenu nipo chuo bado nasoma ndio kwanza nipo mwaka wa pili hapa Jijini Dar es salaam. Kama kichwa cha habari kinavyosema kuhusu kuomba ushauri wa kisheria kwenye suala lililojitokeza siku ya tareh 27 December ya mwaka 2021. Siku ilikuwa ni jioni ya Jumatatu nilienda stend ya mbezi luis kwaajili ya kusafirisha mzigo wangu ambao ulitakiwa uondoke kesho yake ambayo ilikuwa ni Jumanne, na mzigo ule ulikuwa unaenda Tabora na kwa bahati nzuri siku hiyo siku hangaika sana nilikata tiketi ya mzigo na mzigo nikakabidhi ndani ya bahasha ikaandikwa na jina la mpokeaji pamoja na namba zake za simu. ( Katika ule mzigo ndani yake nilisafirisha lain mbili za simu )


Kesho yake siku ya jumanne ambayo niliamini kuwa Bus limeanza safari kuelekea Tabora na nikitegemea kuwa kufikia majira ya jioni au usiku wa Saa2 Bus itakuwa imeshafika na siku itayofuata ya Jumatano ndio mpokeaji aweze kwenda kupokea mzigo, bahati mbaya hiyo siku ya Jumatano mpokeaji alivyokwenda kupokea mzigo katika ofisi za hiyo Bus akaambiwa kuwa mzigo ule hauonekani... Hiyo siku sikutaka kuwapigia simu hao vijana walionikatia tiketi nikijiaminisha kuwa huenda Bus ilipata matatizo ikashindwa kusafiri.

Siku zikaenda mpaka mpaka siku ya Jumapili, na katikati ya siku kuanzia Alhamisi hadi Jumapili nilikuwa nikiwapigia simu ofisi hapo nilipokatia tiketi, muda mwingine namba zao hazipatikani na muda mwingine zinatumika tu na kule pia mpokeaji alikuwa akienda kila siku kufatilia mzigo akifika anaambiwa Bus imefika lakini mzigo huo haupo... Basi bhana nakumbuka siku hiyo ya Jumapili nikiwa mtaani napoishi kigamboni niliwapigia tena kule kwenye ofisi ya Bus nilipokata tiketi kuwaulizia wamefikia wapi kuhusu mzigo wangu, hiyo siku nakumbuka niliwapigia karibu siku nzima wakawa hawapokei na ilipofika jioni alipokea kijana mmoja nikamuelezea shida yangu alipogundua ni issue ya laini akanikatia simu na kuniblock muda ule ule na kesho yake nilikuwa nna mitihani chuoni... Ki ukweli nilichukia sana sikujali kuwa kesho yake nilikuwa na mitihani wala nini, nilichukua usafiri nikaenda mpaka stend kwenye ofisi zao haraka sana kufika pale kuwaelezea na kuwaambia issue yangu wakawa wananipotezea kama hakuna mtu aliekuwa ananijali basi nilikasirika sana nikamtafta mtu aliyenikatia tiketi na kunipa namba zake kumuuliza ananisaidiaje nae pia alinizungusha tu kwa maneno... Niliondoka usiku ule kurudi kigamboni bila kupata majibu yakueleweka kutoka kwao... Jumatatu yake nikaamkia kwenye mtihani ( na kumbuka hapo ishakuwa week sasa mzigo haujulikani ulipo ). Nilivyotoka kwenye mtihani hiyo siku niliamua kwenda mpaka kwenye ofisi zao tena mbezi kuwaambia nmechoka kuzungushwa nataka waniambie kama zimepotea au laah lakini hiyo siku nilivyofika nikakuta wale walionikatia tiketi hawapo, nilikasirika sana nikakosa cha kufanya nikahisi labda kwa sababu ya upole wangu ndio maana wananifanyia vile basi nilirudi nyumbani kubadilisha nguo na jioni ile ile nikarudi pale pale mbezi.

Nakumbuka nilivyorudi sikutaka kwenda tena kwao kwasababu nilikuwa nishapata hasira namimi najijua nikiwa na hasira sometimes ata kuongea nashindwa basi nikaenda kituo cha polisi kuwaelezea wakaelewa wakanipa RB nikaenda kituo cha posta pale jirani kuchukua polisi ili niende mpaka kwa aliyenikatia tiketi, nilifanikisha kumshikilia na tukaenda nae mpaka kituo cha polisi pale kwaajili ya mahojiano. Tuliongea pale mwisho wa siku huwezi amini zile laini zilikuwa zipo huku huku Dar wala hazikusafirishwa, yule kijana alikuwa nazo na akanionesha na kusingizia kuwa zilisahaulika na kuonekana juzi... Yule kijana aliambiwa anilipe gharama zote nilizoingia na laini zile zisafirishwe zifike Tabora haraka sana tena kwa Bus lingine. Alifanya vile kusafirisha kwa Bus lingine usiku ule ule na nikaondoka nikiamini nimemaliza kila kitu.

Kesho yake sikuulizia chochote kuhusu ule mzigo ila tu nilimwambia mpokeaji ajiandae siku yoyote aende kwenye ofisi za Bus hilo lingine kuupokea mzigo. Cha ajabu tena kule kuzungushwa kuliendelea vile vile kwa muda kama siku mbili iv wakidai kuwa mzigo wa namna hiyo haujasafirishwa na tuweze kuongea na konda aliekata tiketi. Ki ukweli nilichoka kabisa kufanya vile na ukiangalia ni week sasa inaelekea ya pili mzigo haufiki tu Tabora.

Nilipotezea mpaka leo hii ule mzigo na mpokeaji nilimwambia aachane nao tu kama wameamua kufanya ivyo ni sawa tu leo kwetu kesho kwake maana hii ni dunia inazunguka Karma ipo. Lakini wakubwa zangu hicho kitu hadi leo hii nikifikiria bado naumia tu kwanini nilifanyiwa vile sielewi ni kwanini tu sina cha kufanya zaidi ya kukasirika na kujitahidi kusahau

Mkawe na jioni njema !
 

Ivan Martin

Senior Member
Jun 13, 2020
155
500
Nasindikiza na picha hizi View attachment 2081168
IMG_20220114_183338.jpg
 

Jasmoni Tegga

JF-Expert Member
Oct 28, 2020
5,718
2,000
Nilitegemea ungeonesha usomi wako kwa kusolve promptly problem kama hiyo; you seem to give up so easily. Sasa elimu yako itakusaidia kweli huko uendako? Hivi haitakuwa mwendo wa kuonewa tu maishani mwako? Nasema hivi, wakusanye hao ^war-who-knee^ wote ofisini wapeleke Oysterbay PS. This is completely unacceptable!
 

Ivan Martin

Senior Member
Jun 13, 2020
155
500
Nilitegemea ungeonesha usomi wako kwa kusolve promptly problem kama hiyo; you seem to give up so easily. Sasa elimu yako itakusaidia kweli huko uendako? Hivi haitakuwa mwendo wa kuonewa tu maishani mwako? Nasema hivi, wakusanye hao ^war-who-knee^ wote ofisini wapeleke Oysterbay PS. This is completely unacceptable!
Oysterbay! Sijui ofisi yoyote ambayo inapatikana huko itayoweza kunisaidia. Kwa hapa Dar mimi ni mwenyeji kiasi si sana.
 

Kambaku

JF-Expert Member
Nov 12, 2011
4,344
2,000
Dogo pambana wakupe line zako. Wasije wakazifanyia mawasiliano meusi ukakamatwa kuungwa kwenye tukio la ujambazi au mauaji.

Sioni sababu kwanini wakatae kusafirisha line tu. Kwani zina nini na umeshawalipa
 

Vishu Mtata

JF-Expert Member
Dec 15, 2019
2,226
2,000
Kama zina umuhimu usipotezee dogo, rudi polisi tena mdake jamaa. Ila safari hii usimwachie laini zako bora uzichukue utajua wewe jinsi ya kuzipeleka tena.

Hapo huenda jamaa kaamua tu kukufanyia mbaya kisa umempeleka polisi, ko na yeye anakuonesha umwamba.
 

Jasmoni Tegga

JF-Expert Member
Oct 28, 2020
5,718
2,000
Kama zina umuhimu usipotezee dogo, rudi polisi tena mdake jamaa. Ila safari hii usimwachie laini zako bora uzichukue utajua wewe jinsi ya kuzipeleka tena.

Hapo huenda jamaa kaamua tu kukufanyia mbaya kisa umempeleka polisi, ko na yeye anakuonesha umwamba.
nikahisi labda kwa sababu ya upole wangu ndio maana wananifanyia vile
SASA NAELEWA KWA NINI JPM ALIMSHAURI PROFESA MBARAWA AVUTE BANGE.
 

Ivan Martin

Senior Member
Jun 13, 2020
155
500
Nenda oysterbay tafuta ofisa mmoja ongea naye afu kawakamate uwapeleke.
Nina mpango huo nikishamaliza ubusy wa mitihani na kutafuta course work chuoni, nitaenda kituo kikubwa kuripoti nipate usaidizi lakini kwa sasa nataka nifanye kama nimepotezea ili mtu yule ajisahau kabisa
 

Ivan Martin

Senior Member
Jun 13, 2020
155
500
Nenda oysterbay tafuta ofisa mmoja ongea naye afu kawakamate uwapeleke.
Alafu kingine nilichogundua ni kuwa ukienda kituoni na RB kwaajili ya kuchukua Askari wa kukusaidia, Askari tena hutaka kulipwa pesa ya ukamataji , na hiyo kumtoa Oysterbay naona kabisa atahitaji nimpatie pesa
 

Ivan Martin

Senior Member
Jun 13, 2020
155
500
SASA NAELEWA KWA NINI JPM ALIMSHAURI PROFESA MBARAWA AVUTE BANGE.
Nashukuru Mungu upole wangu wakati mwingine hunisaidia... Na kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyo maisha yananibadilisha, mpaka nije nimalize chuo basi sitaonewa tena bila hata ya kutumia hizo Bangi
 

Chupayamaji

JF-Expert Member
Sep 19, 2017
4,282
2,000
Alafu kingine nilichogundua ni kuwa ukienda kituoni na RB kwaajili ya kuchukua Askari wa kukusaidia, Askari tena hutaka kulipwa pesa ya ukamataji , na hiyo kumtoa Oysterbay naona kabisa atahitaji nimpatie pesa
Utalipwa gharama zako zote za usumbufuna huyo mtuhumiwa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom