Mimi Lunyungu Matandula nimeshangaa na nauliza sasa ni kwa nini wageni ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mimi Lunyungu Matandula nimeshangaa na nauliza sasa ni kwa nini wageni ?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lunyungu, Dec 26, 2008.

 1. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #1
  Dec 26, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Nimeingia hapa uwanja wa ndege wa JKN naelekeo Moscow kwa kazi yangu lakini maalumu , nikaamua kutembelea maduka haya ya duty free .Nimeshangaa kila mhindi namgusa ni msemaji ama wa kihindi na kiingereza .Kuna kadada humo ndani nakuuliza kulikoni hapa na vipi usalama wa uwanja wetu na pia vipi Visa zao ? Anasema hawa wana siku chache tangia watoke India na Pakistani na wanaingia kinyemela na asubuhi wanaibukia hapa ndani kuuza kwenye duty free shops.

  Jamani nauliza tena kwa sauti mnisaidie vipi Usalama wa Nchi ? Usalama wa uwanja ? Vipi hakuna Wadanganyika wanaweza kuuza maduka yale ? Nime enda kwenye coffee shop pale nimekuta maajabu jamaa wanasema kuna uchafu zaidi na wanaomba nirudi wakati mwingine nipate nyeti.Kwa sasa nawasilisha mniombee nangoja kuchukua mchuma punde tu .
   
 2. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #2
  Dec 26, 2008
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Kwani hayo maduka ni ya nani?
   
 3. M

  Masatu JF-Expert Member

  #3
  Dec 26, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Bon voyage mkuu,

  Ushauri wangu kwako na wewe fungua duka lako ajiri wabantu ndio mambo ya soko huria hayo. Hata huko Moscow uendako usishangae kukuta dereva wako wa Taxi ni Mpaki!
   
 4. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #4
  Dec 26, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Lunyungu Lunyungu Lunyungu, hujui kuwa Tanzania ukiwa mgeni ni deal. Mzungu, mhindi na wengine wasio na ngozi nyeusi wanaheshimiwa sana Tanzania. Sijui wewe ni nani hasa na kama uliheshimiwa ulipokuwa unapita kwenye geti la kwanza. Kuna maswali ya kijinga kweli wanauliza kama ulisema una kwenda Moscow inawezekana walikuuliza unakwenda kufanya nini, utalala wapi, nani anakulipia na ujinga kama huo. Lakini akipita mzungu anaambiwa "have a nice flight"
   
 5. J

  JokaKuu Platinum Member

  #5
  Dec 26, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,790
  Likes Received: 5,051
  Trophy Points: 280
  ..there is something special about Wahindi.

  ..Wahindi wana-dominate hata NASA,IBM,na Oracle, kwa Wamarekani.

  ..halafu kwanini tunahoji hapo Uwanja wa ndege tu. hata maeneo ya kisutu na kariakoo matajiri wa Kihindi wanaajiri watu wa kwao tu.
   
 6. share

  share JF-Expert Member

  #6
  Dec 26, 2008
  Joined: Nov 22, 2008
  Messages: 2,294
  Likes Received: 2,278
  Trophy Points: 280
  Lunyungu kwa kufunga kamba bwana!, eti anakwea pipa kwenda Moscow! Safari njema mkuu hata kama unaenda Moscow mwembe madafu. Ujumbe umefika. Asante sana mkuu. Wahindi wapo kwenye shamba la bibi. Kwani hujui hilo! Hawajaanza leo hao, kila kukicha wanaingia na mfuko wa rambo, baada ya muda wanamiliki Fuso za mchanga na viduka vya ama nguo au madawa. Hawapewi siku 7 hao kupeleka vielelezo vya uhalali wao kuwepo nchini maana siyo tishio kwa usalama wa taifa! Ila Mengi akisema anatendewa mchezo mchafu anapewa siku 7, eti ni hatari kwa usalama wa taifa! Safari bado ndefu nchi ya wadanganyika.
   
 7. K

  Kimbembe Senior Member

  #7
  Dec 26, 2008
  Joined: May 14, 2006
  Messages: 122
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu ungaliweza kuchangia bila kijembe ambacho tuna uhakika huwezi kukitetea juu ya safari ya jamaa.Lakini kubwa ni kwamba pamoja na wahindi kujazana na hawapewi siku 7 Lunyungu hata mimi nashitushwa na jambo la Usalama wa Nchi airport yetu japokuwa wengi hawana permits na inasemekana maduka yale ni ya mafisadi in conjuction na wahindi .Ushahidi ni mawaziri wa JK , MKapa na wengineo hapo muda ukifika tutayataja majina hapa .
   
 8. Majita

  Majita JF-Expert Member

  #8
  Dec 26, 2008
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 606
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Mimi hapo tu,yaani sina mbavu.Kumbe kuna Moscow ya huko na unaenda kwa pipa!!
   
 9. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #9
  Dec 27, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Lunyungu bwana! Hivi kama unaenda Nairobi si bado unaweza kuona hao Wahindi na maduka yao?
   
 10. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #10
  Dec 27, 2008
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Too many Indians in Tanzania,hata kama kwa kusema hivyo ntaitwa m-baguzi.
   
 11. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #11
  Dec 27, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Ninakubaliana na concerns za mzee Lunyungu kuwa sheria zetu za uhamiaji zinazotawala utoaji wa ajira kwa raia wa nje hazifuatwi kabisa. Niliwahi kuuliza swali hili la kuhusu sheria zetu za ajira huko nyuma, lakini nadhani halikupata majibu

  Hapana, soko huria halina maana kuwa uajiri mtu yeyote umpendaye kufanya kazi kaika biashara zako hata kama kufanya hivyo ni kinyume cha sheria. Tuna sheria za uhamiaji ambazo pamoja na mambo mengine zinahitaji mtu ambaye siyo raia wa Tanzania kupata kibali cha kufanya kazi nchini (work permit) kabla hajaajiriwa.

  Hapana, wahindi walioko NASA, IBM, Oracle huko Marekani ama wameshakuwa raia wa Marekani au wana green cards zinazowaruhusu kuishi na kufanya kazi marekani. Ina maana kuwa ajira zao zimefuata sheria zote za uhamiaji. Tatizo hapa ni watu kutoka India au pakstani na kufanya kazi bila kufuata sheria za nchi.
   
 12. J

  JokaKuu Platinum Member

  #12
  Dec 27, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,790
  Likes Received: 5,051
  Trophy Points: 280
  Kichuguu,

  ..hata Tanzania kukiwa na kazi zinazolipa kama hizo za NASA,IBM,..watapatikana wahindi wa kuja kutufunga magoli.

  ..kuna kitu hawa wenzetu wametuzidi ujanja na ni lazima tukitafute ili tuweze kushindana nao. kwa mfano, kwanini hakuna waswahili wenye maduka ya duty free hapo Julius Nyerere DIA?

  ..tunaweza kuziba mwanya huo wa duty free stores lakini wakaibukia ktk sekta nyingine mfano ukandarasi wa ujenzi, government suppliers, etc etc.
   
 13. Opaque

  Opaque JF-Expert Member

  #13
  Dec 27, 2008
  Joined: Oct 24, 2008
  Messages: 1,138
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Asingeweka Moscow ungejuaje kama kaenda Urusi?
   
 14. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #14
  Dec 27, 2008
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Naam, baada ya kimya kirefu narudi hapa jamvini nakutana na karaha yangu ya kila siku. Kila kona hawa ndugu zangu sasa wamejaa. Katika pitapita yangu kwenye shughuli za kikazi, hoteli nyingi huku kaskazini mwa Tanzania zina hata wapishi wa kihindi. Jamani hakuna wapishi Tanzania hadi watoke India? Hawa vijana wetu waliosomea pale chuo cha forodhani hawawezi kweli kupika. Nilimdodosa meneja mmoja akasema yeye kaagizwa tu na bosi wake amwajiri. Nikauliza na mshahara wake ni kiasi gani,,,, hapo ndipo nilipochoka,,,,, wanalipwa kati ya dola 800 mpaka 1000 na nyumba ya kukaa bure na marupurupu kibao, Wakati hawa waswahili wanalipwa elfu 80,000 hadi 120,000 kwa mwezi bila kupewa nyumba ya kulala na marupurupu mengine.Je huku tunajenga nchi ama,,, hizi ajira tunazosema kwa watanzania zitakuwepo kama tunaendelea kuwakumbatia wageni? Idara ya Uhamiaji haioni ama inafunga macho tu?
   
 15. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #15
  Dec 27, 2008
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kwa taifa linaloendelea kama Tanzania bila kuwa na SERA makini za kulinda Raia tutafikia mpaka mayaya watakuwa hawa watu wa kutoka Asia. Tatizo la Tanzania ni sehemu ya kuchumia, yani hatuko makini kabisa, yote hii ni kuwa RUSHWA imekuwa kiasi kikubwa mno. Mtu yuko radhi abinafsishe uwanja wa Ndege wa KIA kwa Dola 5000, sababu tu mwanae atasomeshwa ulaya naye kupata fungu hapo. Lakini haangalii hasara kuwa hata wajukuu zake watakuja kuzipata. Wakati wenzetu wanaangalia hatua 100 mbele, sisi tunaangalia hatua mbili tena tumefunga macho.

  Suala la wahindi lipo, sasa kunakuja suala la Wachina, wanafanya biashara za Machinga, ina maana hata hizo hatuna Sera ya kuwawekea masharti magumu ama kuwazuia, biashara zilizokuwa zifanywe na Machinga wetu sasa hata Wachina wanachukua. Lakini yote hii ni kutokuwa na watu makini. Suala si wahindi tu au wachina, hata watu toka sehemu nyingine (Ulaya, Amerika, Australia nk) wakija tunawapokea kama wameshuka Malaika. Angalieni nchi kama Kenya na Uganda, majirani zetu, wako makini hawataki upuuzi upuuzi. Ukitaka kata mikoko unakuja TZ eti unaanzisha mradi wa Kamba, mbona hawaendi Mombasa. Ukitaka fanya utafiti Ziwa Victoria unapitia TZ, manake hatuweki mikakati hizi tafiti zije zitusaidie (japo hata watu wetu wasomeshwe ili tuje angalau tujitegemee). Ni kwamba waganda na wakenya huwezi fanya mambo kiujanja ujanja. Sasa usiseme warwanda, hawa wanakuja juu mno.

  Hivyo sasa tunasema wahindi, lakini wachina nao hao, nakumbuka miaka mitatu iliyopita ukienda pale King Palace Hotel (sijui jina ni Palace Hotel manake inanichanganya na ile King Palace Hotel ya Sinza, Dar na ile ya Mwanza) iliyo mkabala na Concord Hotel utawakuta Wachina kibao wamemaliza shughuli zao wanacheza pool. Nchi tunatakiwa tuifumue kila sehemu na tuweke MIFUMO MIPYA.
   
 16. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #16
  Dec 27, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hiyo ndiyo Tanzania zaidi ya uijuavyo. Tumeanzisha mfumo wa soko huria, wajuaji wameutafsiri wanavyotaka wao. Leo hii hata ukikutana na Kikwete ukamueleza kuwa kuna expatriates ambao wanafanya kazi ambazo zinaweza kufanywa na wenyeji kama upishi, atawatetea tu. nakumbuka wakati fulani (akiwa rais) aliwahi kuulizwa kuhusu hilo akasema kuwa kuna aina nyingine ya vyakula watanzania hawawezi kuvipika, ndio maana wenye mahoteli wanalazimika kuagiza wapishi kutoka nje. Lakini sijui ni kwa nini hao walipwe zaidi ya wazalendo????
   
 17. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #17
  Dec 27, 2008
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,402
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 180
  Eka Mangi,
  Mpishi ni profession Muhimu sana; huwezi kusema tu hata "Wapishi", labda ungetuambia huyo mpishi anapika chakula cha aina gani. Kama huyo mpishi anapiga chakula cha Kitanzania nitakuelewa. Kama sikosei ni kuwa kuna post kama zile za uuzaji wa dukani, au attendants hawa ni budi waajiriwe wazalendo kwa sababu si kazi za ujuzi ukosekanao nchini.

  Kuhusu Mshahara; hayo ni makubaliano yako na mtaalamu unayemwajiri. Huyo investor si mjinga amwajiri mpishi kwa mshhara wa dollar 800 - 1000 kama anajua angempata mpishi anayeweza kupika kwa Sh 80,000; i doubt on some opinion contributors as are lacking knowledge or experience!
   
 18. Nyangumi

  Nyangumi JF-Expert Member

  #18
  Dec 27, 2008
  Joined: Jan 4, 2007
  Messages: 508
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Matatizo kama haya hayawezi kwisha mpaka pale tutakapobadili namna ya kupata viongozi wetu. Tunapochagua watu kwa kuwa wamewekeza kwetu pesa, au pilau,kofia au hata vilevi, lazima tutegemee nao waende kujizalishia. Ofisi wanazopewa imekuwa ni sehemu ya wao kupangia mikakati ya namna gani arudishe pesa alitumia kwenye uchaguzi na namna gani atapata pesa kwa ajili ya uchaguzi ujao. Tuwe na bunge linalowajibika sio hili bunge butu la chama kimoja.
  Kwa kweli sioni mwanga wa mambo kubadilika huko mbeleni, mpaka hapo CCM watakapoondolewa. Mengi ya mambo ambayo yanahitaji kurekebishwa hayahitaji fedha kuyatatua bali maamuzi na sera tu.

   
 19. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #19
  Dec 27, 2008
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Eeka Mangi,
  Mbaya zaidi, mshahara unaokuwa declared TRA kwa kodi unakuwa chini ya asilimia 20 ya mshahara halisi. Kuna hujuma kubwa Uhamiaji kwenye utoaji wa vibali vya kazi kwa wageni. Kuna mhindi nayemfahamu anaye renew permit yake kila mara kama mtaalamu wa kompyuta wakati hata kazini kwake hatumii hiyo kompyuta.
   
 20. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #20
  Dec 27, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Mbona hapo Uhamiaji ndio dili lao kubwa katika ku renew hizo permit, na ukifuatilia kwa undani zaidi ni aibu tupu na fedheha kwa waTZ
   
Loading...