Mimi huwa nashindwa kumtazama mtu ninayeongea naye ana kwa ana usoni kwake, sababu inaweza kuwa ni nini?

Maulaga59

JF-Expert Member
Feb 1, 2021
2,989
2,954
Haya! Mwenzenu nina tatizo la kutotazamana na mtu ninayeongea naye uso kwa uso, hata angekuwa tofauti ya jinsia yangu.

Huwa tukiongea na mtu, au natazama pembeni au nakuwa kama nainama ili mradi tu tusigongane macho yetu. Lakini akitazama yeye pembeni ndiyo huwa namuangalia usoni na machoni.

Je, hii imewahi kuwatokea baadhi yenu? Sababu yake ni nini, maana kuna watu ukiwaona wanaongea wanatazamana usini muda wote wa maongezi yao, lakini siyo mimi.

Nawasilisha hoja.
 
Haya! Mwenzenu nina tatizo la kutotazamana na mtu ninayeongea naye uso kwa uso, hata angekuwa tofauti ya jinsia yangu. Huwa tukiongea na mtu, au natazama pembeni au nakuwa kama nainama ili mradi tu tusigongane macho yetu. Lakini akitazama yeye pembeni ndiyo huwa namuangalia usoni na machoni. Je, hii imewahi kuwatokea baadhi yenu? Sababu yake ni nini, maana kuna watu ukiwaona wanaongea wanatazamana usini muda wote wa maongezi yao, lakini siyo mimi.
Nawasilisha hoja.

Usije kuwa wewe ni Cyprian Musiba
 
Huna ujasiri kabisa ww au ni muoga sana, ili kutoa tatizo hilo, vuta bangi mara 3 kwa wiki na fanya hivyo mwezi 1 hiyo hali itaisha kabisa.

Au, tumia supu iliwekwa miti ya Ngiloriti inapatikana Arusha, hiyo hali itaisha kabisa, utamwangalia mtu usoni hadi atataka kukimbia ukiwa unaongea nae

Huu sio utani nasisitiza.
 
Kuna kutazama na kukazia macho, mojawapo inaweza kuwa sign ya intimidation au sexual harassment......ni kama pisi kali unaikazia macho kuonyesha kwamba umeikubali.
 
Ninasikitika kwamba uzi huu sitakua na cha kuchangia zaidi ya kupitia comments
 
Huna ujasiri kabisa ww au ni muoga sana, ili kutoa tatizo hilo, vuta bangi mara 3 kwa wiki na fanya hivyo mwezi 1 hiyo hali itaisha kabisa.

Au, tumia supu iliwekwa miti ya Ngiloriti inapatikana Arusha, hiyo hali itaisha kabisa, utamwangalia mtu usoni hadi atataka kukimbia ukiwa unaongea nae

Huu sio utani nasisitiza.
Ova..
 
Mimi binafsi ndugu zangu Esp; Kaka zangu siwatazamagi usoni kwa kuwazingatia.

Mpenzi wangu ndio mtu naongoza kumtazama usoni tena machoni kabisa.

Na mtu anaenipa mchongo/ au anaenieleza matatizo yake / au majadiliano yotote yenye mantiki au Hoja lazima nimtazame mtu machoni.

Hii ni kwasababu naamini macho yanaongea kilichopo moyoni, sio lazima mtu aongee nikimtazama tu machoni najua which is which
 
Umri tuu ukifika 35 hadi 40 huko utawatizama mpk waombe pazia kati yenu
 
eye_contact.jpg

Nnakusaidia uwe unaangalia kati kati ya PUA

20220331_211717.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom