Mimi Deogratius . N. Kisandu nimechoka kupotoshewa kila jambo, sasa naweka wazi

BIMA YANGU YA AFYA BADO INABAINISHA UMRI WANGU WA KUZALIWA JAPO JINA LA MWANZO LIMEPOTOSHWA SPELLINGI.

Katika Bima hii nilipotoshewa pia badala ya kuandika "DEOGRATIUS" ikaandikwa "DEOGRASIAS". Ikumbukwe Bima hii nilichukuliwa na mama yangu mzazi mwaka 2002 nikiwa Form 4. Siku njema. TUKUTANE 2020 TUKAJENGE TAIFA JIPYA. rejea ID hapo chini.
18836019_1560407647356595_3404159499180532695_n.jpg


KANISA KATOLIKI LINIOMBE MSAMAHA.

Hiki nikitambulisho changu cha ubatizo kilitolewa mwaka 1992 baada ya kubatizwa kipindi nasoma shule ya msingi Sunge(Itugunhu) kabla sijahamia shule ya msingi Kahama Imeandikwa nimezaliwa mwaka 80 badala ya mwaka 1980, pia imeandikwa nimebatizwa mwaka 92 badala ya mwaka 1992. NALIMI ni jina la Uji la baba yangu na ALEXANDER ni jina la Ubatizo la baba yangu. Siku njema
18835923_1567532333310793_5156240254380116157_n.jpg


HOSPITALI YA WILAYA YA KAHAMA NITAIFIKISHA MAHAKAMANI KWA KUPOTOSHA CHETI CHANGU CHA KLINIKI MWAKA 28. 6. 1980

1. Cheti hicho kimeandikwa Jina la Baba "NALIMI K, ISMAIL" badala ya "NALIMI ,I, KISANDU". Ikumbukwe jina langu la kuzaliwa ni "MASHAKA" na mwaka 1992 nilibatizwa kanisa katoliki kahama nakuwa "DEOGRATIUS". Hivyo ni MASHAKA NALIMI ISMAIL KISANDU na kuanzia mwaka 1992 ikawa DEOGRATIUS NALIMI ISMAIL KISANDU. Angalia cheti hapo chini.

2. Mimi sijazaliwa mwaka 80, bali nimezaliwa mwaka 1980.Na kama nimezaliwa mwaka 80 maana yake sasa nina miaka 1937. Hospitali inawajibika kunilipa fidia ya kunidhalilisha kwa kipindi hiki chote. Angalia cheti hicho hapo chini kabla sijabatizwa mwaka 1992. TUKUTANE 2020. TUJENGE TAIFA
18881874_1560370564026970_7092040271840342443_n.jpg


BODI YA MIKOPO ELIMU YA JUU IMENIDHALILISHIA UBINI WANGU.

Kitu cha kushangaza bodi ya mikopo hutumia majina yaliyopo kwenye cheti cha kidato cha nne ambapo mimi yameandikwa, DEOGRATIUS P. KISANDU, Cha ajabu ni kuwa Bodi wao wameongeza herufi "I", wakiandika "IKISANDU". Kwakuwa taifa limeamua kunidhalilisha lakini mimi nimekubali yote. Rejea barua ya bodi ya mikopo hapo chini, halafu wananikata 107,000/= kwasasa naitwa "DEOGRATIUS NALIMI KISANDU"
18767394_1560355040695189_9000108626760990309_n.jpg



CHUO CHA UANDISHI WA HABARI CHA ROYAL COLLEGE OF JOURNALISM (rcj)-DSM, KIMENIDHALILISHIA TRANSCRIPT YANGU NA KUSABABISHA KUFEDHEHEKA. NITAKIPELEKA MAHAKAMANI kwa Makosa MAWILI.

1. Nilihitimu Chuoni hapo mwaka MARCH 2003 na sio April 2002 kama ilivyooneshwa kwenye Transcript hii, kwani kwenye Cheti chenyewe kumeandikwa March 2003. Kwa Kozi ya BASIC CERTIFICATE IN JOURNALISM (ambayo kwasasa sawa na Diploma). Nimeambatanisha cheti cha Transcript. Hili ni kosa la kwanza.

2. Kosa la pili, wamesahau herufi "A" kwenye jina langu, wao wameandika "DEOGRTIUS" badala ya "DEOGRATIUS" hivyo wamenifedhehesha sana.Tizama transcript hapo chini.

3. Wamebadili na jina la chuo kutoka Royal College of Journalism na kuwa Tanzania College of Journalism kama sijakosea, chuo kipo Ubungo Urafiki-Dar es salaam.

DEOGRATIUS KISANDU
18671238_1553985491332144_7980971531432240202_n.jpg


MKUU WA CHUO CHA SEKUCo/SEKOMU-Lushoto,Tanga, Aneth Munga NITAMFIKISHA MAHAKAMANI KWA MAKOSA MAWILI YA KIUCHAPAJI KWENYE TRANSCRIPT YANGU YA MATOKEO, KWANI NIMEFEDHEHEKA SANA.

Mimi nimezaliwa 28/6/1980 na sio 28/6/1983 kama inavyosomeka kwenye Transcript na hata fomu zote hapo chuo nilijaza mwaka 1980 na sio mwaka 1983, na pia mimi nilijaza Sanduku la Posta Box 5 KAHAMA, na sio Box 77 Lushoto. Siku ya mahafari nilipopata vyeti na kuvisoma ndipo niligundua hilo tatizo nilipoomba kurekebishiwa niliambiwa haiwezekani. Hivyo kwasasa nafata utaratibu wa kisheria iliwanirekebishie kisheria, Sitaki maneno tena. Ikumbukwe pia nimeshakula kiapo kwa wakili kuwa situmii tena jina la KITAWA la "PIO" nimeweka ubini wa mzee wangu "NALIMI" na hivyo sio tena "DEOGRATIUS PIO KISANDU" bali ni "DEOGRATIUS NALIMI KISANDU"
18697966_1554005161330177_6465639310315381942_n.jpg



NECTA WALININYIMA DIPLOMA YA UALIMU (STASHAHADA YA ELIMU) MWAKA 2009.

Mimi Deogratius Pio Kisandu ambaye kwa sasa ni Deogratius Nalimi Kisandu badaa ya kuondoa PIO,Nikiwa ni Mtanzania wa Kwanza mwaka 2008 kuomba kufanya Mtihani wa Diploma ya Ualimu kama Mtahiniwa binafsi(Private candidate) kwa mwaka 2009, lakini nilikataliwa mpaka nijiunge na chuo, sikuona sababu ya kukataliwa kama Form 4 na 6 huwa tunafanya kama Private Candidate, Naomba NECTA mnipatie Diploma yangu sasa. Nilifanya hivyo ili kuitaka NECTA ibadili mfumo wake. Pitia barua hii niliyojibiwa na NECTA.



HALMASHAURI YA NZEGA ILINIPOTOSHEA JINA LANGU LA KATIKATI KWA MASLAHI YAO, BADALA YA PIO WAKAANDIKA PEOGRATIUS. IKIWEMO KUUGEUZA MHURI.
18664283_1552694228127937_6077147786004188712_n.jpg


HII NDIO SALARE SLIPU YA MSHAHARA WANGU na KOPI YA KITAMBULISHO CHANGU CHA KAZI.

Usalama wa Taifa wameichukulia mkopo salary slip yangu bila idhini yangu na mimi sijawahi kuchukua mkopo, nateseka na Deni lisilo langu tangu mwaka 2013 mpaka leo. Natayari pia Mwezi huu MEI 2017 Bodi ya mikopo Elimu ya Juu wamenikata 107,000/= na hivyo nimebakiwa na 170,000/= kwa mwezi. Nimetoa pia kopi ya kitambulisho cha kazi, maana Mwanza nzima wamenikana kuwa mimi sio Mtumishiwa umma hivyo natoa uthibitisho. Kumbuka pia nimesha kula kiapo kwa Wakili kuondoa jina la Utawani la "PIO" nakuweka jina la mzee wangu "NALIMI" lakini mpaka sasa sijarekebishiwa tangu mwaka jana. NADHALILIKA lakini navumilia, nasaidia Nchi lakini mshahara wangu ni waukapuku kabisa.

DEOGRATIUS KISANDU
18620174_1550474091683284_2490296367218889764_n.jpg


NIMENYIMWA KITAMBULISHO CHA TAIFA KISA WIVU.

Kama Mtumishi wa Umma nilijiandikisha na kutoa Data zote na kuweka dole gumba lakini wenzangu wote wamepewa kasoro mimi, yaani nafanyiwa hujuma kila jambo. Natoa FOMU niliyojaza ambapo niliambatanisha na Viapo na Cheti cha kuzaliwa kwa kuondoa jina la KITAWA la"PIO" nakuweka Jina la Mzee wangu "NALIMI". Sijishushi mpaka mtimize Haki yangu kisheria.

DEOGRATIUS KISANDU.

CC: Halmashauri ya Jiji la Mwanza
18698072_1550458015018225_3768541755395116216_n.jpg


HII ILIKUWA SALARY SLIP YANGU HALMASHAURI YA NZEGA KAMA MWALIMU WA INDUCTION YAANI LESENI KWA MKATABA WA MIAKA 5, KUANZIA 2007 MPAKA 2012.
18664439_1552694244794602_7633218406652997586_n.jpg


MKURUGENZI WA SEKONDARI YA ST.IRENE (SISTER IRENE)-KAHAMA NITAMFUNGULIA KESI YA KUDHALILISHA JINA LANGU LA UKOO.

Nilipoteuliwa kujiunga chuo cha ualimu Tabora kwa kozi ya INDUCTION Course May 2007, Bw. Chimaguli aliniandikia barua ya kunitakia masomo mema, badala ya kuandika "KISANDU" yeye akaandika "JISANDU" kinyume na nyaraka zangu zilivyoandikwa. Nimeambatanisha Barua hiyo ili muone udhaifu wa wakurugenzi wetu. Kwasasa situmii tena jina la KITAWA la "PIO" nimeshaweka ubini wa mzee wangu "NALIMI". Hivyo sio tena DEOGRATIUS PIO KISANDU bali ni DEOGRATIUS NALIMI KISANDU
18698375_1553957708001589_7721211219803921487_n.jpg


Star TV na Radio Free Africa WALININYIMA AJIRA MWAKA 2003 BAADA YA KUMALIZA CHUO CHA HABARI "RCJ".

Kuna mtu alitoa taarifa za uongo kwa Mh. Dialo na kusababisha mimi Deogratius Kisandu kukataliwa maombi yangu. Rejea barua hii ya Sahara Communication, kampuni inayomiliki Startv na RFA.

cc. Antony Dialo
18765896_1559096007487759_7197731748377696974_n.jpg


ENDAPO KANISA KATOLIKI LITANIFUNGULIA KESI YA KUTUMIA JINA LA PADRE PIO, BASI MASHIRIKA YOTE YA KITAWA YAFUNGWE.

Mashirika yote ya Kitawa ndani ya Kanisa katoliki yana ruhusu anayejiunga na Utawa kuchagua jina jipya la kitawa au kujichagulia jina jipya la kitawa au kutumia jina lako hilolilo kulingana na uhitaji wa mtawa husika. Mfumo huu umekuwepo kwa miaka mingi sana, iweje mimi Deogratius Kisandu nilipoamua kutumia jina la Padre Pio wa Pietrecina, Italia imekuwa nongwa na kuwekewa vizingiti vya ajabu ajabu ili hali niliwahi kuwa mtawa hapo zamani sana kwa padre ricardo Maria Morogoro mwaka 1998-1999. hata hivyo nilishaga kula KIAPO kwa Wakili muda mrefu tu na kuachana na jina hilo la Kitawa. Mkifungua kesi nina uhakika wa 100% kuwashinda. Pitia kiapo hapo chini.

DEOGRATIUS NALIMI KISANDU.
19059091_1577099809020712_2098083997154722024_n.jpg



WATUMISHI WOTE WA UMMA WAMEAMBIWA WANIKANE, MIMI NATOA UTHIBITISHO WANGU.
18622131_1546380355425991_7736159634823747936_n.jpg



Ndimi DEOGRATIUS NALIMI ISMAIL KISANDU.
Alhaji Deogratias Nalimi Ismail Kisanduku kaka hapo utashinda hizi kesi utajiri huo unakuja.
 
Andrew sijamuona siku nyingi hapa.

Jamaa wanakuja na habari so off the tangent inabidi ucheke tu.


Andrew tangu wakati wa bifu za wapwa zake kapotea, sijui alipigwa mkwara gani ukamtuliza. Hopeful hajarudishwa kwa ward.

Kipanga huyu mtu, dont know what went wrong.
 
Kisandu babaaaaa kamuaaaa heheee hee heeee nakuelewa sana jinsi unavyosepa na kijiji :D
 
Nisamehe mkuu,mwanzo nilikuwa nadhani ni mwezi mchanga...sasa naanza kuona si bure,lazima utakuwa ni mtu mwenye uwezo wa hali ya juu ndio maana umekuwa ukifanyiwa hujuma toka enzi hizo za ubatizo ili usipate nafasi ya kushine!...all in all Mungu yupo,ipo siku watu watakuelewa km nilivyokuelewa leo.
NB:Usisahau kunywa dawa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe ni wise comedian haswa!
 
Duuh mkuu. Kila chapio ni lako dah!!

sent from my iPhone 7s using JamiiForum mobile app.
 
Kisandu,
Kwa kiasi kikubwa umebainisha jinsi ambavyo Tanzania tumekosa umakini katika kuandika maneno na kunakili majina Kwa usahihi.

Na mlolongo wa shida ulizopitia Kwa vile watu hawakuwa makini ni mfano tosha tusifanye masuala muhimu kama kuandika na kunakili majina Kwa usahihi ktk hati, vyeti, vitambulisho n.k ni mambo ya rahisi.

Tukumbuke kuwa tunawapa matatizo watu siku wakihitaji kutumia hati na vyeti vyao kwa mambo muhimu ya kisheria, uhamiaji n.k
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom