Civilian Coin
JF-Expert Member
- Dec 2, 2012
- 2,305
- 4,379
Nimepewa taarifa na wanasiasa fulani na baadhi ya wadau wa maendeleo kuhusu umri wangu wa kuzaliwa.
Kimsingi mimi nimezaliwa mwaka 1980 na hata vyeti vyangu vyote vya kliniki na ubatizo vina umri huo, kuhusu mwaka 1983 ilifanyika Typing Error ofisi ya vizazi na vifo, na hata hivyo nilipeleka kwa ajili ya marekebisho na kupewa Cheti kipya baada ya kukana mbele ya wakili.
Ndio ni kweli kuna nyaraka zangu za kiutumishi na zingine zinaonesha nimezaliwa mwaka 1983 kutokana na kuwa wahusika walifuata birth certificate iliyokosewa kama ilivyoandikwa, lakini sasa naendelea na marekebisho kisheria ikiwemo Transcript yangu ya chuo baada ya kurekebishiwa kuondoa Typing error.