SoC01 Mimba za utotoni ni "kaburi" la ustawi wa Watoto wa Kike nchini

Stories of Change - 2021 Competition

Uchumi wa Mifugo

JF-Expert Member
May 20, 2021
345
575
Amina (siyo jina halisi)mwanafunzi wa kidato cha tatu katika mojawapo ya shule za sekondari wilayani Kibaha mkoa wa Pwani kila siku anaamka saa 11 ili awahi kwenda shule,shule iliyopo umbali wa kilometa sita kutoka nyumbani kwao.Kila siku anaenda na kurudi kwa miguu, nyumbani hapati kifungua kinywa wala hapati hata mia moja ya kununulia kipande cha muhogo.Nililazimika kufanya mahojiano na Amina baada ya kusikia mazungumzo kati yake na Sofia. Amina alimuomba Sofia kipande cha muhogo wa kukaanga ili atulize njaa kali iliyokuwa inamkabili muda wa mapumziko ya saa nne,badala ya kumpa muhogo Sofia alimjibu kwa kebehi"wewe si unamkataa Roja".Roja kijana dereva bodaboda amekuwa akimshawishi mara kwa mara Amina wawe wapenzi na kwenye mapenzi hayo angekuwa anapewa shilingi 1000 kila siku na kubebwa kwenye pikipiki wakati wa kurudi nyumbani kwao.

Lakini Amina amekuwa akikataa kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi akihofia ndoto zake za kuja kuwa nesi zitapotea kama zilivyopotea ndoto za rafiki yake na jirani yake Asha aliyekuwa anasoma naye darasa moja. Asha alipewa mimba mwaka 2019 na Hamis,kijana anayefanya biashara ya kuuza vitu vya urembo.Asha alipata mimba akiwa kidato cha kwanza na alifukuzwa shule hata kabla ya kufanya mitihani yake ya kumaliza kidato cha kwanza.Hakukuwa na kesi kwa sababu wazazi wa Hamisi na wa Asha walikaa kikao na kukubaliana Hamisi alipe fidia ya 180,000 ambazo alikabidhiwa baba yake Asha.Amina na Asha wote walimpenda nesi Rehema anayefanya kazi kwenye zahanati iliyopo karibu na kijiji chao, walimpenda Rehema kwa sababu ya unadhifu wake na tabasamu lake anapokuwa anahudumia wagonjwa,waliona hata wao wanaweza kuja kuwa manesi kama Rehema lakini kwa Asha ndoto hiyo imepotea imebaki kwa Amina ambaye naye anakutana na vikwazo lukuki.

Asha ni mmoja kati ya maelfu ya wanafunzi wa kike nchini Tanzania ambao ndoto zao za kufanikiwa kielimu na kuja kufanya kazi wanazozipenda zimekufa kwa sababu ya kupata ujauzito wakiwa shuleni.

Pamoja na kuwepo sheria kali ya makosa ya kujamiiana ya mwaka 1998 lakini bado vitendo vya ubakaji vinaendelea kushika kasi.Shirika la utangazaji la Uingereza lilitangaza kuwa kesi zaidi ya 600 za udhalilishaji watoto zilifunguliwa kwenye vituo vya Polisi Zanzibar kwa mwaka 2020 pekee huku ikiaminika kuwa kuna vitendo vingine vingi vya udhalilishaji vinafanyika na kumalizikia nyumbani bila kufika Polisi.Taarifa ya kituo cha sheria na haki za binadamu kuhusu mwenendo wa haki za binadamu ya mwaka 2020 inaonyesha kuwepo ongezeko la matukio ya udhalilishaji 5802 kwa mwaka 2015 mpaka matukio 7837 kwa mwaka 2020.

Taarifa nyingine ya kusikitisha ni ile iliyotolewa wilayani Kibondo mkoa wa Kigoma julai 18,2021 wakati Naibu waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto mheshimiwa Mwanaidi Ali Khamis alipokuwa akikagua na kujionea utoaji wa huduma za ustawi wa jamii na masuala ya maendeleo ya jamiii kuwa wasichana 981 walipewa ujauzito kuanzia januari hadi juni 2021.Yaani kwa miezi sita tu wasichana 981 walipata ujauzito ndani ya wilaya moja!

Pamoja na kuwepo mipango na sera nzuri za Serikali kuhusu ustawi wa watoto wa kike lakini kundi hili linaachwa nyuma,watoto wengi wa kike wanaoanza kidato cha kwanza hawafiki kidato cha nne na wengine wanapata ujauzito wakiwa shule za msingi.

Kuna sababu nyingi zinazopelekea mimba za utotoni baadhi ni hizi zifuatazo;
Umbali kutoka nyumbani hadi shuleni
,njiani wanakutana na vishawishi vingi kutoka kwa madereva pikipiki wanao washawishi kuwapakia bure pia wanapata ushawishi kutoka kwa vijana wengine na watu wazima wanaowashawishi kwa kuwapa hela na ghiliba nyingine.

Baadhi ya wazazi kutokutekeleza wajibu wao pia ni sababu nyingine ya wanafunzi kupata ujauzito.Sera ya elimu bila malipo imechangia ongezeko la mimba kwa sababu wazazi hawafuatilii maendeleo ya shule ya watoto wao kwa sababu hawagharamii elimu,wanaona hawana hasara.Pia hawafuatilii mienendo ya watoto wao,hawajui mabadiliko ya tabia ya watoto wao na hata wakijua hawawakatazi au kuwaongoza kwenye njia sahihi.

Kukosekana kwa chakula shuleni ni sababu nyingine ya kuongezeka mimba za utotoni.Ni rahisi kwa mwanafunzi mwenye njaa anayetoka nyumbani saa 11 asubuhi bila kupata kifungua kinywa na hapewi hela ya chakula kushawishika kuingia kwenye tamaa ya kupewa fedha na wanaume.Mtu mwenye njaa anaweza kufanya chochote.

Kuishi kwenye vyumba vya kupanga karibu na shule nayo ni sababu ya kuongezeka kwa mimba za utotoni kwa sababu wanafunzi wanakuwa huru sana,hawana wa kuwasimamia.Wanaweza kuingiza mtu yoyote na kwa wakati wowote kwenye vyumba vyao.

Pia baadhi ya wazazi wamekuwa wakiwashawishi watoto wao wapate ujauzito ili wafukuzwe shule na kisha waolewe ili wapate hela ya mahari.

Sababu nyingine ni kutokuwepo ufuatiliaji wa makosa ya kujamiiana,kesi nyingi za ubakaji zinamalizikia nyumbani.Hali hii inawafanya baadhi ya wanaume waone si jambo kubwa kumpa mimba mwanafunzi kwa sababu kesi yake itaisha kirahisi kwa kutoa fidia kidogo.

Pia fikra za wazazi kwamba kuliko kumfunga baba wa mtoto na kupelekea mtoto kukosa matunzo ni bora kusiwe na kesi ili baba wa mtoto abaki kwa ajili ya kumtunza mtoto wake inachangia sana kuongezeka mimba za utotoni.

Nini kifanyike?
Yajengwe mabweni ya wasichana katika shule za sekondari na wapewe umuhimu wale wanaotoka mbali na shule
.Mabweni yatasaidia wanafunzi kwa sababu hawatakuwa wanatembea umbali mrefu kwenda shule pia hawatakuwa wanaishi kwenye vyumba vya kupanga.Mabweni yatasaidia pia wanafunzi wa kike wapate muda mrefu wa kujisomea tofauti na nyumbani ambako muda mwingi wanautumia kwa ajili ya kufanya kazi za nyumbani.

Wazazi watimize wajibu wao katika kuwahudumia watoto wao kama kuwapa chakula na huduma nyingine za muhimu,wawanulie hata baiskeli kwa ajili ya kuendea shule,wafuatilie maendeleo ya watoto wao,wasimamie malezi bora ya watoto wao.Pia wasimamie nidhamu ya watoto wao kwa ukamilifu wasiwaachie Walimu tu.

Polisi na wengine wenye dhamana watimize wajibu wao.Kumpa mimba mwanafunzi ni kosa la jinai, wahusika hata wakikimbia au wakimalizia kesi nyumbani wasakwe na wafikishwe kwenye vyombo vya kisheria.

Na mwisho wanafunzi wapewe elimu ya afya ya uzazi, elimu hii ianzie nyumbani na iende hadi shuleni.Walimu na wazazi wawafundishe wanafunzi bila kificho madhara ya kushiriki mapenzi wakiwa na umri mdogo,pia wanafunzi wapewe elimu ya kutumia mipira ya kujikinga dhidi ya mimba na magonjwa ya zinaa. Wanafunzi wafundishwe tarehe hatari za kushika mimba, mwanafunzi auelewe mwili wake kwa undani.Pia wapewe elimu juu ya matumizi ya njia za kujikinga na ujauzito.

Tuache Mila na utamaduni uliopitwa na wakati, huu si wakati wa wazazi kuficha elimu ya afya ya uzazi kwa watoto wao.Ni bora kuwapa elimu na waende kushiriki mapenzi ambayo ni salama kuliko kutokuwapa na kwenda kushiriki mapenzi ambayo si salama.

Imeandikwa na John Ken.
Karibuni kwa majadiliano na kunipiga kura.
 
Raymond Dastan (24)mkazi wa Chamazi Dar es salaam tarehe 30 August 2021 alifikishwa katika mahakama ya wilaya ya Temeke akikabiliwa na mashtaka ya ubakaji na kumpa mimba mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari Magonza mwenye umri wa miaka 16.

Chanzo-Gazeti la Mwananchi la 30 August 2021.
 
Patrick Mtahungwa mwenye miaka 60 anatafutwa na Polisi kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa darasa la tano mwenye umri wa miaka 13 baada ya kumpa pipi,soda na miwa.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora Safia Jongo amesema mtuhumiwa huyo amekimbia baada ya familia ya mwanafunzi huyo anayesoma shule ya msingi Muhulidede kutoa taarifa kituo cha Polisi Shitage kilichopo wilayani Uyui.

Chanzo gazeti la Mwananchi la tarehe 2 Septemba 2021.
 
Mahakama ya wilaya ya Njombe imemuhukumu kifungo cha maisha Steward Ngolle (33) kwa kosa la kumbaka mtoto mwenye umri wa mwaka 1 na miezi 7.Mtuhumiwa alifanya hivyo tarehe 26 julai 2020 katika mtaa wa Mwembetogwa wilayani Njombe mshtakiwa alifanya kitendo hicho baada ya mama yake kwenda kuchota maji.

Chanzo gazeti la Mwananchi la tarehe 30 Augusti 2021.
 
Sasa hivi kila siku nasikia habari za ubakaji,sijui tumepatwa na nini?
Ni kweli ubakaji umeshika hatamu pamoja na kuwepo sheria kali lakini bado matendo ya ubakaji yanaendelea nafikiri kuna mambo mengi yanayochangia kuendelea kwa vitendo hivyo kama imani za kishirikina, matatizo ya kisaikolojia nk.
 
Wasichana 42 wa jamii ya kifugaji ya kimasai wanaoishi wilaya ya Longido mkoani Arusha wamekatisha ndoto zao za elimu baada ya kupata ujauzito.

Chanzo gazeti la Nipashe-tarehe 7 Septemba 2021.
 
Afisa ustawiu wa Jamii mkoani Morogoro Jesca
Kamugelau amesemay matumizi ya mimba na ndoa za utotoni yamezidi kuongezeka katika mkoa wa Morogoro ambapo katika kipindi cha mwaka mmoja 2020/2021 zaidi ya watoto 1200 wamepata ujauzito hali iliyokatisha ndoto zao za kuendelea na masomo.
 
Hili suala la mimba za utotoni limekua miaka na miaka , na hatufanikiwi kwa asilimia kubwa katika jitihada zetu kwasababu hatuangalii sababu kuu. Mabadiliko ya biologia ya mwili ndio huchangia kuleta uhitaji wa kufanya ngono, mwili huwa na mahitaji ya kiasili kila hatua ya ukuaji , ingekua sio sheria za mamlaka ziliopo, makatazo ya kidini , karibia kila mtu angefanya ngono , hivyo basi tunatakiwa tuhakikishe kabla ya vijana kupevuka na baada ya kupevuka wanapata elimu ya maumbile bila kuficha ili waielewe miili yao ya kwamba ukitokea hali fulani inamaanisha nini na nini kitatokea ukifanya kitu fulani, na ni kipi ufanye kisitokee kitu fulani. Tunatakiwa tuondoe mtizamo wa muda mrefu yakua kuwafundisha watoto wanaoekekea kupevuka mpango wa uzazi ni kuwahalalishia kufanya ngono, tunatakiwa tutoe elimu ya uzazi kwa vijana wanaoekekea kupevuka na njia za uzazi wa mpango. Baada ya kutoa elimu ya utambuzi na kuelewa mabadiliko ya kimwili, elimu ya uzazi na uzazi wa mpango , hapo ndipo tufuatie sheria , kujenga shule za bweni . Hawa watoto kama mzazi unaweza ukampa mahitaji yote bado akajiingiza kwenye ngono na kupata mimba kwa kushawishiwa , waweza kumpa hela ya kula shuleni asubuhi , mchana chakula kipo shuleni lakini akashawushika na mwenzake ambaye ananunuliwa chips au chakula tofauti katika canteen ya shule ya bweni badala ya kula chakula Cha shule.
 
Wakazi wa kijiji Cha Ruvu Darajani wilayani Bagamoyo wameamua kujenga shule ya sekondari ili watoto wao wasitembee umbali mrefu kufuata elimu ya sekondari.Walipohojiwa na Star Tv wamesema umbali mrefu unasababisha watoto wao wa kike kupata ujauzito na hivyo kushindwa kuendelea na masomo.
 
Mm naona hii kampeni ya kukataza watoto kuchakatana inaenda kinyume na maumbile (nature) ndiyo maana haifanikiwi. Ngono ni moja ya miito ya asili ya mwili wa mwanadamu. Ni kama njaa ama kiu vile.

Sasa mtu ameanza kubanwa na njaa ama kiu(amebalehe). Ninyi mnataka apambane kujizuia. How?

Itafutwe namna hii kitu iruhusiwe watoto walio balehe wachakatane kama kawaida. Mnapingana na mwenyezi Mungu??!!
Anayeweza muvumilia atavumilia. Asiyeweza kuvumilia njaa ya ngono, ale tu. But ale kwa akili.
 
Kuna msichana mmoja alikuwa anasoma shule ya wasichana Masasi. Shule ya bweni. Akiwa likizo alikuwa anaburudisha vidume. Akiwa kidato cha nne, baada ya likizo ya covid19 mwaka jana, shule ilipofungua, ifika shuleni akiwa na mimba. Amafukuzwa shule mwezi Agosti. Yaani ilibaki miezi miwili ahitimu kidato cha nne.

Bweni ni msaada?
 
Mchango mzuri
Hili suala la mimba za utotoni limekua miaka na miaka , na hatufanikiwi kwa asilimia kubwa katika jitihada zetu kwasababu hatuangalii sababu kuu. Mabadiliko ya biologia ya mwili ndio huchangia kuleta uhitaji wa kufanya ngono, mwili huwa na mahitaji ya kiasili kila hatua ya ukuaji , ingekua sio sheria za mamlaka ziliopo, makatazo ya kidini , karibia kila mtu angefanya ngono , hivyo basi tunatakiwa tuhakikishe kabla ya vijana kupevuka na baada ya kupevuka wanapata elimu ya maumbile bila kuficha ili waielewe miili yao ya kwamba ukitokea hali fulani inamaanisha nini na nini kitatokea ukifanya kitu fulani, na ni kipi ufanye kisitokee kitu fulani. Tunatakiwa tuondoe mtizamo wa muda mrefu yakua kuwafundisha watoto wanaoekekea kupevuka mpango wa uzazi ni kuwahalalishia kufanya ngono, tunatakiwa tutoe elimu ya uzazi kwa vijana wanaoekekea kupevuka na njia za uzazi wa mpango. Baada ya kutoa elimu ya utambuzi na kuelewa mabadiliko ya kimwili, elimu ya uzazi na uzazi wa mpango , hapo ndipo tufuatie sheria , kujenga shule za bweni . Hawa watoto kama mzazi unaweza ukampa mahitaji yote bado akajiingiza kwenye ngono na kupata mimba kwa kushawishiwa , waweza kumpa hela ya kula shuleni asubuhi , mchana chakula kipo shuleni lakini akashawushika na mwenzake ambaye ananunuliwa chips au chakula tofauti katika canteen ya shule ya bweni badala ya kula chakula Cha shule.
 
Hivi si nyinyi nyinyi mlikuwa mnapinga MagufuliJP wakati anasema mimba hapana lazima tuzuie zinaa kwa watoto wetu mkasema oooh haki za binadamu. Waendelee na shule basi.


Tunaelewana tu. MagufuliJP atakuwa anashuka huko kaburini.
 
Screenshot_20210922-125512_1.jpg
 
Back
Top Bottom