Mimba ya mke wangu huaribika akifikisha mwezi au zaidi

Duuh hilo tatizo hata mchepuko wangu analo. Ngoja wataalamu waje!!!
 
Nenda hospital kubwa mkuu,

Mke wangu alikua na tatizo kama lako, sasa hivi tuna 2 kids,

Kama uko moshi, nenda Kilimani pale kuna kituo kizuri sana.
 
Mke wangu mimba hualibika baada ya mwezi au zaidi ya mwez kila akipata ualibika nifanyeje msaada

MIMBA KUHARIBIKA.jpg


MIMBA KUHARIBIKA
MIMBA CHANGA (ndani ya miezi3) KUHARIBIKIWA, CHANZO NA SABABU, DALILI NA NINI UFANYE ILI KUZUIA ISITOKEE TENA

Somo hili ni refu na kwa hiyo limegawanyika sehemu kuu tatu
1- Dalili za mimba kuelekea kuharibikiwa
2- Chanzo na sababu za mimba kuharibika
3- Nini cha kufanya ikiwa huwa unapatwa na hali hiyo mara kwa mara.

SEHEMU YA KWANZA
Ni kawaida sana mimba kutoka au kuharibika bila kukusudia au bila wewe kujua kama imetoka au inakaribia kutoka. Wakati mwingine hutoka tu bila sababu yeyote na hata kama utapimwa na vifaa vya kisasa kabisa bado sababu za mimba kuharibika hazitajulikana. Ikiwa utajua ya kwamba mimba imetoka

CHA KWANZA ni vizuri kujua sababu ya mimba hiyo kutoka, hasa kama imeharibika kwa mara ya pili na zaidi. Sababu zinaweza kuwa nyingi kama vile utakavyo ona katika aya zifuatazo hapo chini, kuna sababu za kijamii na kiafya. Sababu za kijamii zitafutiwe ufumbuzi kijamii, mfano mtu amelaaniwa (hapo kama una amini katika dini) huwezi tena kupona kwa kutumia dawa, lazima ufunguliwe na kifungo hicho kwanza.

CHA PILI kupambana na icho kisababishi, baada ya kupima na kupata ushauri basi itakufaa sasa upate dawa au kufuata ushauri uliopewa, ukimaliza dozi rudi hospitalini ili uweze kujua kama umepona kabisa au la. Kunayo tabia ya watu wengi tu askisha maliza dozi ndio inakuwa basi anaendelea na Maisha yake, hapo unakuwa unakosea. Jitahidi kurudi hospital na kupima tena upate uhakika wa tatizo kama limeisha au la. Kama halijaisha inakuwa rahisi kwa daktarin kuchua vipimo vingine au kukupa dawa ingine.

CHA MWISHO ni kujaribu tena kubeba mimba, baada ya kuona mambo yote yako sawa, au sasa unaamini uko vizuri basi unajaribu tena kupata mimba. Zingatia siku zako za uzazi, na zingatia kupika vyakula vizuri ili mume wako apate nguvu ya kutoa mbegu nyingi na zenye afya njema. Usafi pia wa mwili na kitanda ni muhimu. Usinuke na kutoa harufu mbaya.
Mara nyingi swala la kwanza na pili watu huruka na kuendelea nakutafuta mimba. Zaman wakati vifaa na wataalamu walikuwa hakuna hiyo ilikuwa sawa lakini Siku hizi kuna vifaa ujitahid kutafuta sababu. Hii ni Kwa sababu pia uwezo wa wanawake kuzaa umepungua sana. Wanawake wachache wanazaa watoto zaid ya 6 hata wakitaka kuzaa wanajikuta hawawezi. Wengine wanachelewa kuolewa, kwa mana hiyo wanaanza kutafuta watoto wakati Mayai bora mengi yameishaisha.

DALILI ZA MIMBA CHANGA KUWA IMEHARIBIKA AU KWAMBA INAELEKEA KUHARIBIKA
Kwahiyo ukiona dalili zifuatazo basi jua mimba yako changa imetoka au inataka kutoka kimyakimya.
1- maumivu makali ya tumbo la uzazi (yanachoma)
2- kutoka uchafu kama ugoro au damu ya bleed au mabonge ya damu.
3- kutoka na kitu kama kinyama lakini chenye damu.
Note: unaweza tokwa na damu kama matone hiyo inaweza isiwe mimba imetoka. Jaribu kupima tena na tena. Usipime Siku iyoiyo Kwa kuwa Homoni za mimba zinakuwa Bado zipo.
Cha msingi pia ni kupata ushauri ukikutwa na hali hiyo. Kama ulikuwa unajua una mimba basi dalili zifuatazo ni hatari na lazima zikupatapo uwahi hospitaln.
1- maumivu makali ya tumbo kichwa na mgongo wachini kwa pamoja au mara moja moja.
2- Mafua makali, kutapika sana, kuishiwa maji mwilini na kikohozi.
3- kupata damu ya bleed lakin yenye rangi tofauti na ya bleed.
4- kutokwa na uchafu unaomiminika kidogo kidogo kutoka ukeni.
5- kupungua Kwa dalili za mimba, kujisikia kawaida na kama imeharibika dalili zinakoma kabisa.
Nenda Hospitali Ukampime mke wako na itajulikana sababu ya mimba kuharibika. Asipo pona nitafute kwa wakati wako ili niweze kumtibia mke wako mimba zisiweze tena kuharibika.
 
Back
Top Bottom