MIMBA: Wanafunzi wa chuo wanazidi kutoa mimba

sido9797

Senior Member
Aug 15, 2018
161
225
Hali inatisha kwa hiki kizazi chetu na kinachoendelea kwakweli hawa vijana wa chuo wanatoa mimba sana.
Naona kuna kila sababu ya kuhakikisha elimu inatolewa kwa vijana wa chuo kuanzia mwaka wa kwanza mpaka walio mwisho wa masomo (kuanzia cheti, diploma,degree).

Masters sitaki kuwaongelea sana ila hii tabia sio njema kama nchi inatakiwa kusimama kulisemea hili jambo pamoja na viongozi wa dini.
Nawashauri vijana kuna njia nyigi za kuzuia mimba wazingatie mfano kondomu, sindano, vidonge n.k natambua ni sumu na ni hatari kwa afya ila ni bora ujilishe sumu wewe kuliko mjikute mnashiliki wote wawili kuua kiumbe kisicho na hatia kwa kuogopa kutumia kinga ambazo mnaona ni sumu au kwa kuweka tamaa ya ngono bila kufikiri athari zake bila kujali ni siku ambayo kunauwezekano wa kushika mimba.

Madhara ya kutoa mimba ni makubwa kwa mfano wengi wameharibu afya zao, wamekufa yeye na mtoto, wamekonda na kushindwa kurudisha afya zao, wengine kushindwa kushika mimba milele.
Tena kuna watu wameoa watu waliotoa mimba kiasi kwamba hawezi shika mimba tena na saivi anahangaika nae kwenye maombezi na waganga wa kila aina ila kizazi kilisha tolewa na unahangaika mtu anakuangalia tu kumbe anaelewa yeye alikosea wapi.

Wanaume kama chachu ya haya wamepelekea mimba nyingi kutolewa kwa kuona bado wanatakiwa kusoma hivyo muda bado wa kuzaa hii ndio imekua sababu kubwa na kupelekea haya.

Nalaumu pande zote kwa mwanaume na mwanamke kama mnaoma muda bado kuweni makini mzingatie njia za kuzuia mimba na siku za kushika mimba.
All in all wewe kama kijana unaeenda chuo jali mambo ya msingi na epuka ngono zembe kama ikiwezekana usifanye haya mambo.

NB. Watoto wengi wametupwa kwenye vyoo, wamemwaga damu kama mabomba ya maji, vijusi vimetendwa unyama wa hali ya juu inasikitisha sana lakini yangu ni hayo, wakuelewa ataelewa wakuguswa na aguswe lakini hali sio njema vyuoni.(vyuo vyote Tanzania)


Nakaribisha maoni juu ya hili jambo naamini kuna baadhi mmepitia haya na hamtojisikia vyema lakini msiache kuchangia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom