Nimekuwa nikilitafakari hili na kwa kweli kuna maswali huwa najiuliza ila leo nimeona niwaulize wana MMU. Kwanza kabisa napenda ieleweke kuwa nachukizwa sana ninapoona mtu mzima anamtongoza mtoto mdogo wa shule, yaani huwa inaniudhi sana ni vile tu saa nyingine unakuwa huna la kufanya maana unaweza kuingilia ukajikuta katika wakati mgumu sana.
Pili kwenu wana MMU, hivi ni kweli ni sahihi pale mtoto wa shule anapopewa mimba kumchukulia kuwa hana kosa lolote na hivyo basi mzigo wote wa hatia inatakiwa ubebwe na mwanaume. Nasema hivi kwa sababu kwa namna moja au nyingine mimi naona kama utaratibu huu ni kurudisha nyuma jitihada za kumkomboa mwanamke, kutokana na ukweli kuwa kwa upande mmoja unakuta tunajitahidi kuwaeleza watoto wetu wa kike kuwa wako sawa na wanaume na wanatakiwa kujiamini lakini linapokuja suala la mimba ni kama vile tunawaambia hamna akili za kutosha kufikiri hivyo mimba hizi mnazobeba ni kwa sababu ya wanaume ambao ni wajanja sana na wana akili kuliko ninyi na ndiyo maana wanaweza kuwadanganya na kuwaharibia masomo na hivyo hamna kosa lolote mlilofanya.
Ni maoni tu wadau naomba michango yenu.