Mimba imetoka(imeharibika)...damu haikatiki. Nini tiba yake? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mimba imetoka(imeharibika)...damu haikatiki. Nini tiba yake?

Discussion in 'JF Doctor' started by Baba Matatizo, Mar 3, 2012.

 1. B

  Baba Matatizo JF-Expert Member

  #1
  Mar 3, 2012
  Joined: May 5, 2011
  Messages: 335
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mke wangu alikuwa na mimba ya miezi 2.....alipata homa mimba ikaharibika.mpaka sasa ni siku ya kumi toka aanze kupata damu baada ya mimba kuharibika.huku nilipo ni kijijini sana na dk wa zahanati kasema damu itakata yenyewe.Je ni dawa gani anatumia mwanamke aliyeharibu mimba kama antbiotic?je ni dawa gani inasaidia kukata damu?Msaada jamani. Huku nilipo ni Zaid ya kijijin.
   
 2. phina

  phina JF-Expert Member

  #2
  Mar 3, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 414
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  anatoka damu kiasi gani??kama anajaza pedi moja ndani ya lisaa limoja anapoteza damu nyingi sana!
  Kwa kawaida huwa anaenda hedhi siku ngapi??mara nyingine baada ya kupoteza mimba mtu anaweza kwenda hedhi siku nyingi kuliko kawaida.
  Either way..i suggest uende hospitali kubwa kidogo!maisha ya mkeo yaweza kuwa hatarini hapa!
  Poleni sana..mungu atawaponya!
   
 3. Kennedy

  Kennedy JF-Expert Member

  #3
  Mar 3, 2012
  Joined: Dec 28, 2011
  Messages: 11,345
  Likes Received: 2,984
  Trophy Points: 280
  Mkuu pole sana,hapo hata kama ni kijijini sana mpeleke mkeo hospitali kwaajili ya kunusuru maisha.
   
 4. dubu

  dubu JF-Expert Member

  #4
  Mar 3, 2012
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 3,072
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  mkimbize hospital haraka. usiulize mkuu...kimbiza hospital fasta kabla hata madoctor hawajagoma tena.
   
 5. Dunda kwetu

  Dunda kwetu JF-Expert Member

  #5
  Mar 3, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 265
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Pole sana...mpeleke hospitali ya wilayani kwako aua mkoa kusiwe na ngoja ngoja tena
   
 6. Ndokeji

  Ndokeji JF-Expert Member

  #6
  Mar 3, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 525
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Mkuu pole sana. kwa kawaida baada ya mimba kutoka mwanamke hutoka damu week 3 -5 wengine hadi week 8. Zingatia yafuatayo ili kuokoa maisha ya mkeo 1. Mpeleka hospitali kubwa referal hosp 2. Hakikisha anakunywa maji na juice ya kutosha 3. Hakikisha anatumia matunda ili kupata vitamin kama machungwa,nanasi,embe, papai etc 4. Hauruhusiwi kusex na mkeo mpaka atakapopona 5. Haruhusiwi kuingizi kitu chochote kwenye uke 6. Haruhusiwi kufanya kazi yoyote mpaka apone 7. Haruhusiwi kufanya mazozi yoyote 8.apatiwe vitamin c and k supprement 9. Iron sulphate apewe kwa ajili kuzuia anemia 10. Antibiotic hapa mpaka vipimo ili kujua kama anainfection . 11. Usifanya uzembe kumbuka kutoka kwa damu ni hatari sana anapote maji, minerals, mpeleke hospita fasta kama huna hela kopa
   
 7. k

  kisukari JF-Expert Member

  #7
  Mar 3, 2012
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,760
  Likes Received: 1,050
  Trophy Points: 280
  umetoa ushauri mzuri sana
   
 8. Ndokeji

  Ndokeji JF-Expert Member

  #8
  Mar 3, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 525
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  asante mkuu
   
 9. B

  Baba Matatizo JF-Expert Member

  #9
  Mar 3, 2012
  Joined: May 5, 2011
  Messages: 335
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  asanteni kwa ushauri.ngoja niandae mazingira ya kwenda mbele.
   
 10. k

  kamili JF-Expert Member

  #10
  Mar 3, 2012
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 714
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Mimba yoyote inayotoka ikiwa na umri wa miezi mitatu au chini ni lazima asafishwe kwa evacuation au kwa manual vacuum aspiration.
   
 11. hollo

  hollo JF-Expert Member

  #11
  Mar 3, 2012
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 781
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Pole sana,mpeleke hospital akasafishwe.
   
 12. doctorz

  doctorz JF-Expert Member

  #12
  Mar 3, 2012
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 907
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Poleni saaana.

  Inawezekana ni incomplete abortion. Hii ya kutoka damu hata kama ni kidogo kidogo yaweza ikaleta sepsis. Mungu apishe mbali. Zaidi ya kufanya ka anavyo kushauri Ndokeji, please mpeleke hospitali akafanyiwe D & C. Bila ya hivyo waweza kupoteza wife au ukampatia athar kubwa hata kufikia kupoteza kizai. GOOD LUCK.
   
Loading...