Zifahamu dalili zinazoashiria mwanamke ni mjamzito

View attachment 343171


Hutokea mara nyingi kina mama na wasichana kuwa na kipindi cha msongo wa mawazo pale wanapokosa siku zao na hasa kama hawakutumia njia ya uzazi wa mpango au kinga nyingine ya kushika mimba.

Kukosa siku zako sio dalili pekee ya kushika mimba, bali kuna dalili zingine utalazoziona. Kuna sababu nyingine nyingi zinazoweza kukufanya ukose siku zako, hivyo soma dalili za mimba ili ikusaidie kupata uhakika.

Moja, ni mabadiliko katika siku zako. Hii kitaalamu tunaita spotting. Unaweza kushika mimba ukaendelea kuona damu mwezi huo. Hii hutokea yai lililorutubishwa linapojipandikiza kwenye kizazi. Mishipa ya damu iliyojaa kwenye ukuta huu tayari kulisha kiumbe huachia damu kidogo amabazo mwanamke anaweza kufikiri ni hedhi yake ya kawaida. Hata hivyo mabadiliko yataonekana kwani kiwango na siku za damu hubadilika.

Pili, ni kuongezeka ukubwa na kupata maumivu kwenye maziwa. Hii inasababishwa na ongezeko la homoni za istrogen pale unapokuwa umeshika mimba. Hali hii huisha katika kipindi cha miezi mitatu ya kwanza.

Tatu, ni kichefuchefu na kutapika. Hali hii huwa mbaya zaidi wakati wa asubuhi unapoToka kulala. Hii ni kwa sababu ya homoni ya projestroni ambayo husababisha kupungua nguvu kwa misuli ya mrija wa chakula au koromeo.

Nne, ni uchovu usiokuwa na usingizi usiokuwa na sababu. Hii hutokea kwa sababu ya ongezeko la homoni ya projestroni na mama utajikuta unasinzia mara kwa mara. Hali hii huisha unapoanza mwezi wa nne wa mimba ila hata kipindi cha mwisho wa mimba hujisikia uchovu.

Tano, kusumbuliwa na harufu mbalimbali. Hasa kama unapata mimba kwa mara ya kwanza, utachukia harufu za vyukula na vinywaji mabalimbali. Wakati mwingine hata harufu za watu walio karibu nawe zinaweza kukukera.

Sita, ni kujaa gesi tumboni. Utaona baadhi ya nguo zako zinakubana zaidi hasa sehemu ya tumbo. Hii ni kwa sababu ya homoni nyingi mwilini zinazokufanya kijisikia tumbo kujaa.

Saba, Kukojoa mara kwa mara. Hii kwanza hutokana na kuwa na damu nyingi mwilini ambayo huongezwa na homoni za ujauzito makusudi kutoa rishe ya kutosha kwako na kwa kiumbe tumboni. Ukiwa na damu nyingi pia utakojoa sana za kikemia mwilini. Pili utajisikia kwenda haja ndogo mara nyingi pale kiumbe kitakapoongezeka na kubana kibofu cha mkojo.

Nane, kuongezeka kwa joto la mwili. Kwa kina mama ambao hupima joto lao kama njia ya uzazi wa mpango, watagundua kuwa joto limepanda kwa muda wa wiki mbili au mbili na nusu mfurulizo.

Tisa, kutoona siku sako kabisa. Kwa wale ambao siku zao hazibadiliki na huenda vizuri yawezekana kugundua pale wanapokose siku nap engine kukimbilia hospitali. Hata hivyo kwa wale ambao siku zao hubadilika sana wataona kawaida ila kama ameshika mimba taona mchanganyiko wa kichefuchefu, uchovu na kusinzia pamoja na kukojoa mara kwa mara.

Kumi, kupima mkojo kwa kutumia kipimo cha karatasi ngumu. Famasi nyingi huuza vipimo ambavyo ikikichovya kwenye mjojo wako huweza kugundua homoni za mimba kwenye mkojo.

Hii unaweza kupima mwenyewe ukiwa nyumbani hata kazini. Kipimo hiki ukisha kichovya kwenye mkoja kama katatsi inavyoelekea utaona mistali baada ya dakika moja inajitokeza upande wa chini.

Ikitokea mistari miwili basi unaweza kuwa na mimba na ukitokea mmoja utakuwa huna mimba. Kilingana na kiwango cha homoni mwilini, kuna kina mama hakionyeshi majibu mpaka upitishe wiki moja bila kuona siku zako.

Pamoja na dalili hapo juu, unatakiwa kupata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa daktari.
Hapo kwenye namba moja tafadhali nifafanulie, je, mjamzito anaepata hedhi anapitia dalili na karaha zote za hedhi kv maumivu ya tumbo, mgongo, kiuno na kutoka vichunusi japo damu c nyingi na imetoka siku mbili mfululizo?
 
Unaweza ukawa umeshika mimba, ila bado ni mapema sana kusema umeona dalili.

Kwa sababu kwa sayansi ya kawaida,tendo la kushika mimba lina hatua kuu mbili:

Kwanza kuna sperm kurutubisha yai (fertilization) hii kikawaida inafanyika ktk mirija ya uzazi, baada ya hapo,yai lililorutubishwa linaanza safari ya kushuka kuja kwenye mji wa mimba..na safari hii huchukua siku kadhaa.

Kinachofuata ni lile yai ambalo wakati huo linaendelea kukua,linajipandikiza ktk mji wa mimba,ili kuruhusu mchakato wa kukua kuwa mtoto..na hapo ndipo kondo la mtoto(nyuma) linaanza kutengenezwa..sasa dalili (nyingi) za mimba zinatokana na hili kondo.

Kwa hiyo basi,kwa vyovyote vile kuanza kuona dalili ndani ya wiki moja ni vigumu kiukweli.
 
Kama alimwaga nje na unauhakika kwa asilimia zote haiwez kua mimba hyo labda mabadiliko tu mengine ya kimwili, kawaida ili mimba iingie lazma yai lirutubishwe na sperm hapa ndo itatokea fussion of nucleus but kama hii kitu ilipita nje it means there is no fertilization take place so hakuna mimba hapo. Kama unauhakika 100% hakuna mbegu sperm zilizo mwagikia kwa veginal pore.
 
Mzunguko wangu ni wa siku 30 huwa napata period tarehe 7. Mwezi wa 7 nilipata period, tarehe 21,22,30/7na 5/8 nilisex. Sasa ni mjamzito, je ni tarehe ngapi kati ya hizo ndo nilishika ujauzito?
 
Kuna kesi nimesikia eneo fulani.kuna kijana analalamika kuna binti amekutana nae kimwili siku moja pia wametumia kinga (kondoim)mwanzo mwisho ila baada ya wiki mbili anamwambia ana mimba yake.kijana hamini kilichomtokea. Je, kuna ukweli wa mimba kuwa yake.
 
Marekebisho kipimo ni UPT. Ili hormone ya HCG iweze onekanika kwa wingi kwenye mkojo ni lazima ujauzito uwe na zaidi ya sku 14 tokea sku ya hatari mlio fanya. Na tena kipimo chenyewe huonyesha weak postive sana. Chini ya hapo unaibiwa by rayvany.
Mkuu Mimi nimekula mzigo July 21 akiwa yuko siku ya 19 ( kwa maelezo yake) ....tena siku hiyo kugegeda nikampa juice ya majivu ili incase alidanganya mimba isitunge...cha ajabu ndani ya siku 6 akaniambia Ana hamu ya udongo, Mara usingizi kila Mara...sasa juzi jumanne( zikiwa zimepita week 2) amepima yy mwenyewe kwa kutumia UTP na ameniambia ana mimba...sasa nafikiri nimpeleke hospital for re-check up ili nijue ukweli wa hiyo mimba...je Ina muda gani na ni yanguu?

Ushauri pliz
 
Habari,

Jamani nisaidien. Mwanamke bikra ila amejaribu kukutana na mpenzi wake ilihali hakuvua chupi na jamaa akamwaga juu ya chupi yake.je kuna uwezekano wa mwanamke huyo kupata ujauzito?
 
Habari..jamani nisaidien..mwanamke bikra ila amejaribu kukutana na mpenzi wake ilihali hakuvua chupi na jamaa akamwaga juu ya chupi yake.je kuna uwezekano wa mwanamke huyo kupata ujauzito??
Unamaanisha chupi ilifanya kazi kama kondom,hapo nadhani yale majimaji na sperm za jamaa zimepenetrate bila matatizo yoyote,hongera sana hapo ujauzito ni nje nje kama ulikuwa kwenye danger days zako
 
Naomba msaada. Nimeona dalili hizi na ningependa kujua endapo ni dalili za ujauzito.

1. Kula kupita kiasi
2. Kuchagua chakula
3. kutopenda harufu ya mafuta
4. Kichefuchefu asubuhi
5. Kuhisi joto

Kama si dalili za ujauzito ni dalili za nini?
 
Back
Top Bottom