Mimba hewa yamfukuzisha chuo mwanafunzi wa chuo cha veta kongowe- kibaha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mimba hewa yamfukuzisha chuo mwanafunzi wa chuo cha veta kongowe- kibaha

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by 1973 RAJ MINJA, May 21, 2012.

 1. 1

  1973 RAJ MINJA Member

  #1
  May 21, 2012
  Joined: Aug 28, 2009
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwanafunzi wa kidato cha nne aliyechaguliwa kujiunga chuo cha ufundi veta kibaha kongowe kafukuzwa chuo kwakuwa amekutwa na mimba hewa baada ya kwenda kupimwa katika zahanati ya kongowe. Hakuna kipimo kilichofanyika zaidi ya kuminywa matiti . Kawaida kipimo cha mimba kipo ni strip ya urine for pregnancy test hiki hakikufanyika pale zahanati ila walirubuniwa na pesa kidogo kumuandikia ripoti ya uongo kwamba ana mimba.

  Kwa uchungu familia ya binti huyu walitafuta msaada kwa m.kiti wa zahanati ile hawakupata msaada, wakaenda kwa m.kiti wa serikali za mitaa bila mafanikio, haikutosha diwani kaelezwa naye kashindwa. Masharti wanayopewa kutoka kwa mwalimu mkuu baada ya kwenda kujieleza viongozi hao, anasema walete taarifa za daktari aliyempima akithibisha hakuwa na mimba ili aendelee na shule. Wakienda pale zahanati ya kongowe wanasema ili nao waandike hivyo vyema kwanza wakubali kama alikuwa na mimba ndipo wabatilishe,kwakuwa binti na wazazi wake japo si wasomi wanaelimu ya kujua kama wanarubuniwa hawakuweza kusaini hiyo karatasi.

  Wanajamii wazazi wa huyu binti ni wakulima na uwezo wao ni duni wameshindwa wafanye nini au waelekee wapi? Wanasema ukielimisha mtoto wa kike ume elimisha jamii, je tunakwenda wapi kielimu kuhusu watoto wa kike. Huu ni uuwaji kabisa. Tunaomba msaada wa kimawazo hata wa kisheria. Imeniuma nimeleta kwenu jamii nanyi mchangie juu ya hili. ushahidi na vielelezo wa vipimo vilivyo pimwa hospitali tatu tofauti vipo vikionyesha hakuna mimba kwa siku ile iliyoonyesha ana mimba pale zahanati ya kongowe. Kwa tetesi nafasi amepewa mtoto wa kigogo kwa kuhonga laki nne.
  Huyu mwalimu hafai na hapo zahanati huyo daktari hafai.

  Viongozi wa serikali waliwajibishwa, kwanini na hawa waliohusika kumuharibia binti huyu wasishitakiwe kwa kosa hilo pamoja na mkuu wa shule?
   
 2. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #2
  May 21, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,078
  Likes Received: 7,301
  Trophy Points: 280
  Sina uhakika sana, but nahisi viongozi wote hapo ni magamba.
  Pili kuna vyombo Kama TAMWA, TAWLA & USTAWI WA JAMII jaribu huko.
  Watoto wengine wa vigogo hawana kabisa mwamko wa kusoma, basi tu wanajilazimisha.
  Matokeo yake ndio wanakuja wanafeli wao tu shule nzima na kuiharibia sifa shule.
   
 3. Pasco_jr_ngumi

  Pasco_jr_ngumi JF-Expert Member

  #3
  May 21, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 1,811
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Mbona sielewi????

  Huyo binti anasoma chuo au sekondarii???

  Kama chuo ni ruksa kuendelea na masomo!!!!


  Alafu nna waswas wew umehusika, data hizo zote umepata wapi??????
   
 4. N

  Nguto JF-Expert Member

  #4
  May 21, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,652
  Likes Received: 627
  Trophy Points: 280
  Waunganishe hao wazazi na TAWLA (Chama cha wanasheria wanawake) ndiyo kazi yao kutetea wanyonge. Watalitatua hilo tatizo.
   
 5. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #5
  May 21, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,315
  Likes Received: 19,460
  Trophy Points: 280
  ujumbe utakuwa umeshawafikia..au ingia kwemye website ya Tamwa ama mtafute Halima Mdee
   
 6. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #6
  May 21, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  dah kweli wanadamu wana roho mbaya kweli, atafute msaada wa kisheria zaid kama atapambana kutetea haki yake kuna watu wa 4 hapo mpaka sasa hawana kazi
   
 7. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #7
  May 21, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,559
  Likes Received: 18,284
  Trophy Points: 280
  Raj Minja,
  Kwanza naomba usichafue jina la Chuo cha Veta ambacho kimezinduliwa hivi majuzi tuu kwa sababu it has nothing to do na hii long story yako!.

  Umeandika mambo mengi, umeacha kuweka time frame ili upate symphathy humu!.

  1. Hapo ni kijijini, binti akiwa na mimba kijijini watu wanajua tuu hata bila ya pregnant test.
  2. Siamini kuwa eti ile test ya kumshika maziwa ndio iliyomfukuzisha shule!.
  3. Shule iliona dalili ndipo akapelekwa kupimwa hapo zahanati na kufukuzwa shule!.
  4. Kama shule alifikuzwa hiyo nafasi ya Chuo cha Veta kaipataje?. Kwa matokeo gani?.
  5. Upatikanaji wa Nafasi vyuo vya Veta ni kwa maombi na kupasi usahili na sio kupangiwa kama kupasi sekondari au vyuo vya elimu hivyo hakuna cha mtu kuchukua nafaso ya mtu!.
  6. Inavyoelekea mwanzo mimba ilikuwepo na binti akafukuzwa shule lakini sasa mimba haipo na binti anataka kurudi shule kwa kisingizio hapo mwanzo hakupimwa mkojo!.
  7. Hiyo issue ni simple na straight, aende pale Tumbi akafanye medical exam ni bure, watampatia cheti cha uthibitisho kuwa hakuwahi kushika ujauzito, atakiwasilisha shule, atapokelewa na kuproceed na kujiunga Veta!.

  Pasco.
   
 8. F

  FJM JF-Expert Member

  #8
  May 21, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Pasco, kabla ya kujibu hii hoja ningeomba u-declare your interest (yoyote) kwa VETA.

  Pili, unamjua huyo binti anayezungumziwa hapa? Unataarifa za vipimo vyake? Where you present wakati anashikwa matiti ili kujua kama ana mimba au la? What facts do you have in order to refute whatever claim zilizoletwa hapa?


   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #9
  May 21, 2012
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Kwani chuo hawaruhusiwi kusoma wenye mimba? au hiyo veta ni sekondari kwa sabab kama ni chuo unaruhusiwa kuolewa/kuoa, kuzaa na masoma yanaendelea kama kawa.
   
 10. pgasper

  pgasper JF-Expert Member

  #10
  May 21, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 311
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  stori haielewki
   
 11. papason

  papason JF-Expert Member

  #11
  May 21, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 2,317
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Wabongo ni wajanja wajanja sana! Bila kupindisha maneno huyo 'wakusoma' alipachikwa mimba baada ya ishu kubumbuluka akaishusha sasa anataka kuchezea akili za watu!
   
 12. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #12
  May 21, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,806
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  mie sijaelewa,aliyeelewa anifafanulie hii picha inaelekea ni nzuri.....:eyebrows:
   
Loading...