Bowbow
JF-Expert Member
- Oct 20, 2007
- 541
- 32
Mil. 142.9/- zatumika kutangaza bajeti
MBUNGE VITI MAALUM
na Irene Mark, Dodoma
SERIKALI ilitumia jumla ya sh milioni 142.96 kugharamia safari za mawaziri na wasaidizi wao mwaka jana, wakati wa ziara za mikoa yote nchini kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kutoa ufafanuzi kuhusu bajeti ya serikali ya mwaka 2007/08.
Akijibu swali bungeni jana, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge) Dk. Batilda Burian, alisema ziara hizo zilikuwa muhimu licha ya wabunge, ambao ni wawakilishi wa wananchi kuweza kuifanya kazi hiyo.
Akitetea uamuzi wa serikali kuwatumia mawaziri kuitekeleza kazi hiyo licha ya kuwepo kwa wabunge, Dk. Buriani alisema wabunge kama wawakilishi wa wananchi wanao wajibu wao na serikali nayo kwa upande wake inayo majukumu yake.
Aliliambia Bunge wakati akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Viti Maalumu, Mhonga Said Ruhwanya (CHADEMA), kuwa fedha zilizotumika zilitokana na fedha zilizotengwa katika bajeti ya serikali chini ya mafungu ya safari za viongozi hao.
Katika swali lake, Ruhwanya alitaka kujua sababu zilizoifanya serikali kulitawanya Baraza la Mawaziri mikoani ili kuelezea utekeleazaji wa bajeti ya mwaka 2007/08 na fedha gani zilitumika katika ziara hiyo kuwalipa mawaziri, wasaidizi wao na watendaji wa serikali waliohusika katika ziara hizo.
Aidha, Ruhwanya alihoji sababu za serikali kutumia gharama nyingi kwa ajili ya kazi hiyo badala ya fedha hizo kuzielekeza kwenye utekelezaji wa ahadi zake ili wananchi waone mafanikio.
Lakini katika jibu lake, Dk. Burian alibainisha kuwa serikali iliamua kuwatuma mawaziri mikoani ili kuhimiza halmashauri na madiwani kuimarisha usimamizi wa fedha za serikali zilizotengwa katika maeneo yao ili kuleta matokeo yaliyokusudiwa.
"Serikali imewataka wananchi watambue kuwa fedha za bajeti ni kodi zao, hivyo wasimamie matumizi yake ili zitumike vizuri kwa kazi zilizokusudiwa," alisema Dk. Burian na kuongeza kuwa kazi ya kutoa ufafanuzi huo isingeweza kuachwa kwa wabunge kwa kuzingatia kuwa hawana rasilimali za kutosha kuifanya kazi hiyo ipasavyo.
Jibu hilo lilimwamsha Benson Mpesya (Mbeya Mjini-CCM) aliyehoji iwapo serikali inalitambua hilo, kwa nini isiwaongeze wabunge uwezo ili waisaidie serikali katika kusimamia na kufuatilia matumizi ya fedha za bajeti.
Katika jibu la nyongeza, Dk. Burian alisema serikali itatekeleza hilo na kupitia sheria iliyopendekezwa na kuanzishwa kwa mfuko wa maendeleo ya jimbo, utakaowaongezea wabunge uwezo kirasilimali.