Millennium Goals Tanzania na Shillingi Yetu Kuporomoka

MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,919
3,206
Mh ndio ninavyoangalia shillingi inavyoporomoka na kimya kikuu cha serikali. Inaumiza zaidi serikali imejikita zaidi katika SIASA kuliko UCHUMI.

Akina BENNO NDULU na Mustapha Mkulo wako wapi?

Malengo ya millenia kwa Tanzania yatakamilika kwa kutegemea wawekezaji? Wawekezaji wenyewe wachakachuaji, wanakuja kuchuma na kusepa kwao.

Kwa nini serikali ya CCM haishauriki?? Hawataki hata kuitisha kongamano la wazawa wakajadili uchumi kuporomoka? Wanapiga propaganda tu kuwa uchumi unapanda wakati umasikini ukiwatafuna wananchi. Vijana wanahangaika na ajira wakati wao ccm wanapanga nani awe raisi 2015?

Hata Zambia wametupiku, Rwanda pamoja na VITA wametupiku, Sasa amani ya Tanzania inaimbwa kwa miaka 50 inafaida gani.

Igunga watu hawajui kusoma, wanakunywa maji kwenye mabwawa pamoja na wanyama. MMMHHHH

Nguvu kazi ya vijana inapotea, vijana hawana ajira, wawekezaji wanapora rasilimali zetu, je uchumi utakuwa, shillingi itaimarika???!!!

Hakika uchumi kuporomoka ni KiTanzi kwa ccm, amkeni acheni kukalia siasa jamani. kasi ya kuporomoka kwa shillingi ni kubwa jamani.

Ushauri wangu:
KILIMO KWANZA KIWE KWA WANANCHI WA TANZANIA.

NAPINGA KUITA WAWEKEZAJI NA KUWAPA ARDHI YETU KAMA ZAWADI.

WAWEKEZAJI WANAKUJA BILA HATA SHILLINGI MOJA, WANAPEWA ARDHI HALAFU WANATUMIA ARDHI YETU KUPATA MIKOPO.

HOW FO ..OL ARE WE TANZANIANS? SAMAHANI SIJATUKANA ILA NINASHANGAAAAAA

Kila nafasi nzuri tu ya uwekezaji tunaita wawekezaji, mtanzania akiomba ananyimwa au anawekewa mizengwe.

Angalia mashamba ya mpunga mbarali, amepewa mwekezaji halafu analima, anauza na faida anapeleka kwao nje. Je nani anajua analipa kodi kiasi gani.

NASHAURI TUSIKUBALI NGUVU KAZI YA VIJANA IENDELEE KUPOTEA.

YALE MASHAMBA YA NAFCO NA RANCH KIBAO ZIFANYIWE ASSESSMENT NA VIJANA WAPEWE.

LITOLEWE TANGAZO LA KUSEMA KILA KIJANA ANAYETAKA KULIMA KILIMO CHA BIASHARA AJIOREDHESHE, NA APEWE KIASI AMBACHO ATAMUDU KULIMA AU KUFUGA KIBIASHARA. NA HIVYO ATAZALISHA NA ATALIPA KODI SERIKALI.

WHY KILA KITU WAWEKEZAJI, KISA WANATOA 10%??? - TUACHE KUWAZIA TUMBO ZETU JAMANI, TUONEE HURUMA VIJANA WA TAIFA HILI.

VIJANA HAWA WAKIACHWA LITAKUWA BOMU AMBALO LIKILIPUKA, HAKUNA WA KUZUIA.

Wewe unaependa 10% - angalia na kesho, tosheka ili vijana wa wenzio nao wapate angalao.

Naomba wachangiaji wengine zaidi, ili tuangalie jinsi ya kuinua uchumi wa tanzania. tuokoe vijana

Tuache ushabiki wa kisiasa
 

Daniel Anderson

JF-Expert Member
Aug 7, 2011
872
140
Mkuu umewasilisha kwa uchungu sana. Ningesema mada hii ingewekwa jukwaa la siasa maana kuna wachangiaji wengi, lakini ingechukua sura ya kisiasa zaidi ikaacha ombwe la mawazo ya kiuchumi.
Umegusia sehemu fulani kuhusu uwekezaji. Hapo ndo penye tatizo kubwa. Serikali ilipaswa itoe hamasa kubwa sana kwa uwekezaji wa wazawa, inawezekana badala ya huu wa kigeni ambao unaruhusu capital outflow.
Tunapoteza fedha nyingi mno ikilinganishwa na tunazopata.
Naamini kama tungewekewa mazingira mujarab tungenunua wenyewe hata NAFCO na mengine mengi tu, tungeyaendeleza wenyewe na faida ingerudi humuhumu.
Kuhusu malengo ya milenia ni ndoto kuyafikia, ningeweza kutumia ripoti ya serikali kuthibitisha hili lakin kwa bahati mbaya natumia mobile.
Hata dira ya maendeleo ya taifa 2025 haitafikiwa abadan. Tulitakiwa tuwe tunakimbia lakin bado tunatambaa kwa sababu ya kukosa umakini wa kusimamia mambo yetu.
Hapa tusijadili kwa itikadi ya vyama, bali kwa mustakabali wa taifa. Nawasilisha.
 

MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,919
3,206
Asante sana Ndugu Andersonds,

Ukweli inashangaza sana, hata wachumi wetu tunao wategemea wako kimyaaa, sijui wameingia kwenye siasa au au wameamua kuweka akili pembeni.

Inasikitisha sana wachumi wetu wanaamua kuweka akili pembeni na kuacha liwalo na liwe.

Pia wataalamu wetu wizarani wanatumika zaidi kisiasa (wanatumika kama toilet paper). Mbaya zaidi wengi wa hawa wataamu wanatumika kupindisha ukweli na kupiga propaganda.

Ila ukweli ni kuwa watu wana hali mbaya sana, watu wanatozwa kodi nyingi halafu inatumika katika anasa za serikali kama kulipana posho.

Tuwekeze katika kilimo, wazawa wewezeshwe na mazao yasindikwe hapa tanzania. Tuachana na 10% za wawekezaji.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom