Titicomb
JF-Expert Member
- Jan 27, 2012
- 11,319
- 17,810
Well said mkuu. Couldn't add more. You have said it all.Ndugu yangu kama unataka kuelewa, majibu yote ya hoja zako yapo kwenye jibu langu la awali-labda kama hukusoma mpaka mwisho. Umekuja na hoja nyingine ya mpaper app, hiyo app ni ya nani? Inakuwezesha kusoma magazeti gani? Wamiliki wa hiyo app wana makubaliano gani na wamiliki wa magazeti? Kosa hata likifanywa na watu milioni haliwi halali.
Nitakujibu tena kuwa kisheria, haijarishi umecopy kiasi gani-ukikopi chapter moja au chapter zote bado ni kosa kisheria. Hivyo hoja kwamba anapiga picha kurasa za mbele tu haimfanyi asiwe na hatia. Hoja kwamba kupiga picha hamna tofauti na wale wanaotizama kibandani yanapouzwa magazeti-jibu ni kuna tofauti kama unafanya kwa lengo la kupata faida na Ayo anapata faida ya matangazo katika mtandao wake. Sheria ya hakimiliki ni kongwe sana, ilianza kutumika karne kadhaa zilizopita-haina utata kama unaousema. Wamiliki wa magazeti wana haki ndo maana Ayo ametii wito wao. Atatii pia hata wito wa kutopiga picha magazeti yao wakitaka.
Watanzania hatuna utamaduni wa kuheshimu intellectual property ndo maana unakuta mtu anauza nyimbo sehemu ya wazi na anatangaza (wale wanaotuwekea nyimbo kwenye simu, flash, CD, nk). Msanii anatoa pesa ili wimbom wake upigwe redion wakati ilibidi yeye ndo alipwe wimbo wake ukipigwa redion. Kuna watu wamekua maarufu sana kwa kutafsiri kwa kiswahili movie za kigeni na kila mtu anafurahia uvunjifu huo wa sheria miaka nenda rudi. Wote hao wanafanya makosa ikiwa hawakukubaliana na kuwalipa wamiliki halisi wa kazi zao. Mazoea sio sheria.