Millard Ayo achana na Clouds Media, Umekuwa mtumwa hata kwenye Kazi zako binafsi

LICHADI

JF-Expert Member
Feb 4, 2015
4,294
11,672
Millard Ayo ni moja kati ya vijana ambao wamefanya mapinduzi makubwa katika tasnia ya utangazaji na kuripoti habari mbali mbali mitandanoni hasa katika kampuni yake binafsi ya Ayo tv, Blog, kijana anajitahidi sana kuripoti matukio makubwa kwa haraka na yaliyo katika muonekano mzuri.

Lakini kitu kimoja kinachomuharibia ndugu yetu Ayo ni kuchanganya matakwa ya Clouds media na Media yake binafsi, Ayo ameshindwa kabisa kujiwekea misingi ya mipaka ya kazi zake binafsi na Masharti ya Clouds media.

Clouds ikiwa na mgogoro na mtu basi na yeye ni lazima ajiingize kwenye kazi zake binafsi.

Turudi kwa Lady jay dee, Millard hajawahi kuandika habari zake kabisa japo ugomvi wa jide na clouds ulikuwa haumhusu, Tukija kwa Wcb napo ni hivyo hivyo mgogoro wa Clouds na WCB, millard kauingiza hadi kwenye kazi zake binafsi yani huwezi kukuta millard akiripoti habari za wcb kama alivyo kuwa anafanya zamani.

USHAURI WANGU KWAKO MILLARD

jenga misingi ya kazi zako binafsi bila kuingiliwa na mtu yoyote, wewe sasa ni mtu mkubwa huhitaji tena kuendeshwa na muajiri wako Clouds, ni vyema kuliko kuendeshwa kwa misingi ya kuweka chuki kwa watu ambao wewe binafsi huna chuki nao, ni bora ujiendeshe mwenyewe ili usitumike katika migogoro ya watu wengine wakati wewe huusiki.

Muangalie kijana mwezako Sammisango katika blogs yake na tv online yake huwezi kukuta anambagua msanii au mtu yoyote kwenye kureport habari hata kama huyo mtu ana ugomvi na EATV, Yeye kajiwekea misingi yake binafsi haendeshwi na mwajiri wake, hata EATV wawe na bifu na mtu yeye haingizi hayo mambo anapokuwa kwenye kazi zake binafsi.

Millard ni bora uamue kuwa CEO wa kazi zako binafsi kuliko kuwa kibaraka wa mawingu hapo, jijengee misingi yako katika kazi zako binafsi zisiingiliwe na mtu hata awe mwajiri wako, unapoteza watazamaji na wasomaji wa blog yako kwa kubagua habari za kureport na kujiingiza katika migogoro isiyokuhusu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Clouds wamemtoa mbali alisema, so ana deni kwao hataki kuwaacha japo anaweza kuwa huru

Kabla blog yake haijawa maarufu alikuwa akiipigia promo ndani ya kipindi hapo clouds, jambo ambalo kwingine asingeruhusiwa.. Jamaa ana loyalty ya ajabu
 
Clouds wamemtoa mbali alisema, so ana deni kwao hataki kuwaacha japo anaweza kuwa huru

Kabla blog yake haijawa maarufu alikuwa akiipigia promo ndani ya kipindi hapo clouds, jambo ambalo kwingine asingeruhusiwa.. Jamaa ana loyalty ya ajabu

Nakuunga mkono, na nashauri aendelee hivyo hivyo. Sisi wenye marafiki wa dhati tunafahamu ni jinsi gani huwa tunawachukulia adui wa rafiki zetu, huwa ni zaidi ya yeye mwenyewe anavyomchukulia.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom