Military Intelligence Coup: Kisa cha rubani aliyeiba na kutoroka na Ndege ya Kijeshi ya Iraq

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Military Intelligence Coup: Kisa cha majasusi wa Mossad waliomhonga rubani aliyeiba na kutoroka na Ndege ya Kijeshi ya Iraq (Mikoyan-Gurevich MiG-21)

IMG_20180117_150710.jpg


Kuanzia mwaka 1952 mpaka mwaka 1963 Isser Harel alipata kuwa boss mkuu wa mashirika yote Shin Bet (idara ya usalama wa ndani ya nchi) pamoja na Mossad (idara ya ujasusi wa nje ya nchi).

Mwanzoni mwa mwaka 1963, alipata mbadala wake, aliyeitwa Meir Amit. Kwa siku za mwanzoni Meir Amit alikuwa hakubaliki sana na majasusi wa mossad waliokuwa watiifu kwa Harel, ila baada ya mwanzo mgumu, ulioanza kwa kukosa ushirikiano na uaminifu, alifanikiwa kujenga ushawishi katika uongozi wake ndani ya taasisi (MOSSAD)

Hata wale ambao hapo mwanzo walipinga kwa nguvu zote yeye kuwa boss mkuu wa mossad akichukua nafasi ya Harel walianza kumuheshimu, kumkubali na kumpenda. Meir Amit alifanikiwa kuja kuwa boss mahiri wa operations zote za mossad nje ya nchi.

Chini ya uongozi wake pamoja na boss wa kitengo cha ujasusi cha jeshi Aharon Yariv kwenye miaka ya 1960's, idara za ujasusi za Israel zilipata mafanikio makubwa sana na ya kukumbukwa. Moja kati ya mafanikio haya ilikuwa ni ushindi wa Vita ya siku sita mnamo mwezi wa juni mwaka 1967 pamoja na wizi wa ndege za kivita iliyotengenezwa nchini Soviet Mig-21.

Punde tu baada ya kutwaa u boss wa mossad mwaka 1963, Meir Amit aliomba ushauri wa mawazo kutoka kwa viongozi wa ngazi za juu wa kijeshi ili kuweza kumsaidia kuunda malengo makuu ya mossad, na kuwauliza ni yapi wanahisi mossad inaweza kuchangia katika ulinzi wa taifa la Israel.

Jenerali Mordecai (Motti) kamanda wa kikosi cha anga cha jeshi la Israel mwaka 1963 alimwambia afanye juu chini wailete ndege ya kisasa kwa wakati huo (Mig-21) katika ardi ya Israel.

Ni ngumu sana kufahamu kama Motti aliamini kuwa mission kama hiyo inaweza kutekelezeka. Ezer Weizmann, ambaye alikuja kuwa kamanda wa jeshi la anga kutoka kwa Hod, alipata kumwambia Hamit kitu hicho hicho punde tu kabla ya vita ile ya siku sita. Kama ingewezekana.

MKASA SASA NDIO UNAANZA

Mikoyan - Guverich almaarufu kama Mig-21 ni moja kati ya ndege za kisasa zaidi zinazokimbia kwa kasi kuzidi sauti kuruka kutoka nje ya anga la USSR. Bado inashikilia rekodi ya kuwa ndege iliyotengenezwa kwa wingi zaidi katika historia ya tasnia ya uundaji wa ndege za kasi, na imetumiwa na takribani nchi 60 na katika mabara manne.

Sifa kubwa ya ndege hii ni kwamba ilikuwa na uwezo wa kubebeshwa makombora mazito na ya masafa marefu.

Kati kati ya miaka ya 1960, Mig 21 ilitumiwa kwa wingi sana na nchi za mashariki ya kati katika mogogoro yao. Vikosi vya anga vya nchi kama Misri, Syria pamoja na Iraq walitumia saaanaa ndege hizi hususan kwa mashambulizi dhidi ya wayahudi.

Kwa kipindi cha muda mrefu sana jeshi la anga la Israel lilipambana kupata kwa kuiba ndege hii ya Mig 21 ili kuweza kudadavua uwezo wake katika uwanja wa vita pamoja na udhaifu wake pamoja na kupata kujua ni mbinu gani hutumika na majeshi ya adui katika kupambana wakiwa na ndege ya aina hii.

Idara ya ujasusi ya taifa hilo la kiyahudi (mossad) walipewa jukumu zito sana la kuipata ndege hiyo kwa udi na uvumba katika mpango wa siri sana uliojulikana kama "operation diamond"

Katika jaribio lake la kwanza, jasusi wa mossad aliyejulikana kama Jean Thomas aliyeishi nchini Misri alipokea amri ya kutafuta rubai ambaye angekuwa tayari kutoroka na ndege na kuipeleka Israel kwa kuhongwa kiasi cha pesa cha karibia dola milioni moja za wakati huo mwaka 1966.

Mission hii haikufanikiwa kwa vile rubani yule wa ndege za jeshi la anga la misri alitoa taarifa mapema kwa vyombo vya usalama vya nchi yake mpaka ikapelekea Thomas kukamatwa na kushitakiwa kwa makosa ya kufanya upelelezi ndani ya ardhi ya Misri.

Jaribio la pili la kuiba ndege hiyo ya Mig 21 kwa safari hii lilifanyika nchini Iraq lakini pia halikufanikiwa kwa sababu mpelelezi wa mossad aliishia kupigana na marubani wawili wa jeshi la anga la Iraq wakati akijaribu kuwanyamazisha baada ya kuwa walikwisha kataa kutoa ushirikiano wa dhati katika mpango huo.

Mnamo mwaka 1964, taarifa zilipatikana kutoka kwa mjahudi mzaliwa wa Iraq zilizopelekea mossad kufahamiana na rubani aliyejulikana kama Munir Redfa ambaye alikuwa akichukizwa na ukweli kwamba yeye kuwa na background ya ukristo ndio kunakofanya washindwe kumpandhisha cheo katika jeshi la Iraq. Serikali ya Israel ilimpa redfa kiasi kikubwa sana cha pesa, uraia wa Israel kwake pamoja na familia yake pamoja na ajira ya kudumu.

Katika mkutano wa siri baina yake na maofisa wa kiyahudi uliofanyia ulaya, walipanga mikakati madhubuti ikiwa pamoja na kwenda Israel kutembelea uwanja wa ndege wa kijeshi ambao engetumika kutua ndege hiyo ya wizi.

Ilipokika tarehe 16 August mwaka 1966, Redfa alipata fursa ya kutoroka na ndege alikwa katika mazoezi ya kawaida ya kuruka, ndege ikiwa ipo na mafuta full tank jambo ambalo ilikuwa hairuhusiwi kwa ndege kujazwa mafuta fully ikiwa katika mafunzo.

Ndege ilipita kaskazini mwa Jordan ikiwa katika kasi ya ajabu. Redfa alitoka kutoka katika njia kuu ya ndege kama ilivyopangwa katika mazoezi. Ndege mbili za jeshi la Jordan ziliruka kuifuata Mig 21 ambao ilikuwa ikiruka katika speed ya ajabu tena juu kabisaaa kama futi 30,000 kiasi kwamba kuikamata kwa ndege za Jordan ikawa haiwezekani.

Makombora ya kutungulia ndege ya Jordan yote yalizimwa kisha Mig 21 ikavuka anga la Jordan bila utata wowote.

Ndege hii ya wizi ilipokuwa inakaribia kuingia katika anga la Israel, ilipokelewa na ndege ndogo mbili. Ndogo lakini zilikuwa na nguvu kubwa sana aina ya Mirage III za jeshi ya Israel ambazo ziliaindikiza mgeni wao kwa utaratibu kabisaa mpaka katika uwanja wa ndege za kijeshi wa Hatzor.

Baadaye sana rubani mwizi Redfa alikuwa kisema hadharani kuwa alitua na ndege ikiwa na mafuta kidogo sana sana sanaaaa.

Kuibwa kwa ndege ile kulizua mijadala dunia nzima (mpaka Tanzania) huku serikali za Urusi pamoja na Iraq wakitaka ndege hiyo kurudishwa mara moja. Serikali ya Israel walikataa kata kata agizo hilo la kurudhisha ndege.

Ndani ya wiki chache ndege hiyo ilirushwa tena angani katika mazoezi ya kijeshi ili kuipiganisha na ndege ya jeshi la Israel aina ya Mirage III, pamoja na kuwafunza marubani wa IDF namna ya kupambana na ndege za waarabu aina hiyo hiyo ya Mig 21 wakati wa Vita.

Wakaja kugundua kwamba Mig ilikuwa ni ndege nzuri sana katika mapambano ya anga za juu sana pia ni rahisi sana kuirusha angani. Pia wakaja kugundua baadhi ya madhaifu ya ndege ile.

Mig 21 ikaja kupakwa rangi ya mistari miekundu pembeni mwake ili waitofautishe na ndege za adui wakati wa mapambano na ikaja kitumika wakati wa vita vya siku sita kati ya Israel na mataifa ya kiarabu.

Baadaye pia ndege ikaja kuvunjwa vunjwa na kumong'onyolewa yooote kisha kufanyiwa analysis ya kina zaidi.

Tukio hili lilionekana ndio la mafanikio zaidi kwa mossad kwa vile walifanikiwa kuvunjavunja ndege sita za maadui aina ya Mig wakati wa Vita na Syria wakati ndege yao aina ya Mirage III ikitoka bila kuchubuka hata kidogo.

Israel wakaja wakaipeleka ndege ile marekani mwaka 1968 jambo ambalo lilipelekea marekani kuwapa Israel ndege mpya na ya kisasa aina ya Douglas F-4 Phantom.

***MWISHO WA MKASA HUU WA KIJESHI***

USISAHAU:
ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
View attachment 677885

Kuanzia mwaka 1952 mpaka mwaka 1963 Isser Harel alipata kuwa boss mkuu wa mashirika yote Shin Bet (idara ya usalama wa ndani ya nchi) pamoja na Mossad (idara ya ujasusi wa nje ya nchi). Mwanzoni mwa mwaka 1963, alipata mbadala wake, aliyeitwa Meir Amit. Kwa siku za mwanzoni Meir Amit alikuwa hakubaliki sana na majasusi wa mossad waliokuwa watiifu kwa Harel, ila baada ya mwanzo mgumu, ulioanza kwa kukosa ushirikiano na uaminifu, alifanikiwa kujenga ushawishi katika uongozi wake ndani ya taasisi (MOSSAD)

Hata wale ambao hapo mwanzo walipinga kwa nguvu zote yeye kuwa boss mkuu wa mossad akichukua nafasi ya Harel walianza kumuheshimu, kumkubali na kumpenda. Meir Amit alifanikiwa kuja kuwa boss mahiri wa operations zote za mossad nje ya nchi. Chini ya uongozi wake pamoja na boss wa kitengo cha ujasusi cha jeshi Aharon Yariv kwenye miaka ya 1960's, idara za ujasusi za Israel zilipata mafanikio makubwa sana na ya kukumbukwa. Moja kati ya mafanikio haya ilikuwa ni ushindi wa Vita ya siku sita mnamo mwezi wa juni mwaka 1967 pamoja na wizi wa ndege za kivita iliyotengenezwa nchini Soviet Mig-21. Punde tu baada ya kutwaa u boss wa mossad mwaka 1963, Meir Amit aliomba ushauri wa mawazo kutoka kwa viongozi wa ngazi za juu wa kijeshi ili kuweza kumsaidia kuunda malengo makuu ya mossad, na kuwauliza ni yapi wanahisi mossad inaweza kuchangia katika ulinzi wa taifa la Israel. Jenerali Mordecai (Motti) kamanda wa kikosi cha anga cha jeshi la Israel mwaka 1963 alimwambia afanye juu chini wailete ndege ya kisasa kwa wakati huo (Mig-21) katika ardi ya Israel.

Ni ngumu sana kufahamu kama Motti aliamini kuwa mission kama hiyo inaweza kutekelezeka. Ezer Weizmann, ambaye alikuja kuwa kamanda wa jeshi la anga kutoka kwa Hod, alipata kumwambia Hamit kitu hicho hicho punde tu kabla ya vita ile ya siku sita. Kama ingewezekana
========
Mkasa ndio unaanza sasa.......
Mikoyan - Guverich almaarufu kama Mig-21 ni moja kati ya ndege za kisasa zaidi zinazokimbia kwa kasi kuzidi sauti kuruka kutoka nje ya anga la USSR. Bado inashikilia rekodi ya kuwa ndege iliyotengenezwa kwa wingi zaidi katika historia ya tasnia ya uundaji wa ndege za kasi, na imetumiwa na takribani nchi 60 na katika mabara manne. Sifa kubwa ya ndege hii ni kwamba ilikuwa na uwezo wa kubebeshwa makombora mazito na ya masafa marefu.

Kati kati ya miaka ya 1960, Mig 21 ilitumiwa kwa wingi sana na nchi za mashariki ya kati katika mogogoro yao. Vikosi vya anga vya nchi kama Misri, Syria pamoja na Iraq walitumia saaanaa ndege hizi hususan kwa mashambulizi dhidi ya wayahudi.

Kwa kipindi cha muda mrefu sana jeshi la anga la Israel lilipambana kupata kwa kuiba ndege hii ya Mig 21 ili kuweza kudadavua uwezo wake katika uwanja wa vita pamoja na udhaifu wake pamoja na kupata kujua ni mbinu gani hutumika na majeshi ya adui katika kupambana wakiwa na ndege ya aina hii.

Idara ya ujasusi ya taifa hilo la kiyahudi (mossad) walipewa jukumu zito sana la kuipata ndege hiyo kwa udi na uvumba katika mpango wa siri sana uliojulikana kama "operation diamond"

Katika jaribio lake la kwanza, jasusi wa mossad aliyejulikana kama Jean Thomas aliyeishi nchini Misri alipokea amri ya kutafuta rubai ambaye angekuwa tayari kutoroka na ndege na kuipeleka Israel kwa kuhongwa kiasi cha pesa cha karibia dola milioni moja za wakati huo mwaka 1966. Mission hii haikufanikiwa kwa vile rubani yule wa ndege za jeshi la anga la misri alitoa taarifa mapema kwa vyombo vya usalama vya nchi yake mpaka ikapelekea Thomas kukamatwa na kushitakiwa kwa makosa ya kufanya upelelezi ndani ya ardhi ya Misri.

Jaribio la pili la kuiba ndege hiyo ya Mig 21 kwa safari hii lilifanyika nchini Iraq lakini pia halikufanikiwa kwa sababu mpelelezi wa mossad aliishia kupigana na marubani wawili wa jeshi la anga la Iraq wakati akijaribu kuwanyamazisha baada ya kuwa walikwisha kataa kutoa ushirikiano wa dhati katika mpango huo.

Mnamo mwaka 1964, taarifa zilipatikana kutoka kwa mjahudi mzaliwa wa Iraq zilizopelekea mossad kufahamiana na rubani aliyejulikana kama Munir Redfa ambaye alikuwa akichukizwa na ukweli kwamba yeye kuwa na background ya ukristo ndio kunakofanya washindwe kumpandhisha cheo katika jeshi la Iraq. Serikali ya Israel ilimpa redfa kiasi kikubwa sana cha pesa, uraia wa Israel kwake pamoja na familia yake pamoja na ajira ya kudumu.

Katika mkutano wa siri baina yake na maofisa wa kiyahudi uliofanyia ulaya, walipanga mikakati madhubuti ikiwa pamoja na kwenda Israel kutembelea uwanja wa ndege wa kijeshi ambao engetumika kutua ndege hiyo ya wizi.

Ilipokika tarehe 16 August mwaka 1966, Redfa alipata fursa ya kutoroka na ndege alikwa katika mazoezi ya kawaida ya kuruka, ndege ikiwa ipo na mafuta full tank jambo ambalo ilikuwa hairuhusiwi kwa ndege kujazwa mafuta fully ikiwa katika mafunzo. Ndege ilipita kaskazini mwa Jordan ikiwa katika kasi ya ajabu. Redfa alitoka kutoka katika njia kuu ya ndege kama ilivyopangwa katika mazoezi. Ndege mbili za jeshi la Jordan ziliruka kuifuata Mig 21 ambao ilikuwa ikiruka katika speed ya ajabu tena juu kabisaaa kama futi 30,000 kiasi kwamba kuikamata kwa ndege za Jordan ikawa haiwezekani. Makombora ya kutungulia ndege ya Jordan yote yalizimwa kisha Mig 21 ikavuka anga la Jordan bila utata wowote.

Ndege hii ya wizi ilipokuwa inakaribia kuingia katika anga la Israel, ilipokelewa na ndege ndogo mbili. Ndogo lakini zilikuwa na nguvu kubwa sana aina ya Mirage III za jeshi ya Israel ambazo ziliaindikiza mgeni wao kwa utaratibu kabisaa mpaka katika uwanja wa ndege za kijeshi wa Hatzor. Baadaye sana rubani mwizi Redfa alikuwa kisema hadharani kuwa alitua na ndege ikiwa na mafuta kidogo sana sana sanaaaa.

Kuibwa kwa ndege ile kulizua mijadala dunia nzima (mpaka Tanzania) huku serikali za Urusi pamoja na Iraq wakitaka ndege hiyo kurudishwa mara moja. Serikali ya Israel walikataa kata kata agizo hilo la kurudhisha ndege. Ndani ya wiki chache ndege hiyo ilirushwa tena angani katika mazoezi ya kijeshi ili kuipiganisha na ndege ya jeshi la Israel aina ya Mirage III, pamoja na kuwafunza marubani wa IDF namna ya kupambana na ndege za waarabu aina hiyo hiyo ya Mig 21 wakati wa Vita. Wakaja kugundua kwamba Mig ilikuwa ni ndege nzuri sana katika mapambano ya anga za juu sana pia ni rahisi sana kuirusha angani. Pia wakaja kugundua baadhi ya madhaifu ya ndege ile. Mig 21 ikaja kupakwa rangi ya mistari miekundu pembeni mwake ili waitofautishe na ndege za adui wakati wa mapambano na ikaja kitumika wakati wa vita vya siku sita kati ya Israel na mataifa ya kiarabu.

Baadaye pia ndege ikaja kuvunjwa vunjwa na kumong'onyolewa yooote kisha kufanyiwa analysis ya kina zaidi.

Tukio hili lilionekana ndio la mafanikio zaidi kwa mossad kwa vile walifanikiwa kuvunjavunja ndege sita za maadui aina ya Mig wakati wa Vita na Syria wakati ndege yao aina ya Mirage III ikitoka bila kuchubuka hata kidogo.

Israel wakaja wakaipeleka ndege ile marekani mwaka 1968 jambo ambalo lilipelekea marekani kuwapa Israel ndege mpya na ya kisasa aina ya Douglas F-4 Phantom.
=========
Mkuu hongera sana
 
Back
Top Bottom