Milipuko ya Gongo la Mboto: Kikwete aipa pole na kuipongeza JWTZ kwa kazi nzuri! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Milipuko ya Gongo la Mboto: Kikwete aipa pole na kuipongeza JWTZ kwa kazi nzuri!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Fareed, Feb 18, 2011.

 1. F

  Fareed JF-Expert Member

  #1
  Feb 18, 2011
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ifuatayo ni taarifa ya Rais Jakaya Kikwete kuhusu mlipuko wa Gongo la Mboto. Ukiisoma kwa makini, unaona kuwa msisitizo wa Rais ni kutoa POLE na PONGEZI kwa JWTZ. Rais haoneshi kushtushwa, kukerwa au kukasirika kuwa mlipuko huu umetokea mwaka mmoja tu baada ya mlipuko wa Mbagala uliouwa watu 26 na kujeruhi 700. Hakuna reference ya mlipuko wa Mbagala na kuwa serikali na jeshi wameshindwa kujifunza kutokana na mlipuko wa Mbagala. Badala yake sasa anazungumzia serikali kuomba msaada wa China, Marekani, Ujerumani, etc kuchunguza chanzo cha mlipuko na jinsi ya kuepuka kwa siku zijazo.

  Anajidai eti serikali itagharamia mazishi na kuwalipa watu fidia kwa mali zao na vifo, vilema walivyopata. How much does a human life or limb cost?

  Kweli Rais tunaye!

  Rais makini angemtaka Waziri wa Ulinzi, Hussein Mwinyi, na Chief of Staff wa JWTZ, Abdulrahman Shimbo, wajiuzulu kwa uzembe mkubwa au kama ishara ya uwajibikaji. Tunajua hawezi kuwachukulia hatua yoyote hawa kwani ni maswahiba wake. Katika mipango yake, Shimbo ndiyo CDF ajaye na Mwinyi Rais wa kumrithi (chaguo lake la 3) iwapo Edward Lowassa (chaguo la JK la kwanza) na Bernard Membe (chaguo la JK la 2) watakwama.

  JK amemuweka kando Chief of Defence Forces (CDF), General Davis Mwamunyange, siku nyingi na huwa ana deal na Shimbo tu kama de facto CDF. Hivyo Mwamunyange hana kosa kwani ameshajichokea na yuko kwenye a prolonged unofficial leave kwa muda mrefu sasa.  [FONT=&quot]TAARIFA MAALUM KUHUSU MAAFA YA GONGOLAMBOTO[/FONT]
  [FONT=&quot]Ndugu Wananchi,[/FONT]
  [FONT=&quot] Kama mjuavyo, jana usiku jiji la Dar es Salaam lilipata mtikisiko mkubwa kutokana na milipuko ya mabomu iliyokuwa inatokea katika ghala kuu la Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania lililoko Gongolamboto katika viunga vya Dar es Salaam.[/FONT]
  [FONT=&quot] Milipuko hiyo imesababisha maghala 23 kuteketea kabisa na majengo kadhaa ya shughuli mbalimbali hapo kikosini kuharibika kwa viwango mbalimbali. Mabweni mawili ya kuishi wanajeshi nayo yaliteketea. Aidha, risasi nyingi, mabomu mengi, silaha na magari kadhaa nayo yameharibiwa na mengine kuteketea. Jeshi letu na nchi yetu imepata hasara kubwa sana.[/FONT]
  [FONT=&quot] Katika maafa haya makubwa kwa taifa letu, raia nao wameathirika kwa namna mbalimbali. Nyumba kadhaa za kuishi na majengo ya huduma za jamii nayo yameharibiwa na mabomu yaliyoangukia humo. Zipo ambazo zimeungua kabisa na zipo zilizopata uharibifu mkubwa na zipo zilizopata uharibifu wa viwango vya chini.[/FONT]
  [FONT=&quot] Lakini baya zaidi, katika mlipuko huo, ndugu zetu 20 wamepoteza maisha na wengine zaidi wamejeruhiwa kwa aina na viwango mbalimbali. Baadhi yao walifika katika hospitali za Amana, Temeke na Muhimbili na kupatiwa matibabu. Wengine wameruhusiwa na wengine wapatao 135 bado wamelazwa. Idadi kamili hupanda na kushuka kutegemea na kupokelewa na kuruhusiwa kwa majeruhi.[/FONT]
  [FONT=&quot]Ndugu Wananchi,[/FONT]
  [FONT=&quot] Hakika taifa limepata hasara kubwa kwa ndugu zetu kufariki na kujeruhiwa. Napenda kutumia nafasi hii kwa uchungu mkubwa kuelezea masikitiko yangu na taifa kwa ndugu zetu waliopoteza maisha wakati ambapo taifa lilikuwa bado linauhitaji sana mchango wao.[/FONT]
  [FONT=&quot] Naomba ndugu wa marehemu wapokee mkono wa rambirambi kutoka kwangu na kupitia kwangu kutoka kwa Watanzania wenzetu wote. Tuwaombee kwa Mwenyezi Mungu marehemu wetu wapate mapumziko mema. Amin. [/FONT]
  [FONT=&quot] Aidha, kwa niaba yangu na ya Watanzania wenzangu wote, nawapa pole nyingi ndugu zetu wote waliojeruhiwa na kupata mshituko kutokana na milipuko ya mabomu iliyotokea jana usiku. Tunazidi kuwaombea wapone upesi ili waendelee na kazi zao za kujenga taifa pamoja na kujiletea maendeleo yao binafsi.[/FONT]
  [FONT=&quot] Leo asubuhi na baadae mchana nilitembelea eneo la tukio kule Gongolamboto na kuwatembelea wagonjwa katika hospitali za Amana, Temeke na Muhimbili. Nimeona madhara na hasara tuliyoipata pale Gongolamboto. Nimewaona na kuwafariji wagonjwa wetu. Nimezungumza na madaktari na wauguzi katika hospitali hizo. Nimewashukuru na kuwapongeza kwa kazi kubwa na nzuri waliyoifanya usiku kucha ya kuwahudumia na kuokoa maisha ya ndugu zetu hao. Nimewatia moyo na kuwataka waendelee kuwahudumia vyema.[/FONT]
  [FONT=&quot]Ndugu Wananchi,[/FONT]
  [FONT=&quot] Napenda pia kutumia nafasi hii kuwapongeza viongozi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na wa Bohari Kuu ya Madawa kwa kuhakikisha kuwa dawa na vifaa vya tiba vinapatikana kwa urahisi na kwa wakati, Hali hiyo ndiyo iliyosaidia kuokoa maisha na kuwapunguzia machugu ndugu zetu waliojeruhiwa.[/FONT]
  [FONT=&quot]Baraza la Usalama[/FONT]
  [FONT=&quot]Ndugu Wananchi,[/FONT]
  [FONT=&quot] Leo alasiri mpaka usiku huu, tulikuwa na mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Taifa. Hiki ndicho chombo cha juu cha kumshauri Rais kuhusu masuala yahusuyo usalama wa taifa letu. Kwa uzito na unyeti wa tukio, niliamua kuitisha mkutano wa Baraza hilo mara baada ya maafa hayo kutokea.[/FONT]
  [FONT=&quot] Katika mkutano wetu, tumelitafakari kwa kina tukio hili na mambo mbalimbali yanayotokana na kuhusiana nalo. Baraza limeazimia kama ifuatavyo:[/FONT]
  [FONT=&quot]1. [/FONT][FONT=&quot]Tumesikitishwa sana na tukio hili na hasa vifo vilivyotokea na majeraha yaliyowapata ndugu zetu wengi. Baraza limetoa rambirambi kwa ndugu na jamaa wa marehemu. Aidha, tunawapa pole wale wote waliojeruhiwa na kuwaombea kwa Mola wapone upesi.[/FONT]

  [FONT=&quot]2. [/FONT][FONT=&quot]Kuhusu waliopoteza maisha, tumeamua kuwa, Serikali igharamie mazishi ya marehemu wetu hao popote ndugu watakapoamua wakazikwe. Baadae ndugu wa marehemu wapewe kifuta machozi.[/FONT]

  [FONT=&quot]3. [/FONT][FONT=&quot]Kuhusu waliojeruhiwa tumeamua kuwa Serikali igharamie matibabu yao. Baadae watakapotoka hospitali walipwe kifuta machozi kwa ulemavu walioupata.[/FONT]

  [FONT=&quot]4. [/FONT][FONT=&quot]Kamati ya Maafa ya Mkoa imeagizwa kushirikiana na Kitengo cha Maafa cha Taifa kilichopo Ofisi ya Waziri Mkuu kuwahudumia wananchi waliopoteza makazi yao au waliolazimika kuyakimbia makazi yao kwa nia ya kuokoa maisha yao. Ihakikishwe kuwa kwa haraka wanapatiwa makazi ya muda pamoja na huduma za malazi, chakula, maji, afya na usafi wa mazingira.[/FONT]

  [FONT=&quot]5. [/FONT][FONT=&quot]Aidha, Kamati ya Maafa ya Mkoa imeelekezwa kutengeneza taratibu nzuri zitakazohakikisha kuwa mapema iwezekanavyo, wananchi hao wanarejea makwao ili waendelee na shughuli zao za kawaida hasa sasa ambapo hatari ya milipuko katika maghala ya Gongolamboto haipo tena.[/FONT]

  [FONT=&quot]6. [/FONT][FONT=&quot]Baraza la Usalama limelipongeza Jeshi la Ulinzi kwa uamuzi wake wa haraka wa kuwatuma wahandisi wa medani kufanya kazi ya kutafuta, kutambua na kuyakusanya mabomu yote yaliyoangukia katika maeneo ya raia kwa nia ya baadae kuyaharibu.[/FONT]

  [FONT=&quot]7. [/FONT][FONT=&quot]Tunawaomba wananchi watoe ushirikiano wa hali ya juu kwa Jeshi kwa kuwapa taarifa wanapoyaona mabomu katika maeneo yo yote. Na, jambo kubwa zaidi tunawakumbusha wananchi kutii maelekezo ya Jeshi ya kutokuyagusa au kuchezea mabomu au hata vipande vipande vya mabomu vilivyodondoka katika maeneo yao.[/FONT]

  [FONT=&quot]8. [/FONT][FONT=&quot]Baraza la Usalama la Taifa, limeagiza Kamati ya Maafa ya Mkoa wa Dar es Salaam na Kitengo cha Maafa cha Taifa wazitambue mapema iwezekanavyo nyumba zilizoharibiwa, wenye nyumba na kuhakikisha kuwa matayarisho husika yanafanyika ikiwa ni pamoja na uthamini ili walipwe fidia wanayostahili bila kuchelewa.[/FONT]

  [FONT=&quot]9. [/FONT][FONT=&quot]Vile vile Kamati ya Maafa ya Mkoa imeagizwa kufanya yafuatayo:[/FONT]

  [FONT=&quot](a) [/FONT][FONT=&quot]Kushirikiana na Jeshi la Polisi kuwatafuta watoto waliopotea na kuwaunganisha na familia zao.[/FONT]

  [FONT=&quot](b) [/FONT][FONT=&quot]Kuongoza, kuratibu na kusimamia utekelezaji wa masuala yote yahusuyo waliofariki, waliojeruhiwa na waliohama makazi yao, na huduma zao stahiki.[/FONT]

  [FONT=&quot]10. [/FONT][FONT=&quot] Baraza la Usalama limetoa pole nyingi kwa Mkuu wa Majeshi, Maafisa na Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kwa maafa makubwa yaliyowakuta na hasara waliyoipata kwa milipuko ya mabomu iliyotokea katika Ghala Kuu la Jeshi, Gongolamboto.[/FONT]

  [FONT=&quot]11. [/FONT]
  [FONT=&quot]Baraza pia limelipongeza Jeshi kwa juhudi kubwa ilizofanya kuzima moto huo, hivyo kuweza kunusuru baadhi ya maghala, zana na vifaa vingine visiteketezwe na moto.[/FONT]

  [FONT=&quot]12. [/FONT][FONT=&quot]Baraza limeagiza Jeshi lifanye uchunguzi wake wa ndani wa chanzo cha tukio hili kama Sheria ya Ulinzi wa Taifa inavyoagiza. Aidha, imetaka vyombo vingine vya ulinzi na usalama visaidie katika uchunguzi huo.[/FONT]

  [FONT=&quot]13. [/FONT][FONT=&quot]Baraza la Usalama limeamua kuwa, Serikali ya Tanzania iombe nchi rafiki zisaidie katika uchunguzi wa chanzo cha tukio hili na kushauri namna bora zaidi ya kuimarisha usalama na uhifadhi wa mabomu na risasi katika maghala ya Jeshi letu kote nchini.[/FONT]

  [FONT=&quot]14. [/FONT][FONT=&quot]Mwisho, Baraza la Usalama wa Taifa linawaomba wananchi waliohama warejee kwenye makazo yao kwani kipindi cha hatari ya mabomu kulipuka kimekwishapita. Tunaomba na kusisitiza wajiepushe kuchezea mabomu yaliyodondoka katika maeneo yao ambayo bado hayajaondolewa.[/FONT]


  [FONT=&quot]Ndugu Wananchi Wenzangu;[/FONT]
  [FONT=&quot]Hili ni janga ambalo pamoja na kusikitisha linaleta uchungu hasa pale inapotokea miaka miwili tu baada ya janga la Mbagala. Machungu yenu ndiyo machungu yangu na ndiyo ya viongozi wote Wakuu wa Nchi yetu ambao ndiyo Wajumbe wa Baraza la Usalama la Taifa. Naomba tuwe watulivu katika wakati huu mgumu. [/FONT]
  [FONT=&quot]Napenda kuwahakikishia kuwa tumeamua kulishughulikia tatizo lenyewe na athari zake sasa na siku za usoni kwa uthabiti mkubwa. Naomba tuendelee kuwa na imani na Jeshi letu, viongozi wake na wanajeshi wetu wote. Tuwaunge mkono na kuwapa ushirikiano sasa na siku za usoni.[/FONT]

  [FONT=&quot]Mungu Ibariki Afrika![/FONT]
  [FONT=&quot]Mungu Ibariki Tanzania![/FONT]
  [FONT=&quot]Asanteni kwa kunisikiliza.[/FONT]
   
 2. HekimaMoyoni

  HekimaMoyoni Member

  #2
  Feb 18, 2011
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aibu kubwa kwa Raisi kama amiri jeshi Mkuu, Jeshi na baraza la usalama kwa ujumla...
  Mimi sioni kama tuna Rais hapa....Kuna haja ya wananchi kwa ujumla wetu kwenda pale ikulu kudai funguo yetu maana yule kilaza hastahili kuishi pale kwa ridhaa ya wananchi anaowateketeza kwa mabomu...
   
 3. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #3
  Feb 18, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Katika taarifa ya habari kupitia Channel Ten jana saa 1 jioni, JK alionyeshwa akiwatembelea wahanga wa mabomu ya Gongo la Mboto akimshobokea mtoto aliekuwa akilishwa chakula na mama yake, alipofika JK mahali hapo alichukua kijiko alichokuwa anatumia mama wa mtoto kumlisha na kuchota chakula ili kumlisha yule mtoto, Mtoto alimtolea nje, huku akitikisa kichwa...Niliipenda sana kwani niliona ilikuwa na ujumbe tosha kuwa wewe msanii usinizoee
   
 4. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #4
  Feb 18, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Kwani mlitegemea kitu gani kipya? Kuna watu na Viatu duniani!
   
 5. F

  FUSO JF-Expert Member

  #5
  Feb 18, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,834
  Likes Received: 2,306
  Trophy Points: 280
  Nani anajua wajumbe wa balaza la usalama la taifa? usije ukashangaa ni wale wale kina Chiligatti / Makamba n.k...

  hawa ndiyo wanabeba usalama wa maisha yetu wakuu - je tukae na tuwaamini na kuwakabidhi maisha yetu?
   
 6. HISIA KALI

  HISIA KALI JF-Expert Member

  #6
  Feb 18, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 694
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Najua una uchungu sana na hili janga. Ila napenda tu kukujulisha kuwa taarifa hii imefanya reference ya tukio la Mbagala. Soma mwisho wa Taarifa. Soma RED tu kama una muda.
   
 7. CPU

  CPU JF Gold Member

  #7
  Feb 18, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Full HONGERA, PONGEZI NA POLE kwa JWTZ na Wizara :A S 13::A S 13::A S 13::A S 13:
  Kifuta jasho/machozi kwa wafiwa na walemavu :A S 13::A S 13::A S 13::A S 13:

  Sasa naamini uwepo wa Freemasons members
   
 8. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #8
  Feb 18, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Anawapongeza JWTZ:A S 13::A S 13: nimekatika mkono na mguu kifuta jasho kitanisaidia nini? Kitarudisha mkono na mguu wangu vilivyokatika?Hizi :blah::blah::blah::blah::blah: ndizo wanazojua badala ya kuwajibika na kujiuzulu nyambaffff kabisa
   
 9. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #9
  Feb 18, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145

  Hongera Mheshimiwa Rais unastahili kupongezwa kwa taarifa nzuri kama hii,

  Mambo uliyoyaorodhesha ni dhahiri yanaingia akilini na yana nia kuleta nafuu kwa wananchi.

  Nakuunga mkono katika mambo yafuatayo:-
  a. Kuwasaidia ndugu na jamaa wa marehemu gharama za mazishi (Kwani wao ni walipa kodi wa serikali ).

  b. Kuwalipa fidia au sijui ndio kifuta jasho kwa hasara waliyoipata (Ingawa mie ningelishauri wajengewe nyumba zao kuepusha matapeli wengine kuongeza bei za nyumba zao kwa nia kufaidika umakini unahitajika sana hapa).

  c. Kugharamia matibabu ya ndugu zetu walioathirika na ajali hiyo.


  Kuna mapungufu mawili au matatu nayoyaona ambayo binafsi yanafaa yafanyiwe kazi:-
  a. Report ya tume ya mwinyi mbagala ingelifaa tujulishwe kwani kosa ni mara moja kurudi kosa sio kosa bali ni ila hujuma au uzembe umefanyika tunaomba taarifa ile ya mbagala tupewe ili tujue kinachoendelea.

  b. Pia hujatuambia preliminary report ya Gongo la Mboto inasemaje kuhusu chanzo cha moto na mlipuko ili tuwe na imani ya kuwa hali ni salama watu wapate kurejea kwao.

  c.Kwa wale waliofariki kifuta jasho kikubwa wanachoweza kusaidiwa ni mazingira ya kuwezeshwa kuanza kumudu kimaisha pindi huruma za watanzania zitakapoisha na watu kuanza kurudi katika maisha yao ya zamani.

  d. Vilevile ikija kufahamika ni uzembe au hujuma ni hatua gani umekusudia kuzichukua kuwawajibisha wale waliokuwa wamefanya uzembe huo au hujuma?
   
 10. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #10
  Feb 18, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Ningependa kujua kwa kauri hiii kuwataka wananchi warudi maeneo, Je Eneo la tukio ni kubwa kiasi gani ambalo liko salama kwa wananchi kurudi kumbukeni ni mabomu yaliluka? Jeshi lilikuwa na uwezo gani wa kukusanya vipande vyote vilivyo ruka kutoka eneo la tukio mpaka kwenye nyumba za raia na kutuhakikshia walikusanya vipande vyote? na kama hivyo kanini unawambia wananchi warudi huku unawaambia wasiguse chuma chochote watakachokihisi ni tofauti na watoe taaarifa hapo huoni bado kuna hatari ya maisha ya raia wa maeneo hayo serikali acheni mzaha please. Any Crime Scene Investigation should not be Intrude until all the evidence have been collected together, sasa sielewi hii kamatia ya usalama ilifikilia hilo au inataka kurahisisha kazi na kuficha ukweli wa makosa yao kikazi au kukwepa uwajibikaji?
   
 11. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #11
  Feb 18, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,519
  Likes Received: 1,690
  Trophy Points: 280
  Mnapomchambua Rais eleweni kuwa na yeye ni sehemu ya Jeshi hilo hilo. Haitatokea na hata kama Rais wangu Slaa angekuwa Rais-Dola asinge wachana askari hadharani. Ni ukweli usiopingika kuwa kuna uzembe na hata Rais anaelewa lakini kwakuwa uzembe wenyewe umefanywa na jeshi,na kama kiongozi mkuu wa nchi anaelewa madhara ya kujiingiza kwenye migogoro na majeshi hivi sasa, anatakiwa afunike kombe....Tatizo ambalo wengi tunaliona ni kwa nini hajakurupuka kuwatimua kazi wakubwa hawa wa jeshi na wizara ya ulinzi. Nalo hilo nadhani kutokana na unyeti wake nadhani linapaswa liende taratibu hasa ukitazama kipindi tulichonacho kisiasa na kama tetesi zinavyosema kuwa mkubwa hakubaliki sana jeshini..
   
Loading...