Milioni Hamsini (50,000,000) zimeingia kimakosa kwenye Account yangu

Habari zenu ndugu zangu, nimeacha pesa kidogo sana kwenye
Account yangu ya NMB. (2,356,700) Nimeenda kuangalia salio
nimekuta 52,356,700.

Je naweza kuchukua hizi pesa na nisishitakiwe?
kama nitashitakiwa kuna uwezekano wa kushinda kesi?

Tafadhali naombeni maelezo haraka iwezekanavyo.

NB kwenye heading ni (50,000,000)

chukua mkuu... huo ni mkopo usio na riba
 
Si ajabu watu (wafanyakazi wa bank) wanapitishia pesa za wizi kwenye bank account yako. Zitaachwa hapo kuona huko zilikoibiwa kama wenye nazo watastuka wakiona kimya basi zitachotwa na watu kuweza kutanua mtaani. Sasa wewe umeweka shilingi 10 kwenye account yako ukakuta ziko shilingi 10,000 utachukuaje kile ambacho hakikuwekwa nawe? kwa maana nyingine si halali yako? Ukithubutu kufanya hivyo utakuwa ni wizi na unaweza kabisa kujitafutia matatizo makubwa na kuishia lupango kuchezea mvua kwa miaka kadhaa...Ila ifuatilie hiyo bank account yako kwa karibu ukiona hali hiyo inajitokeza mara kwa mara basi ongea na branch manager.
 
ilikuwa mwaka 82 nasimuliwa eti pale kijijini kwetu kuna ndege ilidondosha gunia la hela, akaliokota mama fulan (hadi leo yupo) afu maaskar walipokuja kawapa, wakamlamba kofi afu wakamwambia utakufa maskini, true 2 the moment she z very poor...WOGA WAKO NDO UMASKINI WAKO

Inaelekea wewe tunatoka kijiji kimoja, kwani hata mimi ninakotoka ilitokea hivyo.
 
Mkuu hiyo pesa kwa sasa imepewa jina la fedha chafu /fedha ya kutakatisha km ulisikia mabilioni yaliyotakatishwa Halmashauri ya Kishapu
Ndio huzo
Wafanyakazi wa Benki yako Makao makuu wanatuma hiyo 50m na ukitumna ATM hutaweza toa zaidi ya 1m weekend hii
Utakapoenda j3 Kaunta atakuelekeza uende kwa Mhasibu watakuelekeza u-Withdraw kwa leaf-check yako 50m na watakupa 1m km asante ww gangamala 5m km10%
Baada ya hapo toa oesa yote na funga A/c
Hiyo pesa Mhasibu anaifahamu na ipo ktk mahesabu yake alipofunga jumamosi
March 2012 BOT Benki kuu walilazimisha kila mwenye A/c aende kwa Mtendaji kwa hiyo km ukitoa na kusepa lazima wataingia kwako
tu km hutawashirikisha hao vijana wa (IT)wa Benki na bila hiyo hela yao hutoi
Huo ndio mchezo wa pesa za kutakatisha
 
Zipo toka Ijumaa, leo Alfajir saa 11 na dk 5 nilikwenda kucheki nimeikuta.

Kuna mfanyakazi mwenzetu aliingiziwa kimakosa kama milioni 2 hivi na jamaa akazichukua haraka na kuzitumia, kumbe ulikuwa mshahara wa mmoja wa wakurugezi pale ofisini kwetu. Ilibidi benki wawe wapole tu maana ni makosa yao lakini jamaa akakubali kuzilipa polepole lakini reputation yake ikawa imeharibika kwa kila mtu pale ofisini kuwa jamaa ni mdokozi a.k.a mwizi. Na pia kwenye akaunti ya ofisi yetu ziliwahi kuingizwa kama milioni 22 hivi kimakosa kumbe ni za polisi. Haya yote yalitokea NBM. Ofisi wakafuatilia ndo ikaja ikaonekana makosa yako wapi na wakazihamishia kwenye akaunti ya polisi. Kwahiyo nakushauri usizichukue na kuzitumia itakuwa wamekosea tu kuziingiza kwako. Na sasa hivi ni mwisho wa mwezi huenda ni za mishahara ya ofisi fulani ya serikali au taasisi ya umma.
 
Kama accout yako iko bize na imkuwa ikipokea transactions kubwa kubwa na at some point in time umekuwa uki maintain balance ya hiyo amount au hata zaidi, nakushauri tumia hiyo hela. lakini account huwa inaingiza vihela vidogo vidogo tu then ghafla unakuta million 50, hiyo mkuu achana nayo na toa taaarifa benk maramoja, kwa maana ukitumia maana yake ulikuwa unajua for sure kwamba hela siyo ya kwako na kwa hiyo umeamua kuiba.
Hela kubwa kuwahi kuingia kwenye AC yangu ni Mil 8 tu.
Haijawahi kuzidi wala kusogelea tena namba hiyo.
 
yawezekana hulali ukimuomba mungu akupe maisha mazuri, sasa kakubip tu ww unaooogopa! hapo alipo anakushangaa kwamba nn ukitakacho, mbona akikupa unatoa macho., take ze money, hv hujachukua tu.
Mkuu, unanichekesha. ATM haiwezi kutoa fedha zote hizo
labda nisubiri JTT nikajaribu bahati yangu au nitoe kidogo kidogo.
 
Kuna mfanyakazi mwenzetu aliingiziwa kimakosa kama miloni 2 hivi na jamaa akazichukua haraka na kuzitumia, kumbe ulikuwa mshahara wa mmoja wa wakurugezi pale ofisini kwetu. Ilibidi benki wawe wapole tu maana ni makosa yao lakini jamaa akakubali kuzilipa polepole lakini reputation yake ikawa imeharika kwa kila mtu pale ofisini kuwa jamaa ni mdokozi a.k.a mwizi. Na pia kwenye akaunti ya ofisi yetu ziliwahi kuingizwa kama milioni 22 hivi kimakosa kumbe ni za polisi. Haya yote yalitokea NBM. Ofisi wakafuatilia ndo ikaja ikaonekana makosa yako wapi na wakazihamishia kwenye akaunti ya polisi. Kwahiyo nakushauri uzisichukue na kuzitumia itakuwa wamekosea tu kuziingiza kwako. Na sasa hivi ni mwisho wa mwezi huenda ni za mishahara ya ofisi fulani ya serikali au taasisi ya umma.

Kweli mkuu anaweza kujikuta anakomba mshahara wa FFU au JWTZ, itakuwa balaa.
 
Ukizikuta kesho, toa na fanya mambo yako...utakuja kujuta sana baadae, BAHATI haiji mara mbili...kama una ATM card ulitakiwa umwe. Umeisha toa walau 5m maana inakupa option ya kutoa 4k mara 3 kwa cku so 1.2 x 3 kwa. Cku....changamka chief ....higher risk higher returns....kama una cmu ya Jitu Patel, Manji, Mengi au lowasa, Waulize ushauri hahaha
 
We vuta mkwanja. liwalo na liwe.Dunia hii bila kuwa jasiri huwezi kutoka na kumbuka bahati haiji mara mbili!
 
Habari zenu ndugu zangu, nimeacha pesa kidogo sana kwenye
Account yangu ya NMB. (2,356,700) Nimeenda kuangalia salio
nimekuta 52,356,700.

Je naweza kuchukua hizi pesa na nisishitakiwe?
kama nitashitakiwa kuna uwezekano wa kushinda kesi?

Tafadhali naombeni maelezo haraka iwezekanavyo.

NB kwenye heading ni (50,000,000)

Jamani acheni kutaka vya bure, there is no free lanchi, si unajua!? ignore tu kwa sababu si zako!
 
Ninachojua ni kuwa pesa inayokuwa ktk akaunti yako ni mali ya mwenye akaunti. Makosa yaliyofanywa na benki hayawezi kuwa shida kwako. Lakini kuna ethical dilema hapo; je Pesa ni zako?? Jambo la pili ni kuwa itakapothibitika kuwa umezilamba, lazima kutakuwa na ishu ya kisheria hapo, ambayo nayo ni mkasa na mchakato mwingine. Wazo langu, nenda benki utoe taarifa. Huwezi jua pengine ni bahati nasibu ya NMB ...
 
Subiri usizitoe halafu one mwisho wake, just be patient. Pia huko benki kuna wafanyakazi wanatumia account za watu kuibia hela. To be safe ziache na ukiona zimetolewa nenda karipoti direct to your Branch Manager (ulipofungulia account au NMB head office). Kama ni mwizi wa ndani ya benki atakamatwa kama panya kwenye mtego. Subiri mtu atalipuka tu!! unaweza kuta zimetolewa account ya mtu, zikapita kwako halafu zinatolewa!!!
 
Gazeti yani inasikitisha sababu hata hujafanyia justice hio avatar yako ya Mheshimiwa Fidel Castro. Kama ni moja ya watu wanao ku inspire I believe you have a long way to go. You are not brave kabisa.

Mwanaume unakua na simile. Chiilll, soma mchezo. Hasa unakuja kujimwaga hapa bwaaaa na intimate details zote mpaka bank na akaunt balance.
Frankly husathili hata punje ya hio hela, na ungestahili kupigwa vibao kama hio story ya huyo bibi hapo juu.

Mimi ilishanitoke a few years back, ziliingizwa milion 8. Nikatoa 6 asbuhi na mapema. Wakanipigia simu next day kua ilikua ni makosa yao nika waambia ningejueje?
Wakaenda kushtaki, nikaenda mahakamani. Ikaonekana nilipe lakini kwa uwezo wangu ambao nilisema ntaweza kulipa elfu 30 kwa mwezi ambapo deni litaisha in 16 years!
Bahati nzuri nilipata vijisenti flani nikalipa ndani ya mwaka (my reputation was at risk) na bank manager akanipa loan moja nzuri tu!
 
Gazeti yani inasikitisha sababu hata hujafanyia justice hio avatar yako ya Mheshimiwa Fidel Castro. Kama ni moja ya watu wanao ku inspire I believe you have a long way to go. You are not brave kabisa.

Mwanaume unakua na simile. Chiilll, soma mchezo. Hasa unakuja kujimwaga hapa bwaaaa na intimate details zote mpaka bank na akaunt balance.
Frankly husathili hata punje ya hio hela, na ungestahili kupigwa vibao kama hio story ya huyo bibi hapo juu.

Mimi ilishanitoke a few years back, ziliingizwa milion 8. Nikatoa 6 asbuhi na mapema. Wakanipigia simu next day kua ilikua ni makosa yao nika waambia ningejueje?
Wakaenda kushtaki, nikaenda mahakamani. Ikaonekana nilipe lakini kwa uwezo wangu ambao nilisema ntaweza kulipa elfu 30 kwa mwezi ambapo deni litaisha in 16 years!
Bahati nzuri nilipata vijisenti flani nikalipa ndani ya mwaka (my reputation was at risk) na bank manager akanipa loan moja nzuri tu!
Mkuu watofautishe hawa wawili kwenye picha.
castro.jpeg nazir karamagi (1).jpg
 
Back
Top Bottom