Milioni 600/= zaibwa kiaina NBC Ltd | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Milioni 600/= zaibwa kiaina NBC Ltd

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kiranja Mkuu, Feb 25, 2010.

 1. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #1
  Feb 25, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  [​IMG]Zilichotwa kwa kutumia kampuni hewa
  [​IMG]Wafanyabiashara, wafanyakazi wahusishwa

  JESHI la Polisi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wanachunguza wizi wa shilingi milioni 600 kutoka Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), uliofanywa na watumishi wa benki hiyo wakishirikiana na wafanyabiashara, Raia Mwema limefahamishwa.

  [​IMG]

  Habari za ndani ya Serikali zimethibitisha kwamba wiki iliyopita makachero walianza kuchunguza wizi huo ambao umehusisha matumizi ya nyaraka za kughushi kutoka taasisi mbalimbali za Serikali.

  Kwa mujibu wa habari hizo, wahusika katika wizi huo kwa msaada mkubwa wa watumishi waandamaizi wa NBC, walifanikiwa kuwasilisha nyaraka za kughushi za Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) pamoja na za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na za Benki ya CRDB Limited.

  Tayari wizi huo umetikisa NBC Limited ambako pamefanyika mabadiliko kadhaa na uchunguzi wa ndani unaendelea kwa uangalizi wa karibu wa wamiliki wa benki hiyo, taasisi kubwa ya fedha Afrika Kusini ya ABSA Group Limited.

  Kutokana na wizi huo, taarifa zinasema NBC imehamisha kitengo chake muhimu cha usalama wa nyaraka kwenda Idara ya Sheria kutokana na udhaifu uliojitokeza.

  Habari zinasema uongozi wa juu wa NBC ulianza kushitushwa na hatua ya kuchukuliwa kwa shilingi milioni 300 zilizochukuliwa na kampuni moja (jina tunalihifadhi kwa sasa) lakini maofisa waandamizi waliitetea kampuni hiyo wakidai kwamba mteja wao huyo ni mwaminifu.

  Ofisa mmoja Mwandamizi wa Polisi ameliambia Raia Mwema kwamba maofisa hao walipitisha hoja hiyo kwa kwa mujibu wa mamlaka waliyonayo ya kumwamini mteja wao ili kuhalalisha udhaifu katika nyaraka za wafanyabiashara walioshirikiana nao.

  [​IMG]

  Makao Makuu NBC, Dar es Salaam

  Uchunguzi wa Raia Mwema umethibitisha kwamba baadhi ya watumishi waliohusika katika wizi huo wamekuwa na rekodi ya matukio kama hayo, lakini wamefanikiwa kukwepa kitanzi cha menejimenti na vyombo vya dola kwa mbinu za kushangaza.

  "Kwa kweli inashangaza. Baadhi ni wazoefu katika wizi na wamewahi kuhusishwa na matukio mengi yenye ushahidi wa wazi, lakini bado wako kazini na badala yake wanaondolewa wale ambao wanahisiwa kuwa chanzo cha kuvujisha habari," kinaeleza chanzo cha habari kutoka Idara ya Upelelezi ya Jeshi la Polisi.

  Imeelezwa ya kuwa awali zilichukuliwa shilingi milioni 300 katika mikupuo kadhaa huku wahusika wakisuasua kulipa hadi ilipokuja kufahamika kwamba tayari zote milioni 300 zilikuwa zimechukuliwa. Baada ya hapo waliomba nyingine milioni 300 na baada ya kuzipata wakatoweka.

  "Baada ya NBC kuona mteja wao haonekani waliamua kwenda kukagua mahali zilipo ofisi za kampuni hiyo na kubaini ni kampuni hewa ambayo haipo popote. Wakaenda BRELA wakakuta kampuni hiyo haijawahi kusajiliwa huko na nyaraka husika zilikuwa za kughushi, wakafuatilia TRA wakakuta nako haifahamiki," anaeleza ofisa huyo wa Polisi.

  Ofisa huyo wa Polisi ameliambia Raia Mwema ya kuwa wezi hao wametumia hata nyaraka za kughushi kutoka benki ya CRDB Limited ambazo zilipokewa katika mazingira ya kutatanisha na NBC.

  Habari zaidi zinaeleza kwamba maofisa wanaotuhumiwa kushiriki wizi huo wamekuwa na tabia ya kupoteza hati za dhamana zinazotumiwa na baadhi ya wateja kuchukua mikopo na kusababisha benki hiyo kupata hasara kubwa kwa kushindwa kukamata mali za wateja wanaoshindwa kulipa madeni.

  Benki ya NBC Limited ilibinafsishwa mwaka 2000 baada ya kuendeshwa kwa miaka mingi kama shirika la umma. Ni kati ya mashirika ya umma yaliyozua utata mkubwa wakati wa kubnafsishwa kutokana na kile ambacho hadi leo wengine wanasema iliuzwa kwa bei ya kutupa.

  Wakati ABSA Group Limited ya Afrika Kusini inamiliki hisa 55 ndani ya NBC, Serikali ya Tanzania inamiliki husa 30 na Shirika la Kimataifa la Fedha (International Finance Corporation) linamiliki hisa 15.

  Chanzo: Raia Mwema
   
 2. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #2
  Feb 25, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,891
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Mwaka huu wa Uchaguzi tutaona mengi, tujipe Muda kabla hujaambiwa Kilimo kwanza fulani alilipwa pesa hizo kama Feasibility study na pesa hiyo italipwa na BOT maana ndio mdhamini wa kilimo kwanza huyo.
   
 3. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #3
  Feb 25, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,973
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 145
  Watu wanatumia kila njia kujipatia pesa mwaka huu au ndo za uchaguzi nn?
   
 4. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #4
  Feb 25, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 42,018
  Likes Received: 37,331
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo haya ma fraudi yanayoendelea kwenye mabenki ni mbinu za kisiasa?
   
 5. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #5
  Feb 25, 2010
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Sheria zetu dhaifu sana hasa za kazi,
   
 6. D

  DOGOO New Member

  #6
  Feb 25, 2010
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kazi kwelikweli
   
 7. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #7
  Mar 3, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,301
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hawa wataibiwa sana hasa kuelekea uchaguzi mkuu....nafikiria Kuanzisha Masanilo Inc nami nikakombe pesa za NBC! am serious buddies ! Hii nchi yangu wakati mwingine naona kama naishi kwenye hekaya za kusadikika!
   
 8. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #8
  Mar 3, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 368
  Trophy Points: 180

  Nawe una jimbo unalogombea mkuu?
   
 9. Lady N

  Lady N JF-Expert Member

  #9
  Mar 3, 2010
  Joined: Nov 1, 2009
  Messages: 1,919
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  mpka huo uchaguzi upite... itakuwa balaa
   
 10. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #10
  Mar 3, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,301
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Niko kwenye mchakato mazee, nahitaji kampeni meneja uko tayari?
   
 11. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #11
  Mar 3, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Duu ufisadi kila kona..This is too much.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...