Milioni 50 za kila kijiji zilikuwa usanii?

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,253
i4yROZ+K.jpg

Leo bungeni wakati waziri mkuu akihitimisha bajeti hotuba ya makadirio na matumizi ya ofisi yake.
Bunge wakati limekaa kama kamati likipitia vifungu vya bajeti ya waziri mkuu.

Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo na mbunge wa Kigoma Mjini Mh. Zitto Zuberi Kabwe amehoji kutoonekana kwa fedha walizoahidiwa wananchi kila kijiji kiasi cha sh milioni 50.
La kushangaza naibu spika akaingilia na akamwambia atulie.

Sasa tunajiuliza, je fedha hizi zilikuwa usanii?
 
Kila jambo na wakati wake bwana! ngoja majipu yapungue,watu tulipe kodi kwa wingi then hyo 50 unayoisema itaenda.mtumbua kaingia juzi tu!
 
Tunapotafuta wachumba ni muhimu kutoa ahadi tamu tamu nyingi ni hewa almradi mchumba aingie box akishaingia ndani ya nyumba unakausha kama vile kauzu, aking'ang'ana sana unamjibu kiulaini "ahadi hazitekeleziki" tuna mambo mengi muhimu..ya kuyafanya kujenga ndoa yetu.

Na siasa ni hivyo hivyo usisubiri 50m jipe shughuli nyingine tafadhali.
 
Kwa kweli utakua unasikitisha sana kama utaamini huu usanii wa huyu mtu anajiita makufuli!!

Bado sijasahau zile nyumba zilizouzwa kwa bei nafuu, meli ya samaki na ile nyumba aliyoongwa kimada!!! Bado sijasahau ile kashfa ya bwana mdogo a.k.a waziri kijana a.k.a february!!! And yet tunakua vipofu...sijui nani katuloga sisi watu wa hii nchi!!!

By the way toka lini lijipu likatumbua jipu???!
 
Tunapotafuta wachumba ni muhimu kutoa ahadi tamu tamu nyingi ni hewa almradi mchumba aingie box akishaingia ndani ya nyumba unakausha kama vile kauzu, aking'ang'ana sana unamjibu kiulaini "ahadi hazitekeleziki" tuna mambo mengi muhimu..ya kuyafanya kujenga ndoa yetu.

Na siasa ni hivyo hivyo usisubiri 50m jipe shughuli nyingine tafadhali.

Mkuu unamaanisha rais wetu alitudanganya???
 
Kila jambo na wakati wake bwana! ngoja majipu yapungue,watu tulipe kodi kwa wingi then hyo 50 unayoisema itaenda.mtumbua kaingia juzi tu!

Yani nyie ndio mnafanya mpaka average IQ ya watanzania inakua chini!! Pathetic...
 
Ataitoa wapi wakati la sukari ya ndani imewashinda? Hivi pale bandarini mbona meli za mizigo sizioni kama mwaka jana zimekwenda kupakua tanga? Tutajiju safari hii.
 
Miliono 50 kila kijiji zitatolewa kila Kijiji bila shaka, kwa mtindo ule ule wa Posho za Wajumbe wa BMK
 
nadhani zito naye anaanza kuota, pia tumuulize na yeye kama ameshatimiza ahadi zote alizowaahidi wana kigoma anao wawakilisha, maana anafikiri kwa miezi hii saba ya magu anaweza kutimiza kila kitu alichoahidi..labda awe super human..
 
Kila jambo na wakati wake bwana! ngoja majipu yapungue,watu tulipe kodi kwa wingi then hyo 50 unayoisema itaenda.mtumbua kaingia juzi tu!
Bado unapiga kampeni? Huu ni muda wa utekelezaji bana!
 
" Tayari Mheshimiwa Rais amewaagiza Wakuu wa Mikoa kuhakikisha kwamba vijana ambao ndiyo nguvu kazi kuu ya Taifa wanatumia fursa itakayopatikana kutokana na Shilingi Milioni 50 zitakazotolewa kwa kila kijiji kuanzisha miradi ya maendeleo ya kujipatia kipato" ~ WM M.K. Majaliwa
 
Mbona haipo kwenye bajeti ya ofisi ya waziri mkuu? watatumia kutoka wapi mkuu?
 
Mbona haipo kwenye bajeti ya ofisi ya waziri mkuu? watatumia kutoka wapi mkuu?
Kwa maelezo ya WM inaonekana maandalizi yanatakiwa yafanyike, vikundi vya SACCOS vihakikiwe kabla fedha haijatumwa. Sijajua itachukua mda gani na pia sijajua zitapitia wizara gani
 
Back
Top Bottom