Milioni 400 kujenga majengo matano ya kituo cha afya cha Mtoa - Iramba

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,886
938
MILIONI 400 KUJENGA MAJENGO MATANO YA KITUO CHA AFYA CHA MTOA - IRAMBA.

Mkuu wa wilaya ya Iramba Mkoani Singida Mhe Suleiman Yusuph Mwenda ameendelea kufanya ziara ya kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi ambapo akiwa kata ya Mtoa amesikiliza kero za wananchi na kufuatilia ujenzi wa kituo cha afya kata ya Mtoa chenye hadhi ya upasuaji ambacho kitakuwa kimetatua adha kubwa wanayokumbana nao wakazi wa kata hiyo na maeneo ya jirani.

Akitoa taarifa kwa wananchi wa kata hiyo Mwakilishi wa Mganga mkuu wa wilaya ya Iramba Dkt Timothy Sumbe amewaambia wananchi waliojitokeza kumsikiliza Mkuu wa wilaya kwenye ziara hiyo kuwa Serikali imeleta Jumla ya fedha Shilingi Milioni 400 na wanatarajia kuanza ujenzi wa majengo 5 ambayo ni jengo la upasuaji, jengo la mama na mtoto, jengo la maabara, jengo la kuhifadhia maiti, jengo la kufulia, nyumba moja ya mtumishi na amewaomba wananchi washiriki katika kuchangia nguvu kazi kama kukusanya mawe, mchanga na maji ili kuweza kufanikisha ujenzi wa kituo hicho cha afya Mtoa.

Aidha Diwani wa kata ya Mtoa amemuhakikishia Mkuu wa wilaya Mhe Mwenda kuwa wananchi wamekubali kuchangia vitu vyote vinavyotakiwa ili ujenzi uweze kukamilika kwa haraka na kuanza kutoa huduma kwa wananchi wa kata hiyo na kata za jirani.

Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya Mhe Mwenda amewatahadharisha watendaji wa Serikali wasiokuwa makini katika kusimamia majukumu mbalimbali kwani tabia hiyo imekuwa ikiwavunja nguvu wananchi wanaojitoa kuchangia na ujenzi uende kwa kasi. Mradi huo wa kituo cha afya una faida nyingi sana kwani mara utakapokamilika utapunguza kusafiri umbali mrefu kwa akina mama wajawazito kwenda kufuata huduma vilevile itawasaidia wazee kupata huduma karibu.

Mhe Mwenda amewataka wananchi wa kata ya Mtoa kumpa ushirikiano ili kwa pamoja kuweza kuleta maendeleo. "Mimi niwahakikishie wananchi wenzangu nitawasimamia watumishi wenzangu kwa kuhakikisha nguvu za wananchi hazipotei na atakayejaribu kufanya hivyo hatutamvumilia hatua kali dhidi yake nitamchukulia." Alisema Mhe Mwenda.

Mhe Mkuu wa wilaya Mwenda anafanya ziara kila kata kwa lengo la kujitambulisha, kuwashukuru wananchi waliofanikisha ugeni wa Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru mwaka 2021, kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi.

#IrambaKaziInaendelea
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom