DOKEZO Milioni 100 alizotoa Makonda, ni za kwake, Serikali au za Nani? TAKUKURU mna jibu?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,792
71,206
Hakika sasa watu watahoji hadi wataonekana wana wivu. Makonda Leo katoa Shilingi milioni 100 kwa Chama chake CCM ili kuanzisha mfuko wa kusaidiana ndani ya Chama.

Kwa sababu hakusema kuwa fedha hizo ni za serikali au mchango wa wadau basi ni fedha zake mwenyewe.

Hivi Makonda huwa anapata wapo fedha za kuweza kushindana na wafanyabiashara wakubwa registered katika kutoa misaada?

Sheria ya maadili ya viongozi inataka kiongozi kuweka wazi vyanzo vya mapato, zawadi na hata michango inayopatikana kwa kiongozi. Kwa nini huyu jamaa ni exceptional?

Jee ni mla rushwa mkubwa? Mnyang'anyi wa fedha za wafanyabiashara wakubwa kama tetesi zilivyo? Au pia habari kuwa anatumwa na aliyemteua kukusanya ndio maana hahojiwi?

Kwenye suala hili hakika TAKUKURU wamebaki kuwa Toothless bulldog, na ni aibu kwa taasisi kumshindwa MTU mdogo kama RC wakati tunaona nchi zingine taasisi kama hiyo zinaweza kumuwajibisha hata mkuu wa nchi.

MAKONDA ANATOA WAPI PESA HIZI ZA KUHONGA?
 
Na hali hii ya walio madarakani kwa sasa kugawa fedha kwa mtindo wa papo kwa hapo bila maelezo ya vyanzo kama ni fuko maalum linalotokana na wananchi walipa-kodi, michango ya wadau , harambee n.k basi tunakaribisha uvujifu wa maadili ya uongozi.

Tukinyamaza bila kuhoji tunakaribisha mianya ya rushwa, ufisadi, kulazimishwa kuchanga bila hiyari , ujambazi-wa-kidola n.k
 
Hii nchi tunakula kwa zamu zamu tu,waliokuwa wanakula enzi za JK hali mbaya,saizi ni zamu yake acha ajinafasi,japo inaleta DOA na PCCB ni toothless
 
Na hali hii ya walio madarakani kwa sasa kugawa fedha kwa mtindo wa papo kwa hapo bila maelezo ya vyanzo kama ni fuko maalum linalotokana na wananchi walipa-kodi, michango ya wadau , harambee n.k basi tunakaribisha uvujifu wa maadili ya uongozi.

Tukinyamaza bila kuhoji tunakaribisha mianya ya rushwa, ufisadi, kulazimishwa kuchanga bila hiyari , ujambazi-wa-kidola n.k
Unadhani hii tabia ya kugawa gawa maburungutu ya fedha wakina Makonda wameiga kutoka kwa nani?
 
Umeonyesha uko kumpinga Makonda basically sababu waijua mwenyewe. Wewe mwenyewe unasema hajasema pesa ni zake au laa ila umeamua kuhitimisha kuwa ni zake kisa hajasema ni zake au laa ili tu ujenge msingi wa hoja yako dhaifu.
2010's Makonda alikua anampiga vita Lowassa mbaya kabisaa kwa kugawa gawa mafedha misikitini/kanisani/kwny mahafla full kumuita fisadi sijui nini kumbe na Makonda alikua anamuonea wivu tu sababu yeye miaka hio hakua na fedha za kugawa hahah.
 
Usiamishe magoli, wapi kasema ni zake au sio zake?
 
Back
Top Bottom