Milioni 1 yampa wakati mgumu msanii ‘hemedi’, ni deni la nguo anazovaa kwa mkopo…!!

Money Stunna

JF-Expert Member
Aug 9, 2011
13,054
6,281
hemedi_phd2.jpg

UKWELI wa mambo juu ya msanii anayependa kulipuka pamba Hemed Suleiman ’Hemedi’ almaarufu kama PHD au Alejandro, umevuja kwani inadaiwa kuwa nguo zote anazoonekana anavaa huwa anachukua kwa mkopo na hulipa baada ya muda fulani lakini sasa kiasi cha fedha anachodaiwa ni kikubwa na hana uwezo wa kulipa kwa sasa kwani ni zaidi milioni 1.

Duka moja la nguo maarufu sana lilipo maeneo ya Kinondoni, ndilo lililotoa ishu hiyo baada kuona jamaa huyo anazingua kulipa na walikuwa wakimpa kila nguo anayohitaji kwani walimuamini kwa kuwa nguo nyingi alikuwa akinunua hapo kwao.

Muuzaji wa pamba hizo katika duka hilo ambaye hakupenda jina lake litajwe na duka pia, alisema kuwa awali jamaa alikuwa akilipa kama kawaida lakini ilifika kipindi alikuwa anachukuwa kila baada ya wiki na hadi hivi sasa anadaiwa si chini ya milioni 1.

“Hemedi tunamuamini lakini sasa hali hii inafikia kuwa vita kwa sababu kiasi cha fedha tunachomdai ni kikubwa kwa sababu watu wanafanya kazi wanahitaji kulipwa mshahara, tunafikilia kuchukua maamuzi ili aweze kutulipa kwa haraka. Jamaa sikuhizi haji hapa na wala sijamuona kupita sasa sijui anakimbia madeni au vipi,” aliongeza

Hata hivyo Hemedi alipotafutwa kuzungumzia ishu hiyo kama ina ukweli wowote hakuweza kupatikana na taratibu zinaendelea za kumtafuta ili aweke wazi juu ya habari hizo.
 
Kwanza simpendi kuna siku alijinadi kwenye TV kabisa kuwa yeye huwa akitoa album huwa anasikilizia ni mademu wangapi wanampigia simu si ubwege huuu kumbe hana kitu haaya ameumbuka sasa
 
Ndiyo mastar wetu hao, mikogo mingi lakini ukiwafatilia ni balaa tupu

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
kuna siku alikuwa anahojiwa kwenye TV akasema yy huwa harudii kuvaa nguo na viatu mara mbili.
 
mkuu alichosema yeye akishaivaa mara moja anampa mtu mwingine.
Kwahiyo huyu basi anamzidi pesa hata Andrew Chenge ambaye suti zake zinapelekwaga kufuliwa London kama percels.

Siko Interested kuwafatilia hawa Masharo uharo, ndio shida ya watu maskini akipata uwezo wa kuanza kula chips mayai badala ya Chips dume basi anaona amemaliza Maisha.:target:
 
Mambo mengine ni kichekesho kwani ajabu yeye kudaiwa jaman tuache ushabiki.ktk hii dunia watu tunategemeana kwa mengi tu.angalia watu malufu wanadaiwa,klabu malufu zinadaiwa ht matajili nao wanadaiwa hvy yeye kudaiwa sio ajabu.ht mi nadaiwa kwan wewe hudaiwi?
 
Back
Top Bottom