Ecclesiastes
Member
- Nov 20, 2016
- 10
- 40
Tupo tunaoielewa..mkuu lugha ya wapi hii!?
andika ueleweke, nafikiri kiswahili au kingereza utaeleweka zaidi
Tupo tunaoielewa..mkuu lugha ya wapi hii!?
andika ueleweke, nafikiri kiswahili au kingereza utaeleweka zaidi
Mkuu wa mko wa Dar es salaam mh Paul Makonda amejitolea kuandaa mpambano mkali sana wa kugombea Tsh 50 millions baina ya wasanii wawili waotumbuiza muziki kupitia live band kati ya king of the best melody Christian bella dhidi ya mkongwe Banana Zoro!
Mkuu huyo wa mkoa ameyasema hayo katika hafla yake fupi ya kujipongeza baada ya ziara ya siku 10 ya kutatua kero za wana Dar es salaam, pia amesema yeye binafsi ni mpenzi wa muziki unaopigwa live.
My take: Wakazi wa Dar es salaam kero zao zimekwisha tatuliwa na mheshimiwa, ndio maana kaamua kuanzisha tamasha hili la watu wawili tu likimtaka mshindi mmoja (winner take all).
Msijali hizo zinatoka kwa Mdosi wa GSM.Hizo zitatoka mfuko wa serikali i.e. ni kodi zetu?
Hizo hela za mshindi atakaezitoa ni nani??Mkuu wa mko wa Dar es salaam mh Paul Makonda amejitolea kuandaa mpambano mkali sana wa kugombea Tsh 50 millions baina ya wasanii wawili waotumbuiza muziki kupitia live band kati ya king of the best melody Christian bella dhidi ya mkongwe Banana Zoro!
Mkuu huyo wa mkoa ameyasema hayo katika hafla yake fupi ya kujipongeza baada ya ziara ya siku 10 ya kutatua kero za wana Dar es salaam, pia amesema yeye binafsi ni mpenzi wa muziki unaopigwa live.
My take: Wakazi wa Dar es salaam kero zao zimekwisha tatuliwa na mheshimiwa, ndio maana kaamua kuanzisha tamasha hili la watu wawili tu likimtaka mshindi mmoja (winner take all).
Makonda mwenyewe!Hizo hela za mshindi atakaezitoa ni nani??
Mkuu unawajua GSM?Hizo 50m aseme amezipata wapi, Maana yeye ni mtumishi wa umma.
Hiii stori ichapishwe isomwe na wanafunzi wa o-lever ni fasihi toshaHadithi ya Mwendapole na Madereva
Hawa ni vijana waliojipatia umaarufu mkubwa katika nchi ya Kusadikika kila mmoja kwa sababu zake tofauti.
Madereva alianza kupanda chati baada ya kusikika hadharani akiwatukana viongozi (hata wa chama chake) na akafika kilele pale alipoonekana wazi akitaka kuvuruga mchakato wa KATI BAR mpya ili juwafurahisha wakuu wake. Anakumbukwa kwa vurugu za pale kwenye LULU ya BULUU aliposemekana alimpiga Mzee War Iobber kwa chupa ya maji na mdahalo kuvurugika.
Kwa upande wa MwendaPole yeye alijipatia umaarufu kwa sababu zote chanya, kwanza alisimamia kile alichoamini kuhusu mchakato wa KATI BAR kuwa KATI BAR ya wananchi ndiyo mwarobaini wa kudumu kwa taifa la Kusadika.
Kwa vyovyote vile...vijana hawa kwa wakati ule hawakuwa marafiki wala kuwa na fikra sawa, mmoja akitetea genge lililomtuma akawa mpiga zumari wa mfalme na mwingine akitaka KATI BAR inayowapa wananchi nguvu zaidi na kumbana mfalme.
Zoezi la Kati Bar likafa kifo cha kimya kimya, likafuatiwa na uchaguzi wa kumpata mfalme mpya lakini kabla yule wa zamani hajaondoka akamteuwa Madereva kuwa mkuu wa WE-LIAR, wengi wakasema ni fadhila kwa kazi nzuri ya upigaji wa zumari. Kuelekea uchaguzi wa mfalme mpya, Mwendapole akaamua kumpigania mfalme mpya kutoka msitu wa kijani, akidhani huyu mpya atakuwa na tofauti na aliyemtangulia. Watu wakasema sana kuwa Mwendapole anataka kupewa mfupa...akakanusha na kujiapia kuwa hataki na anamwomba Mungu amwepushe.
Ukafika wakati mfalme mpya anatoa fadhila kwa wapiganaji wake....Mwendapole akapewa mfupa...watu wakamkumbusha viapo vyake, jamaa akala ngumu. Madereva naye akabadili gia angania akawa dam dam na mfalme mpya akabaki mjini. Yakatokea mabadiliko, Madereva akapandishwa cheo akawa mkubwa wa Mjini na Mwendapole akatolewa kijijini akaletwa mjini sasa yupo chini ya Madereva.
Mambo yamebadilika sana, Mwendapole aliamini na anajua kuwa anauwezo mkubwa kuliko Madereva, na anajua kuwa mfalme mpya hasimamii kabisa misingi ya ile KATI BAR aliyokuwa anaipigania, amejikuta katika wakati mgumu....si wa kumeza wala kutema, amebaki kuwa MWANAFALSAFA akiandika maneno magumu ambayo wadadisi na wachunguzi wa kusadikika wanadai kuwa hali sasa si nzuri kwa Mwendapole.
Wananchi wanamtaka Mwendapole afanye maamuzi na siyo kulalamika kwa mafumbo, achague mmoja awe mpiga zumari wa mfalme au aendelee kutetea KATI BAR ya wananchi iliyomjengea heshima kubwa lakini ajue kuwa, akichagua uamuzi wa pili akubali kujitoa, kujikana na katu hatafanikiwa asipohama katika msitu wa Kijani.
The best way to do a crime,,,is to do it in public...Hivi TAKUKURU hawana meno ya kumchunguza Mkuu wa Mkoa?
Ukimfatilia kwa mwezi mzima matumizi yake ni zaidi mara 100 ya mshahara wake kama mtumishi umma.
Hakuna utakatishaji unaendelea hapa?
23. Bali umejiinua juu ya Bwana wa mbingu; nao wamevileta vyombo vya nyumba yake mbele yako; na wewe, na wakuu wako, na wake zako, na masuria wako, mmevinywea; nawe umeisifu miungu ya fedha na ya dhahabu, na ya shaba, na ya chuma, na ya mti, na ya mawe; wasioona, wala kusikia, wala kujua neno lo lote; na Mungu yule, ambaye pumzi yako i mkononi mwake, na njia zako zote ni zake, hukumtukuza. 24. Ndipo kile kitanga cha ule mkono kikaletwa kutoka mbele zake, na maandiko haya yameandikwa. 25. Na maandiko yaliyoandikwa ni haya; MENE, MENE, TEKELI, NA PERESI. 26. Na tafsiri ya maneno haya ni hii; MENE, Mungu ameuhesabu ufalme wako na kuukomesha. 27. TEKELI, umepimwa katika mizani nawe umeonekana kuwa umepunguka. 28. PERESI, ufalme wako umegawanyika, nao wamepewa Wamedi na Waajemi. 29. Ndipo Belshaza akatoa amri, nao wakamvika Danieli mavazi ya rangi ya zambarau wakatia mkufu wa dhahabu shingoni mwake, wakapiga mbiu kutangaza habari zake, ya kwamba yeye ni mtu wa tatu katika ufalme. 30. Usiku uo huo Belshaza, mfalme wa Wakaldayo akauawa. 31. Na Dario, Mmedi, akaupokea ufalme, naye umri wake alikuwa na miaka sitini na miwilimkuu lugha ya wapi hii!?
andika ueleweke, nafikiri kiswahili au kingereza utaeleweka zaidi