Milion 50 za Paul Makonda kushindaniwa na wasanii wawili, Banana Zoro vs Christian Bella

Mh.Kinana ni kiongozi mzuri saana na anayeweza kuongoza na kuishi na watu wa aina yoyote ile.Kinana hana dharau na hana lugha za tashtiti au matusi.Anamjuwa Mwenyezimungu ni nani.Sifa za Kinana zinashabiana na sifa za Lowassa na wote hali zao kimaisha ni nzuri na wanatoa misaada kwa siri na dhahir pia.
SWALI..........kwa nini hao wako hivyo
JIBU.....ni rahisi saana hawa waliandaliwa wakapikwa wakaiva ndipo wakaletwa mezani....kwa neno moja WAMEANDALIWA...
Kama itifaki inaruhusu basi watusaidie kuwaanda viongozi wengine vijana kwa kesho.
 
1480586381818.jpg
 
Mkuu unatokwa na povu la bule ndugu yangu... Ulishaambiwa serikari haina dini hivyo ukiona viongozi wanawajibika hapo hakuna swala la huruma huruma mkumbuke hii serikali haicheki na nyani kwa maana inaogopa kuvuna mabua.... Hivyo muache mkuu wangu wa mkoa awajibike kwa nafasi yake na hivyo ndio mkuu wa kaya anavyotaka na ndio maana unaona kila analofanya mkuu wa mkoa basi kuna baraka za mkuu wa kaya na sio baraka de prince.
 
tulijaribu kucheza mpira kwa mdomo, tukashindwa. Sa tunajaribu kujenga nchi kwa njia ile ile!
 
Nimeshajua wananchi wangu mna shida gani ngoja kwanza nile raha kidogo kwa kuona live mpambano kati ya nguli hawa wa music wa dance baada ya hapo nirudi ofisini kupanga mipango mikakati ya namna ya kupata fedha za kutatua matatizo yenu. Msiwaze vibaya jamani hivi vi ml 50 ninavyotoa kama zawadi ni kama tone la maji tuu kwenye shida na matatizo yenu. Zinahitajika fedha nyingi sana kuondoa kabisa matatizo ya wananchi.
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema ataandaa show ya kuwashindanisha kuimba live kati ya waimbaji wawili mahiri, Christian Bella na Banana Zoro na mshindi mmoja kati yao ataondoka na kitita cha tsh milioni 50.
xpage.jpg.pagespeed.ic.2zPxAB1qEF.webp

Amesema hayo katika hafla fupi ya kuwashukuru watumishi wa serikali ya mkoa wa Dar es salaam pamoja na wadau mbalimbali walioshiriki katika ziara yake ya siku kumi ya kusikiliza kero za wananchi na pamoja na kuzitatua.

RC alisema yeye ni mpenzi wa muziki wa live hivyo anawataka wasanii hao kukaa pamoja na kujadiliana ni lini watafanya show hiyo ili maandalizi yaanze kufanyika mapema.

“Hakuna mshindi wa pili wala watatu, tunamtaka mmoja tu ambaye ataondoka na milioni 50. Kwa hiyo pangeni muiangalie ni lini mtafanya hiyo show,” alisema Makonda.

Pia Makonda walitoa zawadi mbalimbali kwa baadhi ya watumishi wa serikali pamoja na wadau mbalimbali ambao alionyesha kufanya kazi vizuri katika ziara hiyo.

Katika halfa hiyo Banana Zoro, Christian Bella, Mrisho Mpoto ni miongoni mwa wasanii ambao walitoa burudani.

SOURCE: BONGO5
Nakodi pia ikatwe..kwenye hiyo 50M
 
Back
Top Bottom