Milion 50 za Paul Makonda kushindaniwa na wasanii wawili, Banana Zoro vs Christian Bella


Daniel Agger

Daniel Agger

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2013
Messages
3,217
Likes
3,483
Points
280
Daniel Agger

Daniel Agger

JF-Expert Member
Joined Aug 29, 2013
3,217 3,483 280
Mkuu wa mko wa Dar es salaam mh Paul Makonda amejitolea kuandaa mpambano mkali sana wa kugombea Tsh 50 millions baina ya wasanii wawili waotumbuiza muziki kupitia live band kati ya king of the best melody Christian bella dhidi ya mkongwe Banana Zoro!

Mkuu huyo wa mkoa ameyasema hayo katika hafla yake fupi ya kujipongeza baada ya ziara ya siku 10 ya kutatua kero za wana Dar es salaam, pia amesema yeye binafsi ni mpenzi wa muziki unaopigwa live.

My take: Wakazi wa Dar es salaam kero zao zimekwisha tatuliwa na mheshimiwa, ndio maana kaamua kuanzisha tamasha hili la watu wawili tu likimtaka mshindi mmoja (winner take all).
 
Twalyaninkomi

Twalyaninkomi

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2016
Messages
266
Likes
256
Points
60
Age
27
Twalyaninkomi

Twalyaninkomi

JF-Expert Member
Joined Oct 31, 2016
266 256 60
Hongera saana mkuu paul makonda!
Baada ya kazi ngumu ya kutatua kero za wananchi na kufanikiwa, ni muda rasmi kwako wewe na wananchi wako kujipongeza na kuburudika kwa burudani heavy kama hiyo!
 
F

Farudume

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2013
Messages
3,916
Likes
2,947
Points
280
Age
32
F

Farudume

JF-Expert Member
Joined Jan 10, 2013
3,916 2,947 280
Kuna kipindi alitangaza mashindano ya usafi kwa mitaa yote ya jiji la DSM na kuahidi zawadi ya gari kwa mshindi.Sijajua hili zoezi limeishia wapi au mtaa gani ulishapata zawadi.Tena Tangazo hili lilirushwa moja kwa moja na TBC.Tafadhali mwenye kuelewa chochote kuhusu hili anifahamishe.
 
Twalyaninkomi

Twalyaninkomi

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2016
Messages
266
Likes
256
Points
60
Age
27
Twalyaninkomi

Twalyaninkomi

JF-Expert Member
Joined Oct 31, 2016
266 256 60
Kuna kipindi alitangaza mashindano ya usafi kwa mitaa yote ya jiji la DSM na kuahidi zawadi ya gari kwa mshindi.Sijajua hili zoezi limeishia wapi au mtaa gani ulishapata zawadi.Tena Tangazo hili lilirushwa moja kwa moja na TBC.Tafadhali mwenye kuelewa chochote kuhusu hili anifahamishe.
Jiji chafu mitaa yote, zawadi ishawekwa kapuni!
Hakuna anayestahili
 
King Kong III

King Kong III

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2010
Messages
32,865
Likes
15,392
Points
280
King Kong III

King Kong III

JF-Expert Member
Joined Oct 15, 2010
32,865 15,392 280
Hadithi ya Mwendapole na Madereva

Hawa ni vijana waliojipatia umaarufu mkubwa katika nchi ya Kusadikika kila mmoja kwa sababu zake tofauti.

Madereva alianza kupanda chati baada ya kusikika hadharani akiwatukana viongozi (hata wa chama chake) na akafika kilele pale alipoonekana wazi akitaka kuvuruga mchakato wa KATI BAR mpya ili juwafurahisha wakuu wake. Anakumbukwa kwa vurugu za pale kwenye LULU ya BULUU aliposemekana alimpiga Mzee War Iobber kwa chupa ya maji na mdahalo kuvurugika.

Kwa upande wa MwendaPole yeye alijipatia umaarufu kwa sababu zote chanya, kwanza alisimamia kile alichoamini kuhusu mchakato wa KATI BAR kuwa KATI BAR ya wananchi ndiyo mwarobaini wa kudumu kwa taifa la Kusadika.

Kwa vyovyote vile...vijana hawa kwa wakati ule hawakuwa marafiki wala kuwa na fikra sawa, mmoja akitetea genge lililomtuma akawa mpiga zumari wa mfalme na mwingine akitaka KATI BAR inayowapa wananchi nguvu zaidi na kumbana mfalme.

Zoezi la Kati Bar likafa kifo cha kimya kimya, likafuatiwa na uchaguzi wa kumpata mfalme mpya lakini kabla yule wa zamani hajaondoka akamteuwa Madereva kuwa mkuu wa WE-LIAR, wengi wakasema ni fadhila kwa kazi nzuri ya upigaji wa zumari. Kuelekea uchaguzi wa mfalme mpya, Mwendapole akaamua kumpigania mfalme mpya kutoka msitu wa kijani, akidhani huyu mpya atakuwa na tofauti na aliyemtangulia. Watu wakasema sana kuwa Mwendapole anataka kupewa mfupa...akakanusha na kujiapia kuwa hataki na anamwomba Mungu amwepushe.

Ukafika wakati mfalme mpya anatoa fadhila kwa wapiganaji wake....Mwendapole akapewa mfupa...watu wakamkumbusha viapo vyake, jamaa akala ngumu. Madereva naye akabadili gia angania akawa dam dam na mfalme mpya akabaki mjini. Yakatokea mabadiliko, Madereva akapandishwa cheo akawa mkubwa wa Mjini na Mwendapole akatolewa kijijini akaletwa mjini sasa yupo chini ya Madereva.

Mambo yamebadilika sana, Mwendapole aliamini na anajua kuwa anauwezo mkubwa kuliko Madereva, na anajua kuwa mfalme mpya hasimamii kabisa misingi ya ile KATI BAR aliyokuwa anaipigania, amejikuta katika wakati mgumu....si wa kumeza wala kutema, amebaki kuwa MWANAFALSAFA akiandika maneno magumu ambayo wadadisi na wachunguzi wa kusadikika wanadai kuwa hali sasa si nzuri kwa Mwendapole.

Wananchi wanamtaka Mwendapole afanye maamuzi na siyo kulalamika kwa mafumbo, achague mmoja awe mpiga zumari wa mfalme au aendelee kutetea KATI BAR ya wananchi iliyomjengea heshima kubwa lakini ajue kuwa, akichagua uamuzi wa pili akubali kujitoa, kujikana na katu hatafanikiwa asipohama katika msitu wa Kijani.
 
M

mwasu

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2011
Messages
8,553
Likes
6,660
Points
280
M

mwasu

JF-Expert Member
Joined Jul 13, 2011
8,553 6,660 280
Panya road wameibuka upya, ki uhalisia ile ziara haijatatua kero bali imeongeza kero kwa waajiriwa wa manispaa, pale walipo dhalilishwa na kudhihakiwa.
 
K

Kilityme

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2015
Messages
218
Likes
565
Points
180
K

Kilityme

JF-Expert Member
Joined Aug 13, 2015
218 565 180Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema ataandaa show ya kuwashindanisha kuimba live kati ya waimbaji wawili mahiri, Christian Bella na Banana Zoro na mshindi mmoja kati yao ataondoka na kitita cha tsh milioni 50.


Amesema hayo katika hafla fupi ya kuwashukuru watumishi wa serikali ya mkoa wa Dar es salaam pamoja na wadau mbalimbali walioshiriki katika ziara yake ya siku kumi ya kusikiliza kero za wananchi na pamoja na kuzitatua.

RC alisema yeye ni mpenzi wa muziki wa live hivyo anawataka wasanii hao kukaa pamoja na kujadiliana ni lini watafanya show hiyo ili maandalizi yaanze kufanyika mapema.

“Hakuna mshindi wa pili wala watatu, tunamtaka mmoja tu ambaye ataondoka na milioni 50. Kwa hiyo pangeni muiangalie ni lini mtafanya hiyo show,” alisema Makonda.

Pia Makonda walitoa zawadi mbalimbali kwa baadhi ya watumishi wa serikali pamoja na wadau mbalimbali ambao alionyesha kufanya kazi vizuri katika ziara hiyo.

Katika halfa hiyo Banana Zoro, Christian Bella, Mrisho Mpoto ni miongoni mwa wasanii ambao walitoa burudani.SOURCE: BONGO5
 
number41

number41

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Messages
1,410
Likes
800
Points
280
number41

number41

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2015
1,410 800 280
Kuna mtu amelia njaa sasa atatumia njia gani kumpa hela mana siku izi watu wako macho sasa ngoja tutumie akili kuna milioni 100 hapa wewe kamata hii 50 na we 50 yako hii hapa piga show mshindi tayari amechuka 50 kwa 50 akuna shida ni shindano jmn sijaonga hela
 
mtotowatatu

mtotowatatu

Senior Member
Joined
Jul 31, 2016
Messages
103
Likes
58
Points
45
Age
29
mtotowatatu

mtotowatatu

Senior Member
Joined Jul 31, 2016
103 58 45
Huyu bwana anavituko sana, kwa nini asinge toa angalau hiyo hela kama motivation kwa wafanykz zaid ya kuishia kuwatishia tu ,,hao wasanii wamesaidia nni mkoa huo
 

Forum statistics

Threads 1,274,531
Members 490,721
Posts 30,515,437