Milango ya kupanga katika fremu zilizopo King'azi Maramba Mawili Dsm

Mpenda Uzalendo

Senior Member
Dec 18, 2015
112
58
Anakaribishwa yeyote anayehitaji mlango / milango ya kupanga katika fremu zilizopo King'azi (Maramba Mawili uelekeo wa barabara ya kwenda Kinyerezi).

Fremu hizi zipo barabarani na ni eneo ambalo wakazi wake huwa inabidi watembee mwendo mrefu kabla ya kufikia maduka ya vitu wanavyovihitaji kwa matumizi muhimu ya kila siku kama mchele, unga, mafuta, nyanya, vitunguu nk.
Ni eneo zuri sana kwa biashara pia kwa wale wajasiriamali ambao ni wabunifu wa kutambua ni vitu gani vingine vinaweza kuuzwa kwa faida ili kukidhi uhitaji wa watu wa eneo hili.

Kwa wale ambao watahitaji kupanga kama ofisi pia wanakaribishwa.
Kila kitu kipo tayari ila tunasubiri kuunganishiwa umeme kwenye fremu hizi (malipo Tanesco yameshafanyika)
 

Attachments

  • IMG-20161223-WA0003.jpg
    IMG-20161223-WA0003.jpg
    116.6 KB · Views: 253
Mkuu maeneo hayo kuna duka la dawa kama halipo niambie nije nifungue mkuu. Namba yang n 0658047048

Hakuna kabisa duka lolote la dawa hapo karibu.Tena kuna Mzee hapo jirani anasema wanahangaika sana kwenda kupata bidhaa muhimu sehemu ya mbali.
Nakushauri uende ukatazame eneo hili uone vitu gani watu watavihitaji.
 
Maramba mawili n wap mkuu nielekeze

Maramba mawili ni kama unaelekea Kinyerezi.
Ukitoka Mbezi ya Kimara Mwisho, unachukua barabara ya kwenda Kinyerezi mpaka Maramba mawili (kwenye junction) hapo unachukua barabara ya kulia mpaka sehemu inayoitwa King'azi (unaweza hata kutembea kwa miguu kutoka kwenye junction)
 
Maramba mawili ni kama unaelekea Kinyerezi.
Ukitoka Mbezi ya Kimara Mwisho, unachukua barabara ya kwenda Kinyerezi mpaka Maramba mawili (kwenye junction) hapo unachukua barabara ya kulia mpaka sehemu inayoitwa King'azi (unaweza hata kutembea kwa miguu kutoka kwenye junction)
You mean kwa matuta mzalendo sio
 
Miaka 5 mbeleni kutakuwa na biashara sana maeneno hayo.

Bila shaka umeme wameshamalizia kipande hicho kuweka.


Vipi na mradi wa Muhimbili ndogo unaendelea pande hizo?



Tarajia ugeni.
 
Back
Top Bottom