Milango ya bwawa la umeme, tani 26 kukodi wichi toka nje, ni kutupiga Watanzania na kitu kizito

Sasa hapa mbona unaanza kujifanya taahira wakati mimi najua for a fact wewe sio taahira?

1.)Unasema hujui nani kasema crane inahitajika, Kalemani na Makamba umeshawahi kuwasikia wakizungumza juu ya hilo bwawa na wakataja kuhusu kujaza maji, na Makamba akasema nini kuhusu kushindwa kujaza maji?

2.) Hapo kusema ujenzi bado mbona nimekujibu kwenye hiyo post uliyo-quote, kwamba bwawa linahitaji mwaka au zaidi ili kujazwa vya kutosha kabla kuweza kuzalisha umeme, hivyo hata ujenzi ukikamilika kwa 100%, tunaweza kujikuta tunakaa bila kuzalisha umeme kwa hata mwaka au zaidi kisa tu hakuna maji bado, ndio maana ujazaji wa bwawa unapaswa kuanza angalau mwaka kabla ya kukamilika ujenzi, ili ujenzi ukikamilika na maji ya kuzalisha umeme yawe yameshajazwa tayari.

Sasa mimi sielewi unajifanya taahira kwa faida ya nani zaidi ya kujidhalilisha tu.

Tuachane na hayo, crane la tani 26 tukikoambiwa na Makamba kwamba wanakodi nje ya nchi, liko wapi?
Mkuu sasa tunaigia ile inaitwa shadow boxing.
Nimekueleza facts zote lakini emeng'ang'ania crane!
Liachie utaanguka nalo, halafu halihitajiki.

Unaongelea Makamba na Kalemani, masuala ya kihandisi hao ndio unawaamini sana?
It s at your own peril!

Hao wanasiasa wako hawajui tofauti ya crane, hoist au hata lift!
Mini ni mjuzi na najua nilichokiona na kuelewa mantiki ya ujenzi uliopo Stiglaz.

Au tuseme kwa kifupi, mtu unabisha kwa vile ni mbishi, na hobby yako ni kubisha!

Hapo no reasoning can penetrate, kwa maana kumalizika ujenzi Stiglaz lazima crane la tani 26 lionekane, kama alivyosema Makamba na Kalemani!
 
Mkuu sasa tunaigia ile inaitwa shadow boxing.
Nimekueleza facts zote lakini emeng'ang'ania crane!
Liachie utaanguka nalo, halafu halihitajiki.

Unaongelea Makamba na Kalemani, masuala ya kihandisi hao ndio unawaamini sana?
It s at your own peril!

Hao wanasiasa wako hawajui tofauti ya crane, hoist au hata lift!
Mini ni mjuzi na najua nilichokiona na kuelewa mantiki ya ujenzi uliopo Stiglaz.

Au tuseme kwa kifupi, mtu unabisha kwa vile ni mbishi, na hobby yako ni kubisha!

Hapo no reasoning can penetrate, kwa maana kumalizika ujenzi Stiglaz lazima crane la tani 26 lionekane, kama alivyosema Makamba na Kalemani!
Ni kwanini bwawa halijaanzwa kujazwa hadi leo wakati linahitajika liwe limeshaanzwa kujazwa ili by the time ujenzi Unakamilika na bwawa liwe limashajaa maji tayari kwa kuanza uzalishaji? (Ukizingatia Maji huchukua hadi mwaka kujaa kwenye bwawa)
 
Inaonekana mwandishi ni Mjuzi wa haya mambo. Nadhani inhelikuwa vyema Mh. Waziri angeanzia pale kwenye mradi wenyewe kuona uwezo wa hizo mashine na kama ninkuagiza kuwe ni kamati ya huo mradi ndio watoe hilo pendekezo lakini yeye asiye chanzo.

Pili, ili kuondoa huo utata wangetangaza kandarasi hiyo ya muda mfupi kwa kampuni yeyote ya ndani yenye huo uwezo wa kuweka hiyo milango ili kuondoa hiyo sindofahamu. Lakini kama hapa nchini kuna mashine kubwa zaidi ya hiyo inayotoka nje kwa maelezo ya mtoa mada naona kufanya hivyo kutaonesha mashaka makubwa
 
MILANGO YA BWAWA LA UMEME, TANI 26, KUKODI WICHI TOKA NJE, NIKUTUPIGA WATZ NA KITU KIZITO

Watu wengi wameonekana kushangazwa na maelezo ya Waziri wa sekta husika baada ya kujibu hoja mbungeni kuhusu maendeleo ya mradi wa bwawa la umeme Lililopo kati ya Rufiki na Morogoro.

Ambapo Waziri alisema, Hatua ya kwanza ya kujenga ukuta imeishafanyika isipokuwa hatua ya pili ambayo nikuweka MILANGO YA CHUMBA YENYE TANI 26 ndiyo bado haijakamilika kwa sababu INASUBIRIWA CRANE (WICHI) YA KUKODI TOKA NJE YA NCHI KWA AJILI YA KUJA KUSETI HIYO MILANGO.

WAZIRI kama umeambiwa basi maelezo uliyoambiwa na unayotakiwa kuyatoa kwa umma wa Watanzania yalitaliwa kuwa na ufafanuzi mzuri na wenye kueleweka.

Haiwezekani Crane zilizoko ndani ya mradi wa umeme zishindwe kubeba mzigo wa tani 26. Wakati Crane ZILIZOKO KWENYE MRADI ZIKO ZENYE KUBEBA TANI 25, 50, 60, 90, 120 NA HATA 200

Waziri CRANE ILIYOPO KWENYE MRADI WA UMEME AINA YA XCMG (Total Mass: 36000 Kg Ukichomoa Boom Angle ya Lenght 10.3 na boom ikawa kwenye mlalo wa Mita 4 INAWEZA KUBEBA TANI 43.5, 53 na TANI 55 ILA ITAWAKA ALAMA YA NJANO KUONESHA NI HATARI

Crane XCMG 36000 Kg ikiwa na Counter weight 7.6 boom ikawa Mlalo wa 20.6 na radius ya Mita 3, Crane hii INAWEZA KUBEBA MZIGI TANI 26.0 HADI 27.6.


Hii CRANE ya kusubiriwa kutoka nje ya nchi ina uwezo gani wa ziada kuzidi crane zilizoko ndani ya mradi au ina maajabu yapi kuliko crane zilizopo.

Hii CRANE inayosubiriwa toka nje ni ya nani na inakodiwa dola ngapi kwa saa na itatumia siku ngapi?

Hii CRANE toka nje, itakuwa inaweza kubeba tani 26 na inaizidi vipi CRANE XCMG 56000 KG yenye kuweza kubeba tani 90.

Hii CRANE YA KUKODIWA ina maana inaizidi LIBBER CRANE ambayo inaweza kubeba TANI KATI YA 50, 90 na 120.

CRANE HII TOKA NJE INAIZIDI CRANE AMBAYO IKO KWENYE MRADI NA INAWEZA KUBEBA TANI 200 mbona kama nikuwapiga Watanzania na kitu kizito.

CRANE Toka nje inazizidi uwezo Crane Tower zote zilizoko kwa Mchina, Mwarabu, AFFCO na zinginezo, Hapana Mh, Waziri maelezo hayawaridhisha Watanzania.

Watanzania wa sasa wameishaelimika na wanahitaji ufafanuzi yakinifu ili kuwaridhisha.

#Usisahau like na share page yetu

#lakini pia Inawezekana pamoja na kuwa ni mdua wa page hii ungependa pia kunisapoti kupitia kampuni yangu kwa kuagiza Mchele toka Mbeya. Kama ni hivyo jiunge kwenye gruop la WhatsApp kwa kubofya link hii na utaagiza popote

Nimeikuta mahali:
Wala tusijiulize sana. Kama Tanzania Ridhiwani Kikwete ni naibu waziri wa wizara ngumu kama ya ardhi na January makamba ni waziri wa nishati. Watanzania tunasubiri kupigwa na kitu kizito mara ya ngapi. Saivi ni kugugumia tu maumivu.
 
Hahahah, huu ndio uzuri wa jukwaa, utaruka ruka weeee, ila unaingia nyavuni, hahah, haya sawa, ngoja nimuulize kwanza Makamba crane itakuja lini...
Mkuu tunafuatilia mabishani, tatizo lako wewe ni kukubali maneno yasiyi ya kitaaluma uliyolishwa na wanasiasa.
Jitahidi uwsulize ma crane yanayowezesha kupatikana umeme yalipo duniani.
 
Kwa hatua ulipofikia ujenzi wa tuta kuu tunaruhusiwa kuanza kuhifadhi maji (water emponding) isipokuwa hatujaanza kuhifadhi kwakuwa njia ya kuchepusha maji haijafungwa.

Ufungaji wa geti la njia ya kuchepusha maji lina hatua mbili.

1. Kujenga tuta kuu hadi kimo cha mita 95 kutoka usawa wa bahari. Kazi hii imeshakamilika

2. Kufunga mfumo ya kushushia mageti kwenye njia ya mchepusho wa maji. Mageti yalishafika ila mfumo wa kuyashushia unafika mwanzo mwa Januari 2022.
Mfumo ukikamilika kufungwa mageti yatashushwa, na tutaanza kuhifadhi maji.

Ni mfumo ambao ndani una crane na miundombinu wezeshi ya kutumia na kuendesha crane hizo. Crane hizo zinaitwa wire rope hoist crane zimaendeshwa kwa umeme sio hydraulic
Mkuu hata hizi wire rope hoist crane bado zipo nyingi tena humu humu Tz...

Mfano kwenye mining site za kahama zipo.

Ila kwakuwa ni mambo ya 10% ngoja tutulie.
 
Back
Top Bottom