ngoshwe
JF-Expert Member
- Mar 31, 2009
- 4,131
- 931
Mila nyingine Bwana!.
Mke wangu anatokea kabila fulani kusini wa nchi yetu. Sina uwezo wa kutosha kiuchumi, tunaishi nyumba ya kupanga (Bonyokwa). Nyumba inavyumba viwili na sebule ambapo pana kochi moja tu na TV. Nyumba ina choo cha ndani cha sink la kukaa na pia kuna bafu humo humo.
Katikati ya mwezi uliopita, Mama mkwe kaja toka kijijini kwa ajili ya matibabu ya miguu, inamsumbua sana, ana lala chumba kimoja na watoto wetu. Cha kusikitisha, nimeonana nae ana kwa ana siku moja tu tokea aje kwenye. Siku zote huwa nikitoka kumsalimia anaitika huko huko chumbani, hataki tuonane sura, jana naelezwa na watoto eti "bibi" huwa anaenda kuoga na kujisaidia nyumba ya jirani yetu na mimi ninapofika tu akisikia mgurumo wa gari kama yupo sebuleni ana kimbilia chumbani!
Nauliza kwa nini anafanya hivi, waifu ananiambia eti kwa mila za kabila lao, ni aibu/ fedheha na sio ruksa kabsaaaa kwa mkwe (mzazi wa kike wa mke wangu), kufanya haya:
Hizi mila nyingine mboni mateso kwa sie akina yakhe!...

- Kusalimiana na na mkwewe (yaani mimi) kwa kutazamana usoni au kushikana mikono.
- Kutumia choo au bafu analotumia mkwewe (yaani mimi).
- Kukalia kiti alichokalia mkwewe.
- Kupishana kwa karibu na mkwewe
- Kukaa sebule na kuangalia TV mkwewe akiwa hapo hapo.