Mila na utamaduni: Tanzania wanakozikwa watu wakiwa wameketi hadi Cameroon wanakopiga matiti pasi, angalia tamaduni za ajabu Afrika

MR LINKO

JF-Expert Member
Aug 20, 2016
3,034
3,480
Muacha mila ni mtumwa lakini kuna baadhi ya mila zinazoendelezwa Afrika ambazo ni nzuri na zinawafanya Waafrika kutambua urithi wao kitamaduni lakini nyingine ambazo zitakushangaza.

Baadhi ya mila hizo zimetajwa kama dhalilishi au zinazokiuka haki za kimsingi za binadamu.

Leo tunaangazia baadhi ya mila ambazo ni jambo la kawaida kwa jamii zinazozifuata lakini kwako huenda ukazichukulia kama za kushangaza.

Kuna nyingine ambazo zinapigwa vita na mashirika mbalimbali kama vile Umoja wa Mataifa kwa kuwa mila kandamizi na ambazo hazina nafasi tena katika karne hii.

Kaburi lajengwa kwa miezi tisa​

WAA


Katikati mwa Tanzania katika eneo la Hydom kuna jamii ya Barbaik ambayo hufanya mazishi ya heshima kwa wazee ambao mchango wao kwa jamii umetambulika.

Kinachofanyika ni kwamba mwili huzikwa ukiwa umeketi baada ya kufunikwa kwa ngozi ya ng'ombe.

Kaburi la Wazee hao ni la duara na linajengwa kwa miezi tisa kipindi hicho kinaashiriia muda wa miezi tisa ambacho ndio kipindi anachobeba mimba mwanaume.

Wanaamini kwamba mtu kama huyo hajafa bali atazaliwa tena.

Mazishi yenyewe hayafanyiki kwa kila mtu bali jamii na wazee wanaamua ni mtu yupi anayestahili kupewa maziko hayo ya heshima.

Mazishi ya usiku na wanaume pekee​

zulu


Katika jamii ya Zulu nchini Afrika kusini Mfalme akiaga dunia yeye huzikwa wakati wa usiku katika mazishi yanayohudhuriwa na wanaume pekee.

Mfano ni jinsi mfalme Goodwill Zwelithini aliyezikwa siku chache zilizopita baada ya kuaga dunia kutokana na virusi vya Corona .
Waziri mkuu wa kitamaduni wa Prince Mangosuthu Buthelezi aliliambia shirika la habari la SABC kwamba mfalme huyo angezikwa katika hafla ya kibinafasi wakati wa usiku kwa mujibu wa mila na desturi za jamii ya wazulu.

Na wakati wa mazishi hayo ni kundi maalum la wanaume kutoka nyumba ya kifalme ya Zulu ndio wanaoruhusiwa kushiriki katika mazishi hayo.

'Mwili kuzikwa ukiketi'​

mm


Huko magharibi mwa Kenya kwa kuhofia laana , wazee wa jamii ya Wabukusu waliamua kwenda kuifukua baadhi ya miili ya wapendwa wao na kuizika kwa 'njia inayofaa' kwa kufuata utamaduni wa jamii yao.

Kulingana na desturi za jamii hiyo kichwa cha mfu kinafaa kuangalia upande mbali na boma na vitu kama viatu ,shati , au tai vinafaa kulegezwa katika mwili wa marehemu.

Hilo lilifanyika wakati watu walioaga dunia kwa sababu ya Corona walipokuwa wakizikwa na maafisa wa afya.

Hatua hiyo ilichukuliwa ili kuzuia jamaa za walioaga dunia kuikaribia miili ya wapendwa wao wakati wa mazishi na ndiposa maafisa wa afya ndio waliopewa jukumu la kuizika miili yao.

Wazee wa jamii hiyo walisema Iwapo hilo halingefanyika inaaminika mtu aliyefariki anaweza kuitesa familia yake katika ndoto zao.

'Kupiga matiti pasi'​

Utamaduni au mtindo wa 'kupiga matiti pasi' ili kuyazuia yasiwe makubwa umekithiri Afrika Magharibi na hasa nchini Cameroon.

Wanaotekeleza hilo hudai kwamba hatua ya kuzuia kukua kwa matiti ya wasichana wanaoanza kubaleghe huwazuia wasichana wadogo kuwavutia wanaume na hivyo basi kuepuka dhuluma za kimapenzi lakini jambo hilo limetajwa na wanaharakati kama ukiukaji wa haki za wasichana na dhuluma za kijinsia.

Inafanywaje?​

Jiwe hutiwa katika moto kama kaaa kisha kupitishwa juu ya matiti kwa lengo la kuyapunguza.

Jane(sio jina lake halisi) alifanyiwa utamaduni huo miaka 18 iliyopita na shangazi yake ambaye alikuwa mtawa na alikuwa akiishi Cameroun wakati huo.

Alipokuja nyumbani kwa likizo alimpata Jane akiwa ameanza kuvunja ungo na matiti yake yameanza kujitokeza, yakionekana kupitia nguo yake.

Shangazi yake hakufurahia hilo na mara moja akamuambia mama yake Jane kuhusu hatari ya mwanaye kubakwa na wanaume na hivyo basi kulikuwa na haja ya kuyapunguza matiti yake.

Mama yake alishangaa hilo litafanywaje lakini shangazi yake kwa ajili ya kuwa mtawa aliheshimiwa sana pale bomani na kila alichosema kilikuwa sheria.

Alieleza jinsi utaratibu huo utakavyofanywa na muda sio mrefu-kila siku Jane alikuwa akivumilia takriban dakika 20 za uchungu wakati jiwe la moto lilipokuwa likiwekwa kifuani mwake ili kupunguza ukubwa wa matiti yake.

Wenzake shuleni walishangaa mbona alikuwa akilia wakati wote na kushika kifua chacke kwa uchungu.

Wengine kama rafiki yake wa karibu Stella alishangaa mbona hawakuwa wakioga pamoja kama awali bila kujua kwamba Jane alikuwa akificha alama katika kifua chake na kupungua kwa matiti yake kwa ajili ya uovu aliokuwa akifanyiwa na shangazi yake kutumia mila aliotoa Cameroun.

Alipokuwa msichana mkubwa kujiunga na chuo kikuu, Jane alijipata na matatizo ya kujiamini kwa sababu alijiona na kujihisi tofauti kama wasichana wenzake.

Wengine walikuwa wakimfanyia mzaha kwa kumuita 'mvulana' kwa sababu ya kukosa matiti bila kujua masaibu aliyopitia .
Jane hakuweza kumchukulia hatua yoyote shangazi yake kwa sababu uamuzi huo pia ungemuingiza taabani mamake ambaye alikuwa amekubali afanyiwe utaratibu huo.

Walimuambia wakati huo kwamba kila wanachofanya ni kwa manufaa yake bila kujua athari za kitendo hicho katika maisha yake ya baadaye.

Nchini Cameroun ambako utamaduni huo umekithiri, serikali na mashirika mbalimbali ya haki za binadamu yanapambana na wovu huo ili kuzuia mateso kwa maelfu ya wasichana.

Kupiga matiti pasi ni zimwi kama utamaduni wa kuwakeketa wasichana katika baadhi ya jamii Kiafrika.

Athari za kitendo hicho kwa Jane hazitaisha hivi karibuni na zinamuathiri hadi wakati huu katika maisha yake ya utu uzima .

Ukeketaji/Upasuaji wa sehemu za siri za wanawake​

ukeketaji


Ukeketaji wa wanawake umekuwa mojawapo ya mila ambazo zimepingwa sana katika sehemumbali duniani ikiwemo Afrika.

Mataifa kadhaa yamefaulu kuharamisha utamaduni huo lakini bado kunazo jamii zinazotekeleza utamaduni huo kisiri.

Ukeketaji unafanyika kwa njia mbali mbali kulingana na aina ya upasuaji ama oparesheni inayofanyiwa sehemu ya siri ya mwanamke;

Aina za upasuaji​

Tohara au Sunna ("jadi"): Hii inahusisha kuondolewa kwa ncha ya kisimi. Hii ndio operesheni pekee ambayo, kiafya, inaweza kufananishwa na tohara ya kiume.

Kutoboa sehemu za siri: Hii inahusisha kuondolewa kwa sehemu za siri, na mara nyingi pia labia minora. Ni operesheni ya kawaida na inafanywa kote Afrika, Asia, Mashariki ya Kati na Peninsula ya Arabia.

Tohara ya Mafarao: Hii ni operesheni kali zaidi, inayojumuisha uondoaji pamoja na kuondolewa kwa sehemu za siri na kushona.

Tohara au Sunna ("jadi"): Hii inahusisha kuondolewa kwa ncha ya kisimi. Hii ndio operesheni pekee ambayo, kiafya, inaweza kufananishwa na tohara ya kiume.

Kutoboa sehemu za siri: Hii inahusisha kuondolewa kwa sehemu za siri, na mara nyingi pia labia minora. Ni operesheni ya kawaida na inafanywa kote Afrika, Asia, Mashariki ya Kati na Peninsula ya Arabia.

Tohara ya Mafarao: Hii ni operesheni kali zaidi, inayojumuisha uondoaji pamoja na kuondolewa kwa sehemu za siri na kushona.
 
Back
Top Bottom